Madini ya Dhahabu Kilo 15.78 yenye thamani ya Tsh Bilioni 3.4 yakamatwa Bandari ya Boti Dar yakitoroshwa kwenda Zanzibar

Na wiki hii tutashuhudia mengi sanaaaa lengo tu tusahau unyama na ushenzi ila safari hii kazi wanayo msione ajabu zikavuja picha za uchi za mtu hapa ili mada ihame ila yana mwisho haya ,
Ni Wewe mwenyewe tu hakuna anaekushikia bundukI uache kuongelea swala fulani,na tatizo sio kuongelea just take an action,
Sio sifa kupiga ma kelele mitandaoni
 

Mali yaenda Unguja hii...imekuwaje?
 
Mbona hamuwataji? Acheni maigizo
 
Tukio hili limenikumbusha tukio la miaka mingi kidogo la madini ya dhahabu ya uzito wa tani 3.7 yaliyotelekezwa kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA)jijini Nairobi nchini Kenya.

Kutelekezwa kwa dhahabu hiyo kulitokana na kuanza uchunguzi wa ghafla wa madini yaliyoibwa DRC kuingizwa kisiri nchini Kenya, na kutiwa sokoni na kundi la waasi wa DRC waliopo Kenya.

Awali, dhahabu hiyo ilionekana kuwa ya Mkenya, Paul Kobia Kabebria, lakini akijipa jina bandia la Paul Ilunga Ngoei raia wa DRC, aliyemsaidia Pedro Del Campo, raia wa Uswiss na mume wa Nyasha Mujuru.

Nyasha Mujuru ni binti wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe, na aliyekuwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Solomon Mujuru, waliokuwa na kampuni ya uuzaji madini Ulaya, ya River Ranch Mines.

Lakini, kampuni hiyo ilipigwa marufuku kuuza madini Ulaya ilipobainika kuwa ikinunua madini ya waasi wa DRC, ikiwezesha ununuzi silaha. Ikumbukwe kuwa UN imepiga marufuku ununuzi wa madini ya waasi.

Familia ya Mujuru kwenye kampuni hiyo walikuwa na mshirika wa siri ambaye jina lake halitajwi kokote, lakini alikuwa ndiye big boss, kwa kisa chao kilivyo, nitamtaja baadaye.

Na baada ya River Ranch Mines kuwa kwenye marufuku hiyo, ndipo mume wa Nyasha Mujuru, Pedro Del Campo alipopewa jukumu la kuanzisha nchini mwao kampuni ya ununuzi wa madini ya Berline Equities Corporate.

Hivyo, kampuni hii ikawa ikinunua madini nchini Kenya wakimtumia tapeli, Paul Kobia, akitumia huo utamblisho bandia wa Paul Ilunga Ngoei na kujipa uraia wa DRC.

Ila baada ya Mamlaka ya Mapato ya Kenya (KRA), chini ya Kamishna wa wakati huo, Joseph Cheptarus, Kugundua madini yao ni sehemu ya madini ya waasi yaliyotoroshwa DRC, wakaweka mtego.

Mtego huo ulishtukiwa na Campo, naye akatelekeza dhahabu hiyo JKIA naye kuondoka Kenya kinyemela kwa kupitia Tanzania.

Lakini, hasara hiyo ya kutelekezwa kwa madini yao ilishindwa kupokewa na big boss wa kampuni ya akina Mujuru, na ikagharimu vifo vya watu kadhaa, akiwemo Cheptarus, Solomon Mujuru na zaidi, Joyce kupoteza umakamu wa Rais.

Ova
 
Siyo rahisi itokee tu from no where mtu abebe dhahabu kilo 15.78 aelekee kupanda Azam Marine. Vitu vingine tuwe tuanelezana ukweli tu. Tatizo la biashara haram ndo hilo task force watakunyua alafu mwisho wa siku wanakuuza ili wapande vyeo.
 
Hii ilifaa kuwa thead kabisa b… Kuna mambo kadhaa hapo nimetamani kuyafahamu kiundani. Unanijua napenda details, please ukipata muda.
 
Hii ilifaa kuwa thead kabisa b… Kuna mambo kadhaa hapo nimetamani kuyafahamu kiundani. Unanijua napenda details, please ukipata muda.
Ni kweli b..., tena hii story ni ndefu mno nimejitahidi kuifupisha, lakini bado iko nyingi sijaigusa. Kifo cha Cheptarus kilikuwa cha kutumiwa majambazi nyumbani kwake.

Ilikuwa ni patashika, mchongo ulikuwa umepangwa hadi akaletewa walinzi wa mchongo wa nyumbani kwake. Mletaji ni serikali ya Kenya. Solomon Mujuru aliteketezwa kwa moto akiwa shambani kwake.

Ova
 
Nimeogopa! Hata kama sio hapa basi naomba ikae katika list ya mambo yetu…
 
Madini yote Magufuli alitaka wafungwe na kusafirishwa na wakala wa serikali ambaye kama sijakosea alikuwa ni TASAC ili iwe rahisi kufanya tracking ...Huyu mzenji alipokuja akadanganywa wafanye kazi ile watu binafsi ndio maana kila siku kazi ni kukamata .

Juzi kati hapo yalikutwa kenya ,Wnaomshauri huyu Raisi wengi ni wezi tu .


Haya madini na nyara za serikali zirudi chini ya TASAC .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…