Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

I told you!
Kuna tatizo kubwa guys.

Wale wenye macho wanaona, wanye fikra za kuona mbali wanaona, wenye masikio wanasikia.
Wenye kukubali ushauri na ukosoaji wataanza kutuelewa tunaopiga kelele kuna tatizo sehemu ndani ya upinzani.

Siamini kama watu wote hawa wana nunuliwa.
Erythrocyte nilisikia Mbeya watu wenye msimamo hawanunuliki sasa hiki sijui ndio nini?!!!
'NASHINDWA KUSHANGAAA'.

Yaani wewe ndiyo kima kabisa, kununuliwa kwa wapinzani siyo lazima wapewe pesa mkononi, tatizo vichwa vyenu vipo na kamasi tu ubongo ulishatolewa kitambo! Hao wapinzani hawana tofauti na mijusi wa kijani pale lumumba. Kama hakuna tume huru uchaguzi hakuna, wagombea wote wa ccm watapita bila kupingwa yaani kwa 99.99%.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii haiwezi kuisaidia CCM as long as maisha ya watu yanazidi kuwa magumu.
 
Wanaamini kwenye kununua wanachama na viongozi sio kwenye kuinua maisha ya mwananchi..hii CCM ya Bashiru ni kitu kipya kbs.
ccm mnatia aibu sasa haina maana. kama mliogopa local gov elections hata za urais mtaziogopa sana ndiyo maana slave trade inaendelezwa na slowslow na sasa hata katibu ameingia kichwa kichwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli;

Dr Bashiru ndo katibu mkuu wa CCM aliepokea Wapinzani wengi kuliko makatibu wakuu wengine.

Na John Mnyika ndo katibu mkuu wa Chadema alieongoza kupoteza Wanachama wengi kuliko katibu yeyote yule aliyemtangulia.

Graph inaonyesha Dr Bashiru kawin hapo alipo
Na pia inaonyesha John Mnyika Alivyofeli vibaya mnoo.
 
Mazingira bora ya demokrasia si kudondosha vyama mbadala bali ni kuzijenga ili tupate mawazo tofauti.
 
Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
Unapomnunua meya na madiwani wakati bado miezi kama saba tunafanya uchaguzi. CCM hapa mnatumia akili au matope. Watakaoamua ni wananchi yaani kwakweli mnatumia vibaya pesa za wananchi badala ya kuwapa maendeleo mnatumia pesa zao kuwahonga. Mtashangaa October hao mliowahonga hawatapigiwa kura. Kwa Opposition ni bomba kwasababu wapo watakaopata nafasi kujaza nafasi zao. Ila kwa upande wa ccm wanaenda kugombana na wenye chama, hivyo Mbeya itazidi kuongozwa Opposition. Bashiru ni katibu mkuu wa kwanza kuwa muoga haijawahi tokea ndani ya ccm
 
Wananchi wanawaamini halafu mnawasaliti

Shubamiti!
 
Watanzania kwa sasa tunaogopa tuu virusi vya corona na sio hizo siasa zao za kuhama hama kama matahira
 
Madiwani Na Wabunge Wamevunja Rekodi Kuhama Kuliko Wanachama.Uongozi Chama Taifa Utowe Tamko Kinagaubaga Kwanini Madiwani Na Wabunge Wanatimka?Si Maneno Mepesi Tu
 
Back
Top Bottom