Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Madiwani 11 wa CHADEMA wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya wahamia CCM

Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
I
 
Sugu inabidi ajipange vizuri sana pale mbeya maana kwa udi na uvumba ccm wanataka kumpa jimbo tulia
 
Betina anatumia njia zote lakini Wanambeya watakushikisha adabu kama mwenzako Matilda...
 
I told you!
Kuna tatizo kubwa guys.

Wale wenye macho wanaona, wanye fikra za kuona mbali wanaona, wenye masikio wanasikia.
Wenye kukubali ushauri na ukosoaji wataanza kutuelewa tunaopiga kelele kuna tatizo sehemu ndani ya upinzani.

Siamini kama watu wote hawa wana nunuliwa.
Erythrocyte nilisikia Mbeya watu wenye msimamo hawanunuliki sasa hiki sijui ndio nini?!!!
'NASHINDWA KUSHANGAAA'.
Huamini Kama watu wote hawa wananunuliwa,ila unaamini watu wote hawa wanaweza kuacha stahiki zao baada ya kumaliza kipindi chao cha miaka mitano kwasababu ya kuunga mkono juhudi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sugu moto chini,
Rais wa Mbeya hawamwezi.
Hata kwa wizi wa kura bado ccm Mbeya hawatoboi.
 
Weka hisia pembeni, shauri nini kifanyike.
Acha kujiliwaza na hoja nyepesi, unaamini kabisa wale walishikiwa mtutu wa bunduki na kushurutishwa na vyombo vya ulinzi na usalama ulivyo vituhumu?

Au walipigwa mabomu ya machozi?
Unauliza majibu?sumaye alipokwa mashamba,mbowe walivunja bilicanas,lema alifungwa,sugu alifungwa.wapinzani woote wana kesi kisutu.lowasa mkwe wake siowi kapewa kesi.haya sasa ongea jingine.sembuse madiwani???
 
LESIRIAMU, Mkuu, haya mambo yote haya kunakitu kinatengenezwa kwaajili ya 2025, kuna mtu asali imemnogea anataka kuchonga mzingawake awe analamba mbaka uzeeni.

Biashara asubui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Titicomb,
Mimi ningeelewa na kukubaliana na hoja yako kama hawa wangehamia ACT, NCCR n.k. Lakini kitendo cha kurejea CCM inakuwa ni vigumu kuamini haya uyasemayo. Kama nia yao ilikuwa kuwatoa madarakani CCM, hawawezi kurudi tena hukohuko wakiamini kuwa malengo yao yametimia. Ni kweli kuwa CDM matatizo yapo, lkn nachelea kusema kuwa ndiyo sababu kubwa.

Tujipe muda, tutaona mengi hasa baada ya uchaguzi mkuu. CCM watashinda kwa zaidi ya 99% na wale waliorejea wachache watakuwa miongoni mwao na wengiwao watakosa. Sauti zao zitakuwa zimefungwa moja kwa moja na hakuna atakayekuwa na mahali pa kupazia sauti. Wakati huo watajisifu kuwa wameshinda na mambo yao na taifa letu kwa ujumla tutakuwa tunaimba wimbo mmoja!

Siku yaja, tutajiuliza mengi bila majibu, ila somo litakuwa limepatikana.
 
Madiwani 11 wa Chadema Halmashauri ya Jiji la Mbeya akiwemo Meya wa Jiji hilo wamejiuzulu na kuhamia CCM leo Jumatatu Februari 24, 2020.

Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally amesema kati ya Madiwani hao, 10 ni Madiwani wa Kuchaguliwa na Mmoja ni wa Viti Maalumu huku timu hiyo inayoongozwa na Meya ikiwa na Viongozi Watatu wa Juu wa CHADEMA.

Amesema kuwa Madiwani hao wanatoka katika Jiji la Mbeya kwenye Halmashauri inayoongozwa na CHADEMA na Mbunge wa Jimbo hilo ni Joseph Mbilinyi (Sugu) na kuwa huo ni ugeni mkubwa tangu aanze kupokea Wageni.

Aidha, amesema ameongea na Madiwani hao na kumueleza kwanini wanafanya uamuzi huo wakati huo na amefurahi sana maana kazi yake ni kuifanya CCM kutoa ushawishi na kupata wafuasi kila kona ya Nchi.
 
Nilishaapa, sintakaa nipige kura, hawa watu wanatuona sisi kama ng'ombe
 
Kwa sasa hiyo siyo habari tena maana tushajua nini kinaendelea chini ya kapeti, wacha waende maana wameshafika bei,

In God we Trust
 
Human trafficking is back strongly
BIG BOOM,

Viva JPM[emoji1241][emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
FB_IMG_1521609809883.jpeg

In God we Trust
 
Back
Top Bottom