GE2025 Madoga: Wafanyabiashara tutawafutia kodi zisizo na Msingi

GE2025 Madoga: Wafanyabiashara tutawafutia kodi zisizo na Msingi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Umasikini tulionao ni wakujitakia

------------

Mgombea ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chma cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Aisha Madoga, amesema chama chake kitalinda wafanyabiashara kwa kufuta kodi zisizo na msingi ndani ya siku 100 za kwanza kikipewa dhamana ya kuongoza.

Akizungumza kwenye kampeni kata za Mbambara na Matumburu Septemba 21, Madoga amesema hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira ya biashara na kupunguza mzigo wa ushuru kwa wananchi.

Amesisitiza pia kukuza zao la zabibu kwa kuongeza bei shambani na kuweka mikakati ya kuongeza thamani kabla ya kuingia sokoni.

Madoga ameonesha masikitiko juu ya vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na ukosefu wa huduma bora, akiahidi kushirikiana na Serikali kuhakikisha vituo vya afya vya kisasa vinajengwa katika maeneo hayo.

Aidha, amewataka wananchi wa Dodoma Mjini kuchagua viongozi wenye dira na maono, akisema CHAUMA imejipanga kuleta mageuzi ya kweli yanayolenga maslahi ya wananchi wa kawaida.


 
Back
Top Bottom