LGE2024 Madudu kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2024

LGE2024 Madudu kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2024

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Burure

Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
42
Reaction score
96
Jana tumepata wasaa wa kushuhudia Uchaguzi wa Serikali za mitaa tuliosubiria kwa muda mrefu. Licha ya kuwa umefikia idadi ya chaguzi Tisa (9) Toka uanze kufanyika hapa nchini lakini bado kuna Mapungufu makubwa.

Mosi ni msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni TAMISEMI ambaye na yeye anahusika kwenye kuchaguliwa maana ni CCM na wao.

Pili ni utaratibu wa kuandikisha wapiga kura. Hii ni njia mbovu na ya kizamani yaani tupo 2024 tunatumia madaftari kuandikisha wapiga kura kweli?

Tatu kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani tumeona Nchi nzima wagombea kutoka vyama pinzani ndio waliokosea pekee na waliotoka chama tawala wakipita kwa kuwa wao pekee ndiyo walipata Msaada wa wanasheria hii inawezekanaje?

Nne ni baadhi ya vituo kuona karatasi kuisha pamoja na kuchanganywa wagombea yaani kuweka wagombea ambao sio wa mtaa au kijiji husika ama kuchanganya majina ya wagombea kwa kuweka kwenye vyama tofauti (Mgombea wa CCM anakuwa yupo CHADEMA/ACT au Mgombea wa ACT anakuwa amewekwa CCM)

Mwisho na sio kwa muhimu KUPIGA KURA sio Maendeleo kwa Taifa Lolote.

Hivyo basi sisi kama Taifa yatupasa tutengeneze Mfumo wa chama kimoja Pamoja na kuweka Katiba mpya itakayomlinda RAIS asitoke Madarakani mpaka atakapochoka au kufariki (awe Mfalme Halisi)

Pamoja na kuunda Dira ya Taifa ambayo huyo Rais ataisimamia na kuitekeleza pindi anapokuwa yupo kwenye hicho Kiti

Maana itasaidia kuokoa gharama za uchaguzi hewa na rushwa lukuki tunazoziona kila siku (Iwe direct ama indirect corruption)

Wako Mtiifu,
Katika kujenga Taifa imara,
Burure.
 
Back
Top Bottom