Madudu ya upangaji mpya wa Alama za mitihani CSEE!

Madudu ya upangaji mpya wa Alama za mitihani CSEE!

Surgical Blade

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
349
Reaction score
16
Kwa kutumia mfumo
mpya ufaulu wa
Kidato cha Nne
mwaka jana
ungekuwa asilimia 94 Dar es Salaam.Wakati Mtihani wa Taifa wa
Kidato cha Nne nchi
nzima ukiendelea,
imebainika kuwa
madaraja na alama
mpya za ufaulu kwa shule za sekondari
zilizotangazwa na
Serikali hivi karibuni ni
tofauti na zile
zilizopendekezwa na
Kamati Maalumu iliyoundwa kuchunguza
suala hilo pamoja na
zile zilizotolewa na
makundi mbalimbali
yaliyoshiriki kuandaa
mfumo huo mpya. Mbali na kwenda
kinyume na maoni
hayo, alama hizo
zinaifanya Tanzania
kuwa nchi ya kwanza
duniani kuwa na viwango vya chini vya
ufaulu. Alama hizo
zilizotangazwa na
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Profesa Sifuni
Mchome zinaonyesha kwamba: A=75-100, B
+=60-74, B=50-59,
C=40-49, D=30-39,
E=20-29 na F=0-19,
huku alama endelevu za
upimaji wa mwanafunzi shuleni
(Continuous
Assessment-CA) ikiwa ni
40 na mtihani wa
mwisho ukichangia
alama 60. Kabla ya Serikali
kutangaza alama hizo
mpya, Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi
iliunda Kamati Maalumu
iliyopewa jukumu la kufanya uchunguzi na
kuja na mapendekezo
ya viwango vipya vya
ufaulu na utaratibu wa
CA. Kamati hiyo ilifanya
kazi hiyo na kukabidhi
ripoti yake wizarani
Septemba mwaka huu
na mapendekezo yake
kwenye upangaji wa alama hizo ilikuwa ni
A= 80-100, B= 70-79, C=
50-59 D= 40- 49, E= 35-
39 na F= 0-34 huku
wakitaka CA iwe alama
25. Baada ya kuandaliwa
kwa ripoti hiyo, Serikali
ilitafuta maoni zaidi
kutoka kwa wadau
wengine kupitia
makundi mbalimbali ambayo nayo yalitoa
mapendekezo. Kundi la kwanza
lililotoa mapendekezo
yake ni Jukwaa la
Taasisi za Elimu za
Serikali ambalo lilitaka
ufaulu uanzie alama 40, kundi jingine ni Vyuo
vya Watu Binafsi
ambalo lilipendekeza
ufaulu uanze alama 35
huku Wakuu wa Vyuo
vya Serikali na Wakaguzi Wakuu wa
Kanda wakitaka ufaulu
uanzie alama 40 na CA
iwe 30. Ofisa mwandamizi
kutoka Baraza la
Mitihani la Taifa (Necta),
ambaye aliomba jina
lake lisitajwe gazetini
alisema kitaalamu CA hutakiwa kuwa chini ya
alama ambayo
inahesabika kuwa ndiyo
ufaulu. Alisema baada ya
Serikali kupitisha
mfumo ambao ufaulu
unaanzia 20, ilitarajiwa
CA kuwa chini ya 19
badala ya 40 iliyopitishwa na wizara. Ufaulu wa chini Kwa mujibu wa kitabu
kinachoonyesha
viwango vya ufaulu
duniani kila mwaka cha
International
Qualification, baada ya Tanzania kutangaza
alama hizo mpya, sasa
inakuwa nchi
inayoongoza duniani
kwa kuwa na alama za
chini za ufaulu.
Mwananchi
 
jamani kwani na za advance zimebadilika?kwa sababu nasikia 2 watu wakisema zimebadilika lakini ushahidi hawatoi,sasa mwenye kujua anifahamishe
 
Tupeni na ufafanuzi wa six kama kuna mabadiliko
 
Katika utaratibu huu mpya si yote ni mabaya. Mpango huu ni WIN WIN kwa wote na unaongeza wigo mrefu kwa wale wanojua toka awali wanataka kufanya nini baada ya kumaliza masomo yao.

Kwa mfano, kwa utaratibu wa zamani kama kijana kapata kidato cha nne, Fizikia-C, Kemia-C, Baioloji-B, Hisabati-D, Civics-D, Kiingereza-F, Kiswahili-F. Huyu anapoint 26 dv 4. Kwa sheria za NECTA hawezi kuendelea na masomo A level. Lakini mwingine atayepata kiswahili D katika mtiririko huo atakuwa na Point 25 div 3 na kwa kanuni za Necta atachaguliwa kwenda A level.

Lakini hawa wanafunzi wawili watapokutana A level (PCB) wote ufaulu wao ni sawa yaani fizikia-C, Kemia-C na Baioloji-B) Hivyo kuwa na uwezo wa kimasomo sawa. Hakuna kilichoshuka hapa.

Nani ni mshindi katika hili? Ushindi ni kwa shule zile zitazojiona zinaupungufu wa walimu wa masomo fulani na kuwaelekeza wanafunzi wao wasome kikombi zaidi kwa kulenga lengo kuu la kujua watafanya kazi gani baada ya masomo.

Utaratibu huu kimsingi si mpya baadhi ya vyuo vikuu umekuwa ukiutumia katika kuchagua wanafunzi kuanza mwaka wa kwanza. Kwa mfano kwa wanafunzi wa udaktari waendao Bugando, KCMC, Kairuki n.k Katika masomo ya msingi yaani PCB, vyuo hivyo vyote vimeitupilia mbali Fizikia na unaweza kuingia kwenye kozi hiyo hata kama Fizikia umepata "F". Ni Muhibili univ tu ndio imekazania Fizikia kuwa uwe na min "E".

Hali hii tutaendelea kuiona katika vyuo vingi kwani mfumo wetu wa elimu umewabebesha mzigo mzito sana wanafuzi hata masomo yasiyo na lazima. Soko la kazi ndio muamuzi, na vyuo ndio watayarishaji wa mwisho wa wanafunzi kuelekea kazini.

Ni kihitimisha napenda kusema tu kuwa mfumo wetu wa elimu unahitaji mabadiko makubwa sana yanayoendana na wakati. Hata yaliyofanyika ni madogo bado tuna safari ndefu. Tujifunze toka kwa wenzetu.
 
Madudu yamekuwa ndiyo utamaduni wa kawaida wa Wizara ya elimu. Yaani mchana kweupe wanataka kulegezamashwarti kiasi ambacho waliochora Zombi 2013 wangeweza kufaulu kwa asilimia 93? Ama kweli nchi hii ni ya miujiza
 
Back
Top Bottom