Maduka ya kuuza madini ya Almasi yanapatikana wapi

Maduka ya kuuza madini ya Almasi yanapatikana wapi

Grena

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
656
Reaction score
1,553
Habari zenu wakuu,

Nina rafiki yangu kutoka nje, anatafuta madini ya Almasi sio kwamba anataka mengi lakini vijiwe tu kadhaa.

Kiukweli Mimi si mjuaji wa Mambo ya madini. Nahitaji kufahamu kwa yoyote anayejua maduka wanayouza Almasi ama ambako madini hayo yanapatikana. Sehemu ambayo upatikanaji wake ni uhakika na salama sio matapeli.
 
Dar Kuna maduka ya Vito vya almasi.ukitaka almasi isiyochongwa ni Shinyanga huko maganzo n.k.
Hapa Dar Kama unataka kuuziwa vipande vya chupa karibu.
 
Asante Sana Mkuu.. Lazima shinyanga tu, Dar Hakuna upatikanaji wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Dar kwa special order ,mtu anaweza kuja nazo toka huko Shinyanga.kuna mwaka niliwai pata msaouzi Africa alikuja hapa Dar...ila Biashara tulifanyia SEAMIC Kule Kunduchi. Baada ya kupimwa hayo mawe na kujiridhisha kuwa sio vipande vya chupa🤣🤣🤣
 
Dar Kuna maduka ya Vito vya almasi.ukitaka almasi isiyochongwa ni Shinyanga huko maganzo n.k.
Hapa Dar Kama unataka kuuziwa vipande vya chupa karibu.
Hahaha, Asante Mkuu. So lazima niende Shinyanga.

Na huko Kama mtu sio mjuaji wa Mambo ya madini hali ni vipi, ntakuaje na uhakika kwamba siuziwi vipande vya chupa ??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Sana Mkuu.. Lazima shinyanga tu, Dar Hakuna upatikanaji wake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Dar sina uhakika....Ila shinyanga hasa Maganzo Nina uhakika ila nyingi zinakuwa bado hazijachongwa....sio lazima uende....mnaweza mkafanya mawasiliano nao...wao wakakufuata ulipo...ila inabidi uwe makini sana kwenye biashara ya madini...la sivyo utanunua hata chupa.
 
Back
Top Bottom