Niende kwenye hoja!
Yamekuja maelekezo ya kusainisha waalimu mkataba ambao unamtaka kila mwalimu kufaulisha somo lake kwa asilimia 100. Hakuna mwanafunzi kufeli mtihani wa somo lake! Na kufeli kwao inaanzia B na sio F kama baraza la mitihani linavyo elekeza!
Je, Sikuhiz mwalimu ana sign mikataba miwili ya ajira?
Nimarufuku kutype scheme of work na lesson plans na kwamba zoote ziandikwe kwa mkono,
yaani wakati dunia inaenda digital, ilemela mwalimu anarudishwa analog, badala ya kusimplyfy kaz kuserve muda ili utumike pengine kuboresha taaluma tunaicomplicate kazi ili kumkomoa mwalimu[emoji854] kwamba hata notisi (nukuu) ziandikwe kwa mkono nimarufuku kukutwa na typed notse!
Sasa mpango kazi wa mwalimu uandikwe kwa mkono, je sylabus inayomuongoza mwalimu kuandaa mpango kazi huo husika kwanini wizara haijaziandaa sylabus hizo kwa mkono? Vipi kuhusu mithani pia wanayotunga waalimu kwanini nayenyewe kuanzia sasa wasiandike kwa mkono?? Tuachane kabisa na habari za kutype?? Turudi in 1990s?
Kwamba Mwalimu atoe majaribio mawili na maswali matano kila siku kwa wanafunzi woote.
Kwa wastani tuchukulie form one na two wanamasomo tisa so 9×5 = 45 hayo ni maswali kwa siku
45 × 5 = 225 hayo ni maswali kwa wiki!
Sijaenda form three na four, je hii imezingatia idadi ya wanafunzi kwa shule husika! Kuna shule form one wako 450 mpka 600 , kiuhalisia kuna mtu unaweza kusahisha maswali 225 kwa watoto 450 mpaka 600 kwa wiki, na bado uandae lesson plan kwa mkono??[emoji854] Na utambue weknes za watoto na kuwasaidia??
Nyie mlisoma hivyo? Je Mmewafikiria hawa watoto pia lwamba wafanye maswali 225 kwa wiki?? Na mnaona kabisa hilo ni archivable?
Kwa waalimu wa vidato vya pili na nne, mwalimu anapaswa kuotea ufaulu wa watoto, yaani mwalimu atabili ufaulu wa watoto wake anao wafundisha kwa mwaka, na nimarufuku kuweka utabili daraja C WOTE WAANZIE 'B' mpaka A! Hutakiwi kutabiri watoto watapata C, D na F [emoji23]
So skuiz waalimu wanabeti kuhusu ufaulu wa watoto? Mwisho wasiku shule zikifanya udanganyifu kama pale thaqhafa mta shangaaa?
Kwamba Mwalimu anapaswa fanya kazi kwa muda wake binafsi yaani muda wa ziada bila kudai fedha ya kazi ya ziada[emoji23][emoji23] na anapaswa kuwa na maswali 100 ya kuwapa wanafunzi [emoji23][emoji23] hivi hili hata kwenye sheria ya kazi linakubalika?
Sasa hii ni mikakati ya kuinua taaluma au ni mikakati yakuonekana mnainua taaluma. Nafikiri kunayo laana flani kwenye hii kada!
Kila mtu ni boss wa mwalimu
Kila mtu anauwezo wa kuwapa maelekezo waalimu!!
Na Je huu ndio msimamo wa nchi nzima kuhusu ELIMU? na je Upo waraka unaoelekeza haya?
Wahusika mpo tazameni haya! Kama mnaona yapo sawa haina shida!!