Mussa Dan Luca Mayagila
New Member
- Jul 1, 2024
- 2
- 3
''Usipoteze machozi ya leo kwa huzuni ya jana, dhambi ya zamani inatupa kivuli kirefu"
...................................................................................
Kisiwani Throne Palace
001 Kisiwani Ave st, Kisiwani.
Askari huyu aliekua na chevroni (V) mbili pembeni ya bega la kulia kuashiria ni 'koplo" alisomama katikati ya barabara hii na kunyosha mkono wa kulia juu ishara ya kuutaka msafara huu usimame, ishara hii ambayo kijeshi ni amri ilitekelezwa kikamilifu.Kisha kwa mwendo wa kikamanda alizitupa hatua zake hadi kwenye mlango wa dereva gari ya katikati ambapo kioo kiliteremshwa akatazamana na jamaa aliyevaa suti nyeusi, shati jeupe na tai nyeusi alietoa kitambilisho na kumkabidhi.Akakitazama kwa sekunde kadhaa Kisha akapiga hatua moja na kusimama kwenye mlango wa nyuma.Kioo kikashushwa akatazamana na mwanaume aliyevaa koti la kijivu shati jeusi na miwani myeusi, akampigia saluti kisha kioo kikapandishwa akarudi mlango wa dereva na kumrejeshea kitambilisho halafu akatoa ishara ya dole gumba kuelekea getini.
Geti hili lililofunguka kielektroniki kutoka kushoto kwenda kulia likaupa fursa msafara huu kuingia, baada ya kuingia wakatembea mita mia mbili wakivipangua viunga vya nyasi za kijani kibichi kushoto na kulia kabla ya kulifikia geti kuu la kuingia ndani ya ikulu hii ambapo hapa walisimana kwa sekunde kadhaa geti likafunguliwa kielektroniki kutoka kushoto kwenda kulia, wakaingia na kupita kwenye handaki fupi lenye urefu wa mita tatu na kutokea upande wa pili ambapo walikutana na mzunguko waliouzunguka na kukunja kulia wakatembea mpaka kwenye jengo la ''Maegesho Block" ambapo geti jeusi lilifunguka lenyewe gari zote zikiingia na kwenda kuegeshwa kwenye egesho namba 39 milangoya gari mbili ikafunguliwa wakashuka watu nane waliovaa suti nyeusi na masikioni vifaa vya mawasiliano huku kifuani kushoto kwenye mifuko ya makoti yao vilining'inia vitambulisho.
Mlango wa mbele kushoto wa gari ya katikati ulifunguliwa akateremka askari aliyevaa kombati zenye mabaka rangi ya khaki, daki-grini na nyeusi.Kifuani kushoto juu ya mifuko alikua na utepe wa kijani wenye maandiahi ya dhahabu ''MCPSPU" na juu ya utepe huu alikua na beji ya ''Golden Beret" maadufu kama ''bawa" kuashiria ni askari kutoka kikosi cha weledi maalumu, halafu kulia jina ''RODGERS K.R" , pembeni ya bega la kushoto bendera ya taifa na pembeni ya bega la kulia kulikua na nembo ya idara ya ulinzi wa makamanda wa kijeshi na watumishi wa umma, ya ''MCPSPU" halafu juu ya mabega alikua na nyota mbili kila upande kuashiria ni afisa mdogo cheo cha Luteni.Kichwani kofia rangi ya damu ya mzee.Alitupa macho kushoto kisha kulia na kwenda kufungua mlango wa nyuma ambapo akashuka bosi wao wanaemlinda.
Alikua ni mwanaume mtu mzima mwenye sura ya kitanashati lakini yenye mikazo ya kindava, umri kati ya miaka 48 hadi 50 kavaa suti ya kijivu aina ya Taupe Roma na shati jeusi nguo zilizolificha umbo lake kakamavu lililojengeka kwa ratiba nzuri ya mazoezi.Mkono wa kushoto alivaa saa aina ya kimedani aina ya 'SUUNTO CORE" chini viatu vya ngozi rangi nyeusi.Walinzi wanne walitangulia mbele na wanne nyuma katikati alikua yeye na mlinzi aliyevaa kombati za kijeshi, wakatembea mpaka kwenye mlango wa kutokea eneo hili wakaufungua na kuingia.
Wakatokea kwenye ukumbi maalamu mfano wa sebule ambaoulikuwa na maafisa kadhaa kutoka idara nyeti za ulinzi walioketi kwenye masofa wakipiga soga, wakitazama to runinga na kusoma magazeni huku wakipata vikombe vya kahawa, chai au maziwa kila mtu na alichohitaji.Kuingia kwao hapa kukawalazimisha walinzi wote nane kwenda kwenye masofa yaliyokua upande wa kushoto kutoka mlangoni halafu bosi wao na afisa huyu wakaenda kwenye dawati la mapokezi.
''Habari za asubuhi mheshimiwa?" Binti moja kati ya watu waliokuwepi hapa akamtupia salamu huku akimpa kitabu cha kusaini wageni.
''Salama, hamjambo?" Alijibu.na kupokea kalamu akasaini haraka haraka na kuondoka wakienda kwenye mlango uliokua kando ya mapokezi mbele wakiongozwa na afisa usalama aliyekuja kuwapokea.
Wakaingia kwenye korido ndefu yenye milango kadhaa kushoto na kulia waliyoipita hadi mwisho, wakakunja kushoto na kuingia kwenye ukumbi mdogo ambao kama kule walikotoka hapa waliwakuta watu wengine wa usalama wawili wakipiga sogo na wahutasi wawili waliokua kwenye meza ya mapokezi.
''D -01"
''Naam mkuu" Afisa moja kati ya wawili hawa aliitika halafu akainuka na kumfuata ''Wapeleke hawa" Akaondoka kurudi alikotoka na wageni hawa.
''Sawa mkuu"
Akaenda kwenye meza ya mapokezi alikokabidhiwa funguo halafu akawafuata wageni wake''Naomba mnifuate" Hakuna aliyetia naeno zaidi ya kumfuata ambapo waliifuata milango ya vioo na kutoka nje wakaifuata gari ndogo aina ya Audi A4 Security nyeusi yenye namba za usajili ''DG - CNBB FCC " iliyokua mbele ya ngazi za mlango huu.Dereva aliingia upande wake halafu Luteni huyu akamfungulia bosi wake mlango wa nyuma akaingia na kuufunga halafu yeye akaenda kuingia mlango wa mbele kando ya dereva aliyeondoa gari hii upesi.
Kiutaratibu mgeni yeyote anaeingia ikulu gari yake huishia katika jengo hili la Maegesho Block halafu kutoka hapa gari maalumu zitamchukua na kumpeleka sehemu anayoenda kama ni Eastern Point zilipo ofisi za rais, makamu wa raisi, first lady na second Western Point zilipo kumbi za mikutano vikao na ofisi za watumishi wa ikulu, Southern Point yalipo makazi ya familia za rais, makamu na wageni au North point yalipo majengo ya maktaba, makumbusho na ofisi za The Guardian.Walipitoka hapa kwenye jengo la Maegesho Block waliingia barabarani na kwenda umbali wa mita mia hamsini Hadi kwenye mzunguko ambao ulizikutanisha barabara nne wao waliuzunguka na kupitiliza mbele wakiifuata barabara ya Eastern Drive.
Wakavipita viunga vya nyasi na maua na miti ya hapa na pale iliyokatwa na kutunzwa vizuri ili kuipa mvuto mandhari ya ikulu, wakayapita majengo meupe ya ghorofa mbili yaliyokua upande wa kushoto na kulia.Mita mia mbili mbili wakakutana na mzunguko mdogo ambao waliuzunguka na kunyooka Hadi kwenye jengo ambalo mbele yake kulikua na jengo la ghorofa mbili kwenye mlango wa kuingilia ndani kukiwa na maandishi ''PRESIDENT OFFICE" (Ofisi ya rais), ilienda kusimama hapa na afisa huyu aliteremka na kwenda kufungua mlango wa nyuma, akateremka bosi wake.
Wakatembea taratibu wakavipita viunga viwili kushoto na kulia mpaka kwenye ngazi tatu walizozipata na kuifikia veranda fupi wakakutana na watu watatu waliovaa suti nyeusi na vitambulisho waliowapokea kwa salamu za kuishikana mikono kisha wakawaongoza kwenda ndani.Safari ya mlinzi huyu ikaishia hapa ambapo alipelekwa kwenye ukumbi maalumu na mmoja wa wanawake wawili waliokuwepi kwenye kaunta ya mapokezi wakati bosi wake akielekea kwenye ngazi wakapanda mpaka ghorofa ya pili na kutokea kwenye korido ndefu na fupi yenye milango miwili kushoto na mitatu kulia wao wakaingia mlango wa pili kulia ambapo nje waliwakuta walinzi wawili waliosimama kushoto na kulia.
Ukumbi huu mdogo katikati uliokua na meza ndefu ya mstatili kushoto na kulia kulikua na viti vinne vya kuuzunguka vyenye hadhi ya kibosi halafu mbele kiti kimoja ambacho kwa wakati huu kulikua kitupu!Kabla ya kuketi kwenye kiti hiki alisalimiana na watu aliowakuta katika namba ambayo wasiomjua walishangaa lakini wengine waliomgahami waliichukulia kawaida tu, Naam aliwaputishia salamu ya kimtaani kwa kukunja ngumi na kuwapa wagonge.
''Habari za asubuhi wakubwa?"Akawatupia salamu baada ya kumaliza kugonga Tano kwa wote saba ''Salama!...nzuri!...safi!" Wakatofautiana namna ya kujibu ingawa wote walijibu kwa wakati mmoja.Baada ya salamu hii akaketi kulia kiti cha mwisho kulia na kukamilisha idadi ya watu nane na sasa alingojwa mtu mmoja tu.Kimya kilikua kimejitangazia jamuhuri ukumbini hapa kila mtu aliwaza lake, na yeye alipoketi alianza kuwatupia macho ya kishushushu aliowakuta ili kujaribu kujua wito huu alfajiri hii ulihusu nini?Hili angeweza kubashiri kama angejua aina ya watu waliopo hapa!Akatumia dakika nzima kuwasoma nyuso zao.
Kushoto waliketi waziri mkuu, katibu mkuu kiongozi, mkuu wa serikali za majimbo na waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za majimbo, mikoa na serikali za mitaa.Kulia waliketi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la taifa, mkurugenzi wa shirika la usalama wa taifa, mkurugenzi wa idara ya ulinzi na usalama wa makamanda wa kijeshi na watumishi wa umma pamoja na yeye mkurugenzi wa idara ya ujasusi jeshini.Kwa jinsi ambavyo nyuso zao zilitawaliwa na wasiwasi aliamini Kuna jambo halipo sawa, kabla hata hajaanza kuulazimisha ubongo wake ufanye kazi mara mbili hadi mara tatu ya uwezo wake ili kumpatia bashiri juu ya ajenda ya wito huu mlango wa ukumbi huu ukafunguliwa na kuingia wanaume mrefu na mwembamba kiasi mwenye kitambi cha pesa aliyevaa suti ya daki blue, shati jeupe bila tai chini viatu vyeusi na mkono alishika faili jeusi akaja mbele ya meza hii na kuwafanya wote wasimame Kisha wakaketi baada ya mwanaume huyu kuketi.
''Habari za asubuhi waheshimiwa viongozi?Ni matumaini yangu mlikotoka mambo ni shwari, sio?"
''Ndiyo mheshimiwa"
''Naomba nijikite kwenye hoja ya msingi kuokoa muda maana nina ratiba ngumu sana leo," Wakatikisa vichwa kutoka chini kwenda juu kisha kurudi chini ishara ya kukubaliana na alichokisema.
''Nahitaji kubadili muundo wa serikali yetu" Akaanza na kunyamaza akatazama muitikio wa wajumbe hawa ambao waliokua wakimtazama, hakuna aliyetia neno hii ikamfanya aendelee ''Magavana wamepewa nguvu kubwa mno kikatiba kiasi cha kugomea mamlaka yangu halali niliyopewa kisheria.Nimefikia uamuzi huu sababu nimechoshwa na vitendo vya baadhi yao kupingana na maono yangu bila sababu za msingi na jeuri hii wanaipata kwenye katiba"
''Nahitaji waondolewe nguvu ya kugomea teuzi za wakuu wa mikoa na wilaya vilevile makatibu tawala wateuliwe na rais na sio wao.Pili magavana wateuliwe na rais ili kupunguza gharama za chaguzi"
''Unahitaji sisi tufanye Nini mheshimiwa?"Waziri mkuu akahoji.
''Nahitaji mnisapoti katika hili, nitawapa mtakachohitaji na katika serikali yangu ya muhula wa pili sitawaacha" Akaongea kwa msisitizo wenye kumaanisha halafu ''wangapi mko tayari katika hili?"
Watu wote wakanyoosha mikono juu isipokua mkurugenzi wa idara ya ujasusi jeshini ''Kanali Edu wewe hauko tayari kunisapoti katika hili?"Akahoji kwa sauti yenye ukali kiasi huku akimtazama kwa macho yaliyotangaza vita!Watu wote wakamtazama mkurugenzi huyu kwa macho yenye kuuliza wakichukizwa na kitendo hicho maana ataharibu mambo.
''Ndiyo sikubaliani na jambo hili,"Kwa kujiamini alijibu na rais akakasirika kabla ya kubwata
''Kwa nini?"
''Halina maslahi kwa taifa, litasababisha migogoro isiyo na ulazima.Nakushauri achana na hili kwa usalama wa utawala wako"
''Hiyo sababu yako haina mashiko!Toa sababu nuingine"
''Hili ulitakalo ni kwa maslahi yako binafsi, aliekushauri hivi hakutakii mema.......usijifikirie wewe hata kama una nia njema je, watakaofuata baada yako watalitumia kwa nia njema?"
''Hebu kuwa muwazi?" Waziri mkuu akadakia
''NASEMA HIVI HUU UJINGA SIKO TAYARI KURUHUSU UTOKEE"
''Whaaaaat!!?"
...................................................................................
Mussa Dan Luca Mayagila
The Great Industrious
There is a story in everything.
...................................................................................
Kisiwani Throne Palace
001 Kisiwani Ave st, Kisiwani.
Msafara wa gari tatu aina ya Toyota land cruiser V8 zenye namba za usajili ''CNBB FCC 01" ziliiacha barabara hii ya Kisiwani Drive na kuchepuka kulia zikiingia barabara ya Ikulu-Rd baada ya kuuzunguka mzunguko wa Kisiwani round about.Kutoka hapa zilitembea umbali wa mita hamsini Hadi kulifikia geti la ikulu na kusimama.Hazikusimama kwa matakwa yao bali mkono wa askari aliyevaa buti nyeusi, kombati ya rangi ya khaki yenye mabaka ya rangi nyeusi, daki-grini na kahawia.Mkononi livaa glovu za kimedani na kuishika bunduki aina ya The IMI Galil Arm- Assault rifle.Alivaa vesti ya kuzuia risasi kifuani ikiwa na magazini nne, mbele ya bega la kushoto simu ya upepo aina ya 'RMV 2080-Walkie Talkie" na sikioni alikua kavaa ''Conambo Bluetooth" na kiunoni alikuwa na bastola Beretta M9, kichwani kofia rangi ya damu ya mzee yenye nembo ya jeshi la wananchi wa Blackland.Askari huyu aliekua na chevroni (V) mbili pembeni ya bega la kulia kuashiria ni 'koplo" alisomama katikati ya barabara hii na kunyosha mkono wa kulia juu ishara ya kuutaka msafara huu usimame, ishara hii ambayo kijeshi ni amri ilitekelezwa kikamilifu.Kisha kwa mwendo wa kikamanda alizitupa hatua zake hadi kwenye mlango wa dereva gari ya katikati ambapo kioo kiliteremshwa akatazamana na jamaa aliyevaa suti nyeusi, shati jeupe na tai nyeusi alietoa kitambilisho na kumkabidhi.Akakitazama kwa sekunde kadhaa Kisha akapiga hatua moja na kusimama kwenye mlango wa nyuma.Kioo kikashushwa akatazamana na mwanaume aliyevaa koti la kijivu shati jeusi na miwani myeusi, akampigia saluti kisha kioo kikapandishwa akarudi mlango wa dereva na kumrejeshea kitambilisho halafu akatoa ishara ya dole gumba kuelekea getini.