Maelekezo kwa wanaoifahamu Dodoma

Kaluluma

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
468
Reaction score
619
Ndugu zangu, naombeni maelekezo ya siku za minada kwa Dodoma na sehemu inakopatikana hasa Vijijini na jinsi ya kufika ukitokea Sabasaba Stand. Namaanisha Minada ya vitu kama nguo n.k.

Itafaa kama nitapata ratiba ya wiki nzima na mahali mnada unapokuwepo.

Natanguliza shukrani
 
Ndugu zangu, naombeni maelekezo ya siku za minada kwa Dodoma na sehemu inakopatikana hasa vijijini na jinsi ya kufika ukitokea Sabasaba stand.

Namaanisha minada ya vitu kama nguo n.k. Itafaa kama nitapata ratiba ya wiki nzima mahali mnada unapokuwepo. Natanguliza shukrani
 
Kila jumamosi kuna mnada msalato A, usafiri - panda daladala za msalato zipo 77

Kila j2 kuna mnada veyula, usafiri- panda daladala za veyula zipo 77

Kila Alhamisi kuna mnada msisi,
Usafiri - unapanda gari zinazoenda mchito, lamaiti unashukia msisi magari yapo chang'ombe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Minada mingi ya Dodoma Vijijini bora kaanzie Independence karibu na soko la Majengo
pale mpaka mibada ya Usandawe, Kiteto, Lamaiti na Wilaya zinazoizunguka Dodoma utaipata palepale
km uko stendi ya Sabasaba panda Daladala ikupeleke Majengo shukia Independence
 
Au nenda mnada maarufu wa nyama na wanyama Kigwe Kila Ijumaa...77 panda magari yanaenda Mnada Mpya...ukifika hapo,unachukua ya Kigwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…