Maelekezo ya mabasi ya abiria kukaa stendi za wilaya na Mikoa watu wale na kupata huduma ya maliwato yanatekelezeka?

Maelekezo ya mabasi ya abiria kukaa stendi za wilaya na Mikoa watu wale na kupata huduma ya maliwato yanatekelezeka?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Naona Kama nchi Sasa inakopelekwa si kuzuri, kila Jambo analoona Waziri au kiongozi wa chama linakuwa sheria. Nimemsikia polepole na Waziri chanel ten wakitoa maelekezo kwa mabasi yote kukaa stand muda mrefu watu wale nakujisaidia.

Najiuliza Hawa watu wanajua hizo stand zina hadhi gani? Wanaelewa kwamba wapo wananchi wa hadhi tofauti? Wanaelewa umuhimu wa usafi?

Wamefanya utafiti wowote kuhusu hii hoja? Wanajua kuwa hoteli binafsi zinalipishwa Kodi kubwa na halmashauri kuliko Kodi ya wanaotoa huduma stand?

Leo hii kwa mfano mkoani tanga ukifunga hotel zote kubwa kwa maelekezo ya abiria wote wanaokwenda kaskazini waingie stand ya Korogwe hivi Kuna huduma pale?

Issue ya gharama ya chakula kwenye hoteli binafsi haitokana na wamiliki inatokana na mfumo wa serikali pamoja na huduma zinazotolewa. Choo bure, maji yakutosha Hadi yakuoga, eneo la maliwato safi , chakula safi, nk

Tujifunze kuwakemea wakina polepole wanaoishi kwenye mashangingi nakutaka siasa iwe ndo sheria kwetu.
 
... lengo ni kuwanyang'anya private biashara na kuzipeleka serikalini (owners wa stendi ni halmashauri/serikali) hakuna kingine. Kuna stendi moja iko pale Kibaigwa sipati picha basi lisimame pale kwa muda mrefu ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kula na kujisaidia! Hiyo stendi ni mahali ambapo usingetamani kusubiri hata kwa nusu dakika!
 
Aisee mdau pale stendi ya korogwe haina uwezo wa kuhudumia hata wale abiria wanaosubiri mabasi....
 
... lengo ni kuwanyang'anya private biashara na kuzipeleka serikalini (owners wa stendi ni halmashauri/serikali) hakuna kingine. Kuna stendi moja iko pale Kibaigwa sipati picha basi lisimame pale kwa muda mrefu ili wananchi wapate muda wa kutosha wa kula na kujisaidia! Hiyo stendi ni mahali ambapo usingetamani kusubiri hata kwa nusu dakika!
Napajua pale mkuu ni shiida aiseee
 
Mkuu wakitaka kukomesha urasimu huu wa Bus kulazimisha abiria wapate chakula kwenye hotel binafsi za bei mbaya ni njia moja tu inayofaa, TRA wafanye research halisi.ya bei wanazotoza abiri, waangalie Bus ngapi zinaingia hata kama ni kutungiwa sheria kila Bus ijulikane vituo vyake vya chakula na kujisaidia na mwisho wa siku oils Hotel ilipe kodi kulingana na ukubwa wa huduma plus matumizi ya EFD, bila hivyo uchochoro huu utaendelea kunenepesha vigogo wa biashara na maafisa wasiowaaminifu wa TRA wanaofanya makadirio madogo kwa hotel hizo, ni jambo la kusikitisha kuona kuwa wachuuzi wadogowadogo ambao ni wazawa wa sehemu hizo hufukuzwa na kuamriwa kukaa mbali na hoteli hizo kwa makusudi ili wasipate chochote toka kwa wasafiri
 
Back
Top Bottom