Maelekezo ya mahesabu mapya kwa wadaiwa wa HESLB

Maelekezo ya mahesabu mapya kwa wadaiwa wa HESLB

jacklinekahu

Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
7
Reaction score
1
Habari,

Mie ni mdaiwa wa bodi ya mkopo nilikua naomba kupata maelekezo kuhusu upigaji upya wa mahesabu wa tunaodaiwa na Loan Board, kiukweli nilipata shida sana ambapo siku ya alhamis nilifika katika ofisi za Bodi ya Mkopo nia ni kulipa deni langu ambalo lilikua limebakia kiasi cha sh milioni moja cha ajabu niliambiwa inabidi nipigiwe mahesabu upya na kujikuta nadaiwa kiasi cha sh milioni sita kiukweli niliishiwa nguvu na nilivyouliza nikaambiwa ni waraka umetoka na wao wanautekeleza.

Hoja yangu ni kwamba kwanini wasitujulishe kupitia vyombo vya habari ama kupitia waajiri wetu maana mwajiri wangu anajua nadaiwa kiasi cha sh milioni moja ndo outstanding balance, pili je hili deni kwa wataalam wa sharia si inabidi iwaguse wale ambao hawajaanza kukatwa sio sie ambao tumeshakatwa kwa miaka minne mpaka sasa?

Na tatu je ambao walishamaliza kulipa je nao watapigiwa mahesabu upya?
 
Duhh...wenye taarfa waje watujuze jaman . Ata ne naona hiyo kitu ni ngumu kwa kwel
 
mkuu ulikuwa umekopeshwa mil 1 tu au? ulikaa mda gani bila kulipa deni lao? kumbuka kuna walomaliza chuo kama miaka 4 hivi waliambiwa baada ya mwaka uanze kulipa kwa hiari vinginevyo utapata % fulan kama adhabu kila mwaka. na kama wamekuonea nenda na ule mkataba wako wa mkopo hasa ile form ya mwanzo ulojaza ndo ina mkataba pake mafisadi ukicheka nayo utatoa hyo lela wataipiga tu
 
Back
Top Bottom