Maelekezo ya vitisho kwa Bwana Harusi siku ya Harusi kutoka kwa Wakwe hasa Mama wakwe sisi Watibeli hatuyaruhusu hata kidogo

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
MAELEKEZO YA VITISHO KWA BWANA HARUSI SIKU YA HARUSI KUTOKA KWA WAKWE HASA MAMA WAKWE, SISI WATIBELI HATUTAYARUSU HATA KIDOGO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kila mtu akae kwenye mipaka yake. Huko ndiko kuheshimiana.

Kuna familia ambazo Wamama ndio vichwa vya familia. Wao ndio wenye sauti na maamuzi kuliko Waume zao.

Jambo hili hupelekea wamama hao wanadhani kila mwanaume wanaweza kumuendesha watakavyo.
Wewe kama unamuendesha huyo mumeo ni huyohuyo.

Kama ukiongea na mumeo ambaye ni Baba mkwe wangu, kisa mzee ni mpole au hapendi shari, au ni lofa, basi usifikiri kila mwanaume utamuendesha hivyo.

Sisi Watibeli tuliofikia umri wa utu uzima, tukaoa kwanza hatupokei maelekezo kutoka kwa Wanawake. Iwe ni Mama mzazi au mwanamke yeyote.

Nimeshuhudia baadhi ya harusi kadhaa, sisemi watu wote wawe kama sisi Watibeli ila nazungumzia ile aibu yenyewe.

Unakuta muda wa wazazi kutambulishwa na kutoa neno kwa watoto.
Mzazi anaanza maelekezo yasiyo na kichwa wala miguu. Vitisho na vita ya kisaikolojia ya kumtisha Bwana Harusi.

Hasa wanawake ndio wanatabia hizi za kijinga jinga. Na ilivyo bahati mbaya unakuta inaachwa iende kama inavyoenda. Hakuna anayetoa marekebisho na kukanusha kauli na vitisho vya Mama mkwe.

Harusi moja niliishuhudia Mama mkwe akizungumza aibu utaona wewe.
Dhihaka, jeuri, vitisho na kumshusha Bwana Harusi.

Wewe Mama Mkwe kama unapesa ni zako. Kama una cheo au kazi nzuri ni yako. Huwezi leta mambo yako kumpa maelekezo mume wa binti yako tena mbele ya halaiki. Kwa sisi Watibeli kwa kweli siku hiyo itakuwa siku mbaya kwako. Kwani hautavumiliwa hata kidogo. Na binti yako akiwa mpuuzi kama wewe harusi itakuwa imeishia hapo.

Mama Mkwe anashika maiki anaanza kuzungumza;
Ooooh huyu hajafukuzwa huyu. Huyu ana ndugu huyu.
Babaake alikuwa hana lolote mimi ndiye nimemjenga,
Babaake alikuwa analeta zile za kuleta nikamuweka sawa. Hivyo nawe ujiangalie. Sio kama nakutisha ila nakutahadharisha.

Kwetu mwanamke hagombezwi, sitaki umgombeze binti yangu.
Binti yangu namjua. Ole wako! Ole wako anipigie simu unamtesa. Blah blah blah!
Binti anandugu sio waje nyumbani kwake(kwa binti) uwafukuze, alooh utanijua mimi ni nani? Watakuja kwa dada yao. Wataamua wakae muda gani kwani dada yao sio njaanjaa. Nafikiri nimeleweka"

Hayo maelekezo yenye vitisho ukitoa kwa watibeli hapo lazima maelekezo hayo yazuiwe papo hapo. Tena na Kijana mwenyewe anayeoa.

Baba wakwe wanajua nini chakusema. Wanajua binti akiolewa anaenda kwenye himaya nyingine. Na kila himaya inasheria na taratibu zake.
Baba wakwe wengi wanaelewa wanaume timamu hatupendi kupangiwa na kupewa pewa maelekezo jinsi ya kuendesha familia zetu.

Baba Mkwe kama ananeno atakuita, mtazungumza kiume. Mkiwa wawili. Kisha mtazungumza tena ataongea kwa mipaka.

Lakini hivi vimama vilivyokosa adabu na haya, kukukosea adabu ni jambo la kugusa.

Na ukitaka uharibu familia yako ni kustahi au kuwa na busara pale unapokosewa adabu. Kamwe usinyamazie kukosewa adabu tena mkeo akiwepo, kisha baadaye na watoto.

Kwenye Harusi, mzazi ukipewa nafasi ya kuongea. Shukuru, pongeza, kisha mwambie asisahau mafunzo mema na asichoke kujifunza mambo mema.

Mkwe halikadhalika, Shukuru, pongeza, ambia wafuate maadili waliyofundishws.
Wote watakieni Maisha mema ya ndoa.

Sio unakuja hapa unataka kutoa mahubiri na mafunzo ili uonekane unajua kufundisha na kujifanya mkali usio na maana yoyote. Kutaka sifa za kijingajinga.
Sisi watibeli tutakuzimia maiki. Maana tayari Fundi mitambo na MC watakuwa wamearifiwa hivyo.

Na ukitoa maelekezo na vitisho kwa kung'ang'ania. Watibeli nasi tutakupa maelekezo. Hapohapo.

Mfano Scenario kama hiyo hapo juu. Mtibeli angejibu jibu linalofanana na hili;
" Tunashukuru Wazazi kwa kutulea na kutusapoti mpaka kufikia hatua hii. Ni wazi Mungu ametupa bahati ya kuwa na wazazi kama ninyi.

Lakini nitumie sherehe hiihii kukumbushana kuwa, Kila Familia inautaratibu na sheria zake.
Wazazi wangu, kaka, dada, ndugu na marafiki. Kwa heshima na kwa desturi zetu. Sisi kama wanandoa wapya, na mimi kama Kichwa cha Familia hii ambayo wote tupo hapa kusherehekea uanzishwaji wake.

Sitaturuhusu mtu yeyote aingilie familia yangu. Aniletee sheria au utaratibu. Nami sitaingilia familia zenu.
Wazazi wangu, wakwe zangu, ndugu, jamaa na marafiki lazima tuheshimu mipaka yetu.

Familia hii kichwa ni Baba, mimi. Tunawakaribisha wote katika familia yetu. Mtutembelee. Ninyi ni muhimu sana kwetu. Lakini mkija mjue sheria zitakazofuatwa ni zetu. Nasi tukija kwenu tutafuata sheria zenu"

Hivyo yaani! Sauti tulivu, sura isiyo na shaka, macho ya kiongozi anayejua kulinda na kuongoza watu wake.

Vijana msijiume ume. Msiogope kugombana au kuonekana wabaya kwa kusimamia mipaka yenu. Mtatumika vibaya. Mtatumiwa. Mtakosa furaha.

Onyesheni msimamo wenu tangu mwanzo. Msiwe watu wa kuhofia sijui utaachwa, sijui watakuonaje. Acha wakuone hivyohivyo.

Ukishakuwa na msimamo na unajali mipaka yako. Unatengeneza mazingira ya kuheshimiwa.

Ukiwa mtu nyeusi, ni nyeusi. Nyeupe ni nyeupe. Unafanya watu wakuamini na wasikuchezee. Wasikutumie.

Moja ya sababu ya ndoa nyingi wanaume kushindwa kuongoza familia zao. Ni kujifanya wana staa na busara hata wanapovunjiwa heshima.

Mtu akukuletea vita unampa vita.
Mtu akiumwa Malaria unamtibu na dawa za malaria sio umpe dawa za UTI.

Mimi nimemaliza. Tunatembea kwenye laini hiyo.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hakuna ulazima wa kumjibu mbele ya hadhara mtu wa aina hiyo maana hauwezi kufahamu ni kivipi ataypokea maneno yako.

Ili kuepusha harusi isivurugike subiri ikishamalizika kama kutakuwa na ulaziwa wa kuzungumza naye/nao, fanya hivyo.
 
Nafikiri kijana akipewa maiki ya kushukuru, hotuba yake inapaswa kuwa fupi na ya kukata mzizi wa fitina kuelekea kwa Mama Mkwe:

"Shukrani sana kwa wazazi wetu. Tumepokea ushauri na maonyo yote. Lakini niweke wazi: kuanzia sekunde hii, huyu ni mke wangu na hii ni familia yangu. Sisi ndio tutakaoweka sheria za ndani ya nyumba yetu, nani aingie, nani akae, na nani asikae. Hakuna mamlaka nyingine nje ya nyumba yetu itakayopanga jinsi ya kuendesha maisha yetu. Asanteni."
Hapo unakuwa umeweka bonge la ukuta kama ule wa Berlin. na hicho kimama mkwe atajua hapo hapikwi mchuzi, na binti atajua hapo amepata mume, sio wa kuchezewa.

Watibeli hawanaga subira kwenye baadhi ya ishu.

Kama yeye hafikirii maneno yake yatapokelewaje. Pia sio kazi yako wakati unajibu kufikiria atapokeaje
 
Nafikiri kijana akipewa maiki ya kushukuru, hotuba yake inapaswa kuwa fupi na ya kukata mzizi wa fitina kuelekea kwa Mama Mkwe:

Hapo unakuwa umeweka bonge la ukuta kama ule wa Berlin. na hicho kimama mkwe atajua hapo hapikwi mchuzi, na binti atajua hapo amepata mume, sio wa kuchezewa.

Sahihi Kabisa.
Na itatoa hamasa kwa wanaume wengine na kurudisha nyuma wamama wengine wasio na adabu..litakuwa funzo
 
Familia za hivi au mama mkwe wa hivi huwa ni watata na wanajaza binti zao upuuzi mwingi, ukikaa vibaya ndoa yako inabomolewa mapema iwezekanavyo. Msingi wa ndoa unaanza kwenye uchumba, kufikia kwenye ndoa umeshajiridhisha na huyo mwanamke na upo tayari kuipokea familia yake, na yeye yupo tayari kuipokea familia yako.
Tabia za mama mkwe ulizotoa zinaonyesha mwanaume hakuwa makini kuitambua familia anayoenda kuishi nayo.
Mwanaume makini na anayependa utulivu wa ndoa yake, angebaini hili mapema.
 
A wedding ceremony is exclusively an affair of Bwana Harusi.

Mama Mkwe's skanky behaviour cannot travel beyond the walls of The Kitchen Party and Send-Off.
​
 
Kwenye harusi yeyote wa upande wa mwanamke akiongea maneno kama hayo nitamuomba kistaarabu kabisa, kwa heshima na taadhima afute hayo maneno.

Kama ni mama au baba mkwe ameongea hivyo, kisha wakagoma kufuta hizo statements, wanaondoka na binti yao palepale.
 
Familia za hivi au mama mkwe wa hivi huwa ni watata na wanajaza binti zao upuuzi mwingi, ukikaa vibaya ndoa yako inabomolewa mapema iwezekanavyo. Msingi wa ndoa unaanza kwenye uchumba, kufikia kwenye ndoa umeshajiridhisha na huyo mwanamke na upo tayari kuipokea familia yake, na yeye yupo tayari kuipokea familia yako.
Tabia za mama mkwe ulizotoa zinaonyesha mwanaume hakuwa makini kuitambua familia anayoenda kuishi nayo.
Mwanaume makini na anayependa utulivu wa ndoa yake, angebaini hili mapema.

Upo sahihi

Ila wakati mwingine unaweza kukuta binti/kijana mzuri lakini wazazi vimro.
Au wazazi wazuri lakini binti/kijana kimeo
 
Kwenye harusi yeyote wa upande wa mwanamke akiongea maneno kama hayo nitamuomba kistaarabu kabisa, kwa heshima na taadhima afute hayo maneno.

Kama ni mama au baba mkwe ameongea hivyo, kisha wakagoma kufuta hizo statements, wanaondoka na binti yao palepale.

Kuwaambia wafute itakuwa kipengele kingine

Kutoa kauli za jumlajumla bila kumuattack moja kwa moja mhusika itakuwa ndio kauli zenye uongozi na utawala

Mfano; unatambua nafasi za wazazi lakini hutokubali mtu kutumia nafasi yake vibaya kuvuka mipaka yake na kuingilia familia yako.
 
Asante sana ndugu kwa andiko lililoshiba na ililokamilika.....kama ulivyo tangulia kusema kwenye tahadhari hakika huu ni mwiba mchungu kwa "makahaba" na wale waliolipa mahari kuoa "makahaba"

Kwa kweli kuoa mwanamke asiyekuwa na bikra(isipokuwa mjane na mtarakiwa) ni kujidhalilisha na kujishusha thamani yako mwanamume!!!

Kuoa mwanamke asiyekuwa bikra ni sawa na kununua sahani ya ubwabwa ambayo wenzako wamekula kula na kuacha uchafu wao alafu wewe unafungashiwa unanunua na kwenda kula....kwanza hata anayekuuzia atakudharau.....

Kuoa mwanamke mjane ni sawa kuuziwa sahani ya chakula ya mtu ambaye aliweka oda ya chakula lakini akapata dharula na kutokula chakula kile ingawa alikifunua......

Kuoa mwanamke mtarakiwa ni sawa kununua sahani ya chakula ya mtu aliyewekewa chakula kingi akapunguza baada ya kuona hawezi kukimaliza kabla ya kukitia tia MIKONO......
 
Back
Top Bottom