Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

sasa dogo baada ya kujifunza soka yeye ana iba simu

Hana tofauti na wanasiasa na vijana wengi wa Afrika, wao wanataka shortcut. Vijana wengi siku hizi wakipata kazi tu, mwaka wa kwanza wanataka wamiliki gari, na mwaka wa pili wamiliki nyumba.

Wanasiasa wetu vivyo hivyo, wakipewa madaraka tu mfano kutuliwa Uwaziri, ni kwenda kuiba tu. Yaani mtu akiteuliwa kushika nafasi ya juu serikalini, hata vyombo vyetu Vya habari vinasema KAULA!

Vv
 
Kama ni kweli, we have a long way to go... uhuni hata kwa mama.

Mama yako hata akikukosea namna gani bado ni Mama yako na hautakiwi umvue nguo na watu wengine waone udhaifu na makosa yake! Makosa ya wazazi ni ya kumwachia Mungu tu! Adebayo kwa kumwanika mama yake (hata kama anayosema ni kweli) amejianika mwenyewe kuwa hana heshima! Amepata faida gani kwa kumwanika mama yake! Anatafuta huruma ya watu itamsaidia nini? Sana sana amefanya kuwa ngumu zaidi uwezekano wa kupatana na ndugu zake!
 
Mbaya sana hii. Ukiendekeza ndugu watakufilisi au watakuua kwa presha. Adebayor aachane nao kabisa.

Hakuna jinsi ya kuachana na mama! Unaweza kuachana na marafiki lakini siyo na mama. Amwombe mama yake msamaha kwa kumwanika hadharani! Adebayo hana adabu! hata kama aliyosema kuhusu mama yake ni kweli!
 

Tatizo pia waafrika tunapenda sana sifa na kujionyesha! Yawezekana matatizo aliyaanza mwenyewe! Yawezekana alijionesha kuwa anapesa nyingi labda kwa kugawa pesa kwa marafiki tu na ndugu wakaona kama ana uwezo wa kugawa mkwanja kwa watu baki basi ndugu atupe mshahara kabisa! Samahani nafikiria tu!
 
sipendi kudharau utu wangu kwa kusema waafrika tunamatizo wakati sijaenda ulaya kuishi na kujua tabia za huko je ni zote zinazoandikwa ni njema kuliko zetu? ukijidharau utadharauliwa tu

Ila ukweli unabaki kuwa waafrika tunatia aibu sana! inauma lakini ndivyo ilivyo! Siyo kwa wote lakini madudu mengi yanafanywa na waafrika wenzetu mpaka tunajisikia vibaya! Angalia wenzetu wa afrika kusini walivyofanya! Angalia Viongozi wetu wanavyofanya ufisadi mpaka mataifa ya nje yanaamua kusitisha misaada! Angalia mauaji ya albino! Angalia Viongozi wa kiafrika wanavyong'ang'ania madaraka kama yule wa burundi halafu amesababisha maelfu ya wakimbizi halafu hajali kabisa!
 
Aisee, waafrika sijui alieturoga Nani[emoji848]
 
Sasa inawezekana vipi ndugu wote wakawa against na ww kila jambo? Mm nahis Adebayor ndio chanzo cha matatizo yote
 
Hivi ndugu mmoja akipata nafuu ya maisha kusaidia wenzake ni lazima au hiari au hisani?

Isitoshe ndugu wengine huenda ni wabwetekaji tu au wafujaji.

Kila mtu apambane, akipata ashukuru, akikosa wala asijutie bali aendelee kupambana.

Wapi imeandikwa usiposaidiwa ukeshe ukilalamikia watu.
Ndugu waache wivu, husuda na kufuatiliana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…