Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

Huyo alieiba simu za wachezaji wenzie kafunika. Alimuaibisha sana jamaa. Inadhihirisha ni jinsi gani wana roho masikini adi afikie hatua ya kuiba simu 21 hahaha.

Huyo mama yake atakua mchawi kweli kwani hakuna mama asiyefurahia maendeleo ya mwanaye.
 
Fikiria wanatuma mpaka barua kwenye team yake ili atimuliwe? Mama mwenyewe kwenye picha anaonekana ana roho mbaya sana.
 
Bahati mbaya ya Adebayor ni kwamba ndugu zake wameunda umage (umoja) dhidi yake ukiongozwa na mama yao..

Kazi anayo..
 

ha ha ha u made my day son!
 
alifanya kosa kubwa sana kuwafanya ndugu zake wamtegemee. alikuwa na wajibu kumtunza mamake tu, hao wengine hata wakija kwake kuomba hela walitakiwa wakopeshwe, sio wapewe bure. amenunua nyumba ameweka ndugu zake, kuna mengi naona yanaendelea hapo. jambo ninalojifunza ni kwamba, inawezekana ndugu zake wanakijua kitu kibaya sana alichokifanya, na inawezekana alifanya keli, wasingeweza kumruka kiasi hicho na yeye akawa mtumwa kiasi hicho, labda anakuwa mtumwa kiasi hicho ili kujibembeleza kwao wapotezee kitu kibaya sana alichokifanya.

tatizo kubwa ambalo naona watu wanamuonea huruma na kumtetea ni kuhusu kusingiziwa uchawi kumuua kaka yake. watu hawaamini kuwa kuna kuuana kiuchawi, mimi binafsi nilishawahi kuuliwa na dadangu tumbo moja kiuchawi, na ilikuja kuthibitika na muuaji kiuchawi akakiri na kuomba msamaha ukoo. haya mambo yapo, hivyo wakati mwingine ukiona kuna minong'ono kuna jambo. yeye anavyowalea sana ndugu zake hivyo kuna ishara ya kuwabembeleza fulani hivi kama anajikomba kwao fulani hivi, na kitendo hadi cha mama yake kumruka na ndugu zake kumruka kiasi hicho na yeye akawa anawalamba miguu kiasi hicho, why? if he's clean kwanini hajapata ujasiri wa kuwapa za uso na kuwatimua mbali huko? najua inaweza kuwa ngumu kumtimua maza lakini mamake mzazi aliyemfanyia makubwa hivyo amemruka, kuna jambo. si kawaida. ukiua ndugu zako hata kama unawapa mali haziwezi kuziba pengo la roho ya mtu. asitafute huruma za wanadamu hapa kama alifanya kweli kosa akatubu, kama hakufanya hata majuto yake yangekuwa makubwa sana.

ukisingiziwa kuua ndugu, na ukawa haujafanya hivyo, nakuambia unaweza kuumia moyo kiasi kikubwa sana kiasi cha yeye asingekuwa na hata uwezo kucheza mechi. lakini kama ni kweli, unajikaza kisabuni tu hivyohivyo kama yeye. kwenye hayo mambo nilishapitia sana, nilishafanya sana, shetani yupo na Mungu yupo na usione kila mtu anafanikiwa, mwingine anaendesha prado kwa kupitia nyota za wenzie, mwingine anacheza mpira kwa kupitia nyota za wenzie, kama hauamini uchawi basi wewe haupo duniani. sijamuonea huruma kwasababu kwa ushahidi wa mazingira naona kuna kitu ambacho yeye hajatubu kwa ndugu zake na ndugu zake wanaona hata akiwapa hela kinyongo bado wanacho moyoni mwao haitoshi.

unaaminije mwanadamu wa kawaida, adebayo amenunua nyumba ya bilioni mbili tshs, akaweka ndugu zake, alipoenda kuwapigia simu ndugu huyohuyo amtukane kwa nusu saa? huo ujasiri aliupata wapi? mamake naye huo ujasiri aliupata wapi, lazima kuna sababu, kuna kosa ambalo amelifanya na ndugu zake wanamchukulia mateka awafanyie chochote kila kwasababu ya kosa hilo, na alilifanya kweli ndio maana ameendelea kuwalea kiasi hicho, asingekuwa amefanya kweli angeshawatoa ngeu muda mrefu tu. kwa mtu mwenye akili ataona hili ila wanafiki wanaojifanya wako mbinguni hawaamini haya mambo watakuja juu.
 
Nyani Ngabu na ule usemi wake miafrica ndivyo tulivyo unahusika hapa

Kwanini tunajichukia hivi? Mimi nadhani weupe ndio wanaongoza kwa viroja dunia hii... Na vingine wanavifanya kuwa halali kila kukicha! Kilichotokea ni kitu cha kawaida kabisa kwenye familia za Kiafrika hasa ndugu mmoja anapotoka kimaisha.

Halafu hiyo ni stori ya upende mmoja, hatujawasikia hao ndugu zake wana maoni gani/lipi la kusema!
 
na bado tunasema eti weusi na wazungu wana akili sawa!!

Emencipate yourself from mental slavery. We unawaona wazungu kwenye TV basi unafikiri wako perfect kwa kila kitu. Wazungu ni binadamu tu nao wanamigogoro ya kifamilia au wanagombea mali kama sisi waafrika. Sio lazima kuishi na wazungu kujua hilo lakini ukiishi nao utajua kuwa wanamigogoro ya ajabu hata Afrika haiwezi kutokea.
 
Hute inaonesha wewe ni ile design ya watu wanaamini ushirikina 100%...pia inaonyesha una kipato cha chini mno...na pia shule kwako ni ile ya kukariri....haya manyanyaso yanawapata sana watu waliondelea hujui tu....
 
hapa Tanzania tabia ni hizo hizo ndugu wanaweza kuuza hata kiwanja na nyumba yako usipoangalia,waafrica inabidi tubadilike asante kwa wakenya they don't take nonsenses utakuta wanaishi kila mtu kivyake vyake
 
Adebayo ni mwafrika, anajitambua, ndugu zake hawapendi anavyofanikiwa, wamemshawishi mama yao amshinikize mwanae (adebayo) agawane nao mapato yake. Pamoja na hivyo adebayo amejitahidi sana kwa mujibu wa maelezo yake.
Naliona tatizo kwa mama yake, hao ndugu zake ndio kabisaaaaaa sina jema la kusema.
 

Nielewavyo mimi mama amekulea ukiwa mtoto huna akili akakulinda mpaka umekua na kujitegemea!! hakuna ubaya nawe ukimlea akiwa kama mtoto!! no matter what!! udhaifu wake hauwezi kutangazwa kwenye mitandao.. hakuna ambacho mama hakijui kuhusu mtoto wake, anajua hadi nyeti zako wakati zinakua zilikuaje!!...kama kina mama wangekua wanatangaza mapungufu yetu sijui tungekua wageni wa nani!! ... hawa kina mama waachwe tuu hata akikutukana inamisha kichwa chini na sema samahani!!... wanatujua kuliko tunavyojijua!! mioyo yao imebeba mengi kuhusu sisi na hawatangazi!!...
 

Kaka hii sio stori ya upande mmoja
Kama ulifatiliaa kwa kina habari hizi
Hii ni stori ya upande wa pili
 

Nakuhusu ndugu zakee ongea pia mkuu
 
Duh nakumbuka G Bale wakati anasajiliwa na Madrid ule mpunga akataka awanunulie wazazi wake mjengo wa hatari ila wazazi wakakataa wakisema wanafurahi kubaki mtaa ule ule na nyumba ile ile ili waendelee kufurahi na jirani zao ingawa nyumba ilikua ya kawaida sana.
Mbombo ngafu kweli.
 
Afrika mwenye uwezo siku zote anaonekan mbaya.....bora uwe bandidu....

Akili hawana yani mijitu mizima imekaa tu inataka ilipwe mshahara na nyumba wajenhewe kwa kazi gani kubwa waliyofanya kama ni miguu si wanayo nao wakacheze mpira?!

Huyo mwingine kapelekwa academy ufaransa kaishia kuiba simu, mjinga wa mwisho kabisa huyo,

Mtu ambaye kanisaidia mpaka nikapata mafanikio ndio nipo obligated kumsaidia otherwise asinipigie mtu kelele fullstop
 

Kuna wengine wanakumbushia kukubeba ukiwa mchanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…