alifanya kosa kubwa sana kuwafanya ndugu zake wamtegemee. alikuwa na wajibu kumtunza mamake tu, hao wengine hata wakija kwake kuomba hela walitakiwa wakopeshwe, sio wapewe bure. amenunua nyumba ameweka ndugu zake, kuna mengi naona yanaendelea hapo. jambo ninalojifunza ni kwamba, inawezekana ndugu zake wanakijua kitu kibaya sana alichokifanya, na inawezekana alifanya keli, wasingeweza kumruka kiasi hicho na yeye akawa mtumwa kiasi hicho, labda anakuwa mtumwa kiasi hicho ili kujibembeleza kwao wapotezee kitu kibaya sana alichokifanya.
tatizo kubwa ambalo naona watu wanamuonea huruma na kumtetea ni kuhusu kusingiziwa uchawi kumuua kaka yake. watu hawaamini kuwa kuna kuuana kiuchawi, mimi binafsi nilishawahi kuuliwa na dadangu tumbo moja kiuchawi, na ilikuja kuthibitika na muuaji kiuchawi akakiri na kuomba msamaha ukoo. haya mambo yapo, hivyo wakati mwingine ukiona kuna minong'ono kuna jambo. yeye anavyowalea sana ndugu zake hivyo kuna ishara ya kuwabembeleza fulani hivi kama anajikomba kwao fulani hivi, na kitendo hadi cha mama yake kumruka na ndugu zake kumruka kiasi hicho na yeye akawa anawalamba miguu kiasi hicho, why? if he's clean kwanini hajapata ujasiri wa kuwapa za uso na kuwatimua mbali huko? najua inaweza kuwa ngumu kumtimua maza lakini mamake mzazi aliyemfanyia makubwa hivyo amemruka, kuna jambo. si kawaida. ukiua ndugu zako hata kama unawapa mali haziwezi kuziba pengo la roho ya mtu. asitafute huruma za wanadamu hapa kama alifanya kweli kosa akatubu, kama hakufanya hata majuto yake yangekuwa makubwa sana.
ukisingiziwa kuua ndugu, na ukawa haujafanya hivyo, nakuambia unaweza kuumia moyo kiasi kikubwa sana kiasi cha yeye asingekuwa na hata uwezo kucheza mechi. lakini kama ni kweli, unajikaza kisabuni tu hivyohivyo kama yeye. kwenye hayo mambo nilishapitia sana, nilishafanya sana, shetani yupo na Mungu yupo na usione kila mtu anafanikiwa, mwingine anaendesha prado kwa kupitia nyota za wenzie, mwingine anacheza mpira kwa kupitia nyota za wenzie, kama hauamini uchawi basi wewe haupo duniani. sijamuonea huruma kwasababu kwa ushahidi wa mazingira naona kuna kitu ambacho yeye hajatubu kwa ndugu zake na ndugu zake wanaona hata akiwapa hela kinyongo bado wanacho moyoni mwao haitoshi.
unaaminije mwanadamu wa kawaida, adebayo amenunua nyumba ya bilioni mbili tshs, akaweka ndugu zake, alipoenda kuwapigia simu ndugu huyohuyo amtukane kwa nusu saa? huo ujasiri aliupata wapi? mamake naye huo ujasiri aliupata wapi, lazima kuna sababu, kuna kosa ambalo amelifanya na ndugu zake wanamchukulia mateka awafanyie chochote kila kwasababu ya kosa hilo, na alilifanya kweli ndio maana ameendelea kuwalea kiasi hicho, asingekuwa amefanya kweli angeshawatoa ngeu muda mrefu tu. kwa mtu mwenye akili ataona hili ila wanafiki wanaojifanya wako mbinguni hawaamini haya mambo watakuja juu.