Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

Maelezo binafsi ya Emmanuel Adebayor kuhusu mgogoro wake na Familia yake

Dah!
Pole zake sana, nilikuwaga sijui yanayomsibu ktk familia yake!
 
Emencipate yourself from mental slavery. We unawaona wazungu kwenye TV basi unafikiri wako perfect kwa kila kitu. Wazungu ni binadamu tu nao wanamigogoro ya kifamilia au wanagombea mali kama sisi waafrika. Sio lazima kuishi na wazungu kujua hilo lakini ukiishi nao utajua kuwa wanamigogoro ya ajabu hata Afrika haiwezi kutokea.

Ahsante sana kaka!

Ipo kasumba moja kuhusu sisi, kutojikubali na kuona kila kitokacho Magharibi ni chema... Huko ni kawaida mtu kumfukuza nyumbani mtoto akifikisha miaka 18, na kupeleka wazazi kwenye vituo, wakiugua maradhi, uzee na zaidi upweke unaotokana na kuachwa na watoto wako wa kuwazaa!

Kiafrika ni wajibu, na ni lazima kuwatunza ndugu na wazazi, ikitokea umeyapatia maisha kwa maana lazima nao wana mchango wao katika hilo.

Kuna wakati home tulikula mlo mmoja ili kaka na dada wasome vizuri chuo, leo wamebutua ni wajibu wao kutushika mkono hadi nasi tujitegemee na kuwapokea baadhi ya mizigo kama kulea wazazi na kadhalika!

Najivunia utamaduni wetu!
 
Kaka hii sio stori ya upande mmoja
Kama ulifatiliaa kwa kina habari hizi
Hii ni stori ya upande wa pili

Kwenye mambo kama haya huwa kuna kuigiza upole, mtu anajifanya kama yeye ni mwema sana... Inawezekana wazazi na ndugu wana makosa, lakini hadithi imetiwa chumvi! Sijawahi kusikia popote mtu akiomba alipwe mshahara na ndugu... Hata siku moja!
 
Sasa kwa Mara ya kwanza Leo umeskiaa..😉

la msingi ni kuutafuta tu ukweli
 
Nielewavyo mimi mama amekulea ukiwa mtoto huna akili akakulinda mpaka umekua na kujitegemea!! hakuna ubaya nawe ukimlea akiwa kama mtoto!! no matter what!! udhaifu wake hauwezi kutangazwa kwenye mitandao.. hakuna ambacho mama hakijui kuhusu mtoto wake, anajua hadi nyeti zako wakati zinakua zilikuaje!!...kama kina mama wangekua wanatangaza mapungufu yetu sijui tungekua wageni wa nani!! ... hawa kina mama waachwe tuu hata akikutukana inamisha kichwa chini na sema samahani!!... wanatujua kuliko tunavyojijua!! mioyo yao imebeba mengi kuhusu sisi na hawatangazi!!...

Mkuu, inaelekea hii issue hujaipata vizuri, au ungerudia kusoma pale juu kwenye maelezo yake kagusia kidogo. Nini kimepelekea Adebayor kuandika huu waraka na kuutuma kwenye social media?...
Miezi michache nyuma, gazeti la The Sun la Uingereza liliandika habari za mgogoro wa kifamilia wa huyu bwana. Kaka wa Ade ndio alikuwa sterling katika ule mchezo, yeye alichukua hela kwa The Sun akampaka matope vya kutosha, na habari nyingine tulizisoma humu humu JF labda wewe hukubahatika kuziona. Baada ya ile habari dunia nzima pamoja na wanachama wa Jamii forums wote, nikiwemo mimi mwenyewe, walikuwa against Adebayor. Tulimjaji moja kwa moja bila kusikia story kutoka upande wake, sasa wewe unataka akae kimya unafikiri tungejuaje ukweli?

Haya mambo ya kusema wazazi wametuzaa, sio wote wanafanana na wa kwako wewe. Shukuru umepata bahati, lakini huu ulimwengu umejaa wazazi mabandidu huwezi kuamini. Wapo ambao wanafikia hatua ya kuwatia upofu watoto wao ili wapate hela.
 
kwani adebayo hakuwashika mikono??? sasa huyo dogo aliyepelekwa academy akaenda kuiba simu ni kosa la nani? hadi kasema ujue kapitia mengi
 
Ahsante sana kaka!

Ipo kasumba moja kuhusu sisi, kutojikubali na kuona kila kitokacho Magharibi ni chema... Huko ni kawaida mtu kumfukuza nyumbani mtoto akifikisha miaka 18, na kupeleka wazazi kwenye vituo, wakiugua maradhi, uzee na zaidi upweke unaotokana na kuachwa na watoto wako wa kuwazaa!

Kiafrika ni wajibu, na ni lazima kuwatunza ndugu na wazazi, ikitokea umeyapatia maisha kwa maana lazima nao wana mchango wao katika hilo.

Kuna wakati home tulikula mlo mmoja ili kaka na dada wasome vizuri chuo, leo wamebutua ni wajibu wao kutushika mkono hadi nasi tujitegemee na kuwapokea baadhi ya mizigo kama kulea wazazi na kadhalika!

Najivunia utamaduni wetu!

Nimeona mgogoro wa kifamilia wa kizungu ambao Tanzania hauwezi kutokea. Nina rafiki yangu mmoja wa kike, baada ya baba yao kuachana na mama yao, yeye na kaka yake hawakutaka mawasiliano nae tena mpaka wakapelekewa habari za msiba. Wote walikuwa wanaishi Rotterdam, huyu mzee aliendelea na maisha yake, akakutana na mwanamke mwingine akazaa watoto mpaka wanakua hawakuwahi kukutana jinsi walivyokuwa na hasira. Mpaka baba yao alivyokufa wakapelewa habari za msiba ndio wanakutana na ndugu zao kwa mara ya kwanza. Sasa wangekuwa weusi, wangesema waafrika hawana akili.
 
Inabidi tuanzie hapa? natamani ningesikia na upande wa pili wa hii hali.
FaizaFoxy hili saga miaka yote io tunasikiaga upande wa walalamikaji tu,dada mara mama mara kaka n.k zaidi yakujibu kiwestern Emma alikuwa ajawahi kujibu kwa kina na mkasa mzima,sasa leo upande wake yani yeye kajibu still mnataka upande wa pili kuusikia?au mnataka wa tatu jama...maana wa kwanza wa family members tumewasikia sana otherwise saga hili kama ulikuwa nalo mbali,ajabu pamoja na yooote ayo Emma anasema na anamthamini mama yake na familia yake,Drogba kamshauri dada na bro wapate kazi yakufanya ikibidi ya ajira,watapoa...seems baaado ana ithamini familia yake,wao bado wana ambaaa na media,wameenda media za Hispania,UK n.k sasa wakaweka base yao media za Ghana,ndio mwandishi OBAMA akalivagaa saga nae katoa shit saaana,ndio mwanaume katoka chimbo kajibu kifupi na kirefu pia...
 
Hii story imenigusa sana, kuna wakati inafika unajiuliza kama umezaliwa kusaidia watu na pamoja na jitihada kubwa unazofanya ndivyo matatizo yanazidi kuongezeka na lawama, it's like you're gifted & cursed at the same time... Kuna wakati unaweza kuomba hata upotee tu, familia za kiafrika ni shida sana.
 
Kwenye mambo kama haya huwa kuna kuigiza upole, mtu anajifanya kama yeye ni mwema sana... Inawezekana wazazi na ndugu wana makosa, lakini hadithi imetiwa chumvi! Sijawahi kusikia popote mtu akiomba alipwe mshahara na ndugu... Hata siku moja!

kaka hujawahi sikia ndio umesikia sasa achana na ndugu kabisa omba Mungu isijetokea kwako.
 
huyu ndiye mwandishi alimkashifu EMMA pasipo kufahamu upande wa pili,alizongwa na huzuni ya kaka ake Emma...Ndio kamfanya Adebayor anene yote hayo mwisho wa siku!

'SEA, I severely criticized you yesterday. As a journalist, I wrote a story when your family invaded Peace FM last year. I also thought their story was sad. But upon reading all this from you, and realising that this whole thing started long ago, I SAY
A BIG SORRY BROTHER.

clearly your family is there to ruin your life by living lavishly on your wealth without wanting to do anything. Apparently they have lived in poverty for a long time and so your shot to fame and richness came as a shock to them and they're dazed with the monies they read and hear in the media that you make, and want all for themselves.

Some African families are just bad, petty and ungrateful. Some are just lazy,and so even for you reaching this height and making the family proud, they think you got here easily. African families are basically the reason why most African footballers don't make it to the top.

I',m very sure about that. In the normal family standards and as it is in Europe, you should be spending your money on your wife, kids and charity BUT not your family. It is only within your jurisdiction and humility to help them but that is not compulsory.

Rio Ferdinand is one of the richest footballers in the World. His wife died and Ive not heard the family accusing him of not saving her with money because he aint God.

President's have seen their sons die young, they can't save them with money so why should your family accuse you of not doing enough to save your brother? Cristiano Ronaldo lost his dad, nobody has accused him of neglecting his dad. Western Families don't depend on people who have risen to fame for livelihood.

And so these guys there have absolute concentration. INTERESTINGLY, your sisters are suppose to be married and having life with their husbands now.

Why do they have to behave like being married to you? Emmanuel Adebayor, I think you have tried even sustaining at this level with all these issues for all these years. Any other star would have been hit down low with these distractions by now I tell you. You have a strong heart brother. You are blessed. I won't accuse your family because they are not mine.

But you don't belong to them alone now. you belong to the whole of Africa, specifically Ghana and Togo. We will help you to live. Don't neglect them completely. Talk to those who wanna talk to you. Keep playing your game and let those who want to destroy you have their way. GOD is the ULTIMATE JUDGE.

Sorry that I criticised you yesterday. Sorry again bro. Thank God that you have opened up on this

FaizaFoxy
 
Mbaya kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati

mbaya zaidi ni kuwa na ndugu halafu kichwa maji_Fid q
 
Kwa comments zote hapo, mimi sitii neno zaidi ya hili hapa chini...

This is Bible Article.
-------------------------------------
The Lord requires of us the same treatment toward His followers that we receive of Him.-We are to exercise patience, to be kind even though they do not meet our expectations in every particular....

The last six commandments specify man’s duty to man.-Christ did not say, You may tolerate-your-neighbor, but, “Thou shalt love thy neighbour as thy self.”
 
Nimeona mgogoro wa kifamilia wa kizungu ambao Tanzania hauwezi kutokea. Nina rafiki yangu mmoja wa kike, baada ya baba yao kuachana na mama yao, yeye na kaka yake hawakutaka mawasiliano nae tena mpaka wakapelekewa habari za msiba. Wote walikuwa wanaishi Rotterdam, huyu mzee aliendelea na maisha yake, akakutana na mwanamke mwingine akazaa watoto mpaka wanakua hawakuwahi kukutana jinsi walivyokuwa na hasira. Mpaka baba yao alivyokufa wakapelewa habari za msiba ndio wanakutana na ndugu zao kwa mara ya kwanza. Sasa wangekuwa weusi, wangesema waafrika hawana akili.

Mkuu, umesema lingine... uafrika ni alama mbaya kwa maamuma flani hivi!

Kuna nchi zikifanya ujinga, watu wakifanya madudu wanasifiwa au kutangazwa kama watu wa tofauti, lakini akifanya mbari ya Kiafrika inakuwa nongwa na weusi wote kuonekana hawana akili.

Narejea kauli yako ya mwanzo, tujitoe kwanza kwenye huu utumwa wa akili ndiposa tutaweza kusonga kama taifa moja, kama watu wamoja!

Kwa sababu hizi huwa nalazimika kufungamana na kila kilicho cha Kiafrika, maana kukosoana kwema ni kule kwenye nia ya kusaidiana na kuboresha maisha yetu, sio huku kukosoana kwa kudhalilishana!
 
kaka hujawahi sikia ndio umesikia sasa achana na ndugu kabisa omba Mungu isijetokea kwako.

Aye know nigga! Ila hii habari ina chumvi nyingi sana... Afu si unajua hawa wenzetu walioenda kuishi mashenzini huwa wana vitabia fulani vya kuiga huko? Simlaumu Ade, ila simuamini kiviiile...
 
Kwenye familia za kiafrica umoja na upendo uko tu wakati kila mmoja hana. Leo umetoka kimaisha kwa bidii zako mwrnyewe watakuponda na kukutakia mabaya huku wakilazimisha kusaidiwa. Ule upendo na umoja unapotea kabisa lawama zinakuwa nyingi. Ukifungua kampuni watataka uwaajiri wao bila kufikia vigezo uwalipe mishahara minono doing nothing isipokuwa kukuingizia hasara. Hata ukiwa mfanyakazi wa hospital au bank hawatataka kusubiri kwenye line kama wengine na usipowapa favor lawama hazitaisha. Ukichunguza vizuri adui namba moja mara mtu apatapo maendeleo ni ndugu na watu wa karibu.
Habari ya adebayor kugombana na familia nimeisikia siku nyingi hasa chanzo ni dada zake na mama yake. Kwa jinsi ya hiyo stori napata picha sasa. Mwanzoni EMA alikuwa analalamika mama yake na dada zake wanamloga. Familia za AFRIKA HAZIPISHANI. UKIWA NA MKWANJA kila atataka msaidie kwa lazima hata kama undugu wenu ni wa kugandisha na gundi.
 
Back
Top Bottom