Maelezo kidogo: Sole proprietorship Vc limited company.. kipi bora?

kanyagio

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Posts
1,021
Reaction score
366
wanajamvi pole na kazi. kwa wajuvi wa mambo ya usajili wa kampuni naomba kufahamisha je kuna advantage yoyote ya kusajili kampuni kama sole proprietor au limited company katika masuala yafuatayo:

1) aina na kiwango cha kodi ya kulipa (hapa kuna mambo mawili-- AINA na KIWANGO).. ni aina gani isiyokuwa na kodi kubwa?
2) upatikanaji wa mkopo bank

nauliza hivyo kwa sababu nataka kuanzisha kampuni ya biashara ya studio na children games ambapo share value ni kwenye 10,000,000 Tsh.

nitashukuru kwa watakoweza kudadavua ili tusiojua tupate elimu ahsanteni sana,
 

Limited company inakubana zaidi kwa maana ya kufaili return za kodi, BRELA, Municipal Levy nk. Sole proprietor kama mauzo yakio hayatazidi 40 million na wafanyakazi wakawa si zaidi ya watatu (3) ukishafanyiwa makisio ya kodi mwezi March hakuna tena usumbufu mpaka Mwaka mwingine. Ila kwa kukopesheka, unaangukia kwenye wajasiriamali wadogo hivyo kulingana na ufanisi wa biashara yako unaweza kwa mteja wa NMB au ACB ambao wanakopesha wafanya biashara wadogo.

Kwa upande wa kampuni faida ni kubwa zaidi kwani kampuni na wenye kampuni huhesabika kama ni watu tofauti hata hivyo unavyojituma wewe ni tofauti na mbia mwenzako atakavyokuwa anajituma; ukiweka familia kuwa wabia wako ni sawa lakini bado "risk appetite" ni tofauti wewe unaweza taka kukopa mkeo akawa anaogopa vitu kama hivyo.

Kwa kuanzia nakushauri anza na sole proprietor. Kama uko Arush ni PM kwa ushauri wa mambo ya kodi
 
kodi kubwa kwenye limited liability nafikiri corporate tax 30%..sema kuna tax avoidance unaweza fanya au possibly evasion(illegal) so unaweza ukawa fresh tu....
 
 

Mkuu nakushukuru, maelezo yako yamenisaidia mimi pia. Vipi kuhusu usajili, hivi usajili wa Kampuni ni sawa sawa na usajili wa Sole proprietor? ni documents gani zinahitajika kwa ajili ya kusajili wa Sole Proproetor na je una sajili Brela au sehemu tofauti. Nitashukuru kama nitapata majibu ya haya kutoka kwa wadau wanaofahamu.
 

Usajili wa kampuni una mlolongo ambao utamhusisha mwanasheria hivyo Mwanasheria atakudai gharama za kuandaa "Memorandum and Articles of Association" na Fomu nyingine ambazo lazima asaini ndiposa kampuni isajiliwe. Vile vile kabla ya kuchagua jina lazima ufanya "name search" pale kwa msajili ili kujiridhisha kwamba jina ulilochagulia halijasajiliwa na mtu mwingine. Gharama za kulipa BRELA na kumlipa mwanasheria kwa uchache hazitapungua TShs. 1,000,0000/= kutegemeana na kiwango cha mtaji unaosajiliwa

Kwa upande wa "Sole Proprietorship" kinachohitajika ni kwenda pale "BRELA" na kusajili jina la biashara, gharama yake haizidi 10,000/=
 
Katika Aina za Biashara au Mfumo, Campuni ndo Mfumo Bora kabisa, pamoja na kwamba ni very Complicated, lakini Limited Company ndo mfumo mzuri, Kama unataka ku trade na watu wa aina mbali mabli ikiwemo wa Ndani na Nje ya Nchi basi Limited ndo mpnago mzima, Ila kama unadanya for Substance basi tumia sole pr,

Invester wengi sana wanapenda sana Kufanya kazi na Kampuni na si mtu individualy na kuna sababu nyingi sana kwa nini wanapenda kufanya kazi na Kampuni na si mtu,
 


Ndachuwa
hapo kwenye red, je ukishasajili jina ndo basi, hakuna utaratibu wa kusajili kampuni kwa kuwasilisha BRELA documents za usajili like the "memorandum" and "articles".
Je kwa hapa Tanzania, ukiwa na kampuni sole propriator unaweza ku-compete kwenye tender zinazotolewa na makapuni mengine mfano chukulia Halmashauri ya Wilaya xyz wakatangaza tender ya ku-supply stationeries or kufanya usafi. Je unaweza kutumia sole proprietor company ku-tender?
 

Mkuu Inawezekana lakini kwa taabu sana, That is why nasema Mara Nyingi Limited Company ndo the best katika maswala ya Biashara, Ila kama unataka kufanya biashara for Survive wewe fanya individualy, Ila for sustainability ni lazima utumie kampuni,
 
kanyagio "name register" hahitaji MEMARTS utakachopewa ni Certificate of Registration na document ingine ya kuwaelekeza benki wakubadi ufungua akaunti kwa jina la biashara.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Inawezekana lakini kwa taabu sana, That is why nasema Mara Nyingi Limited Company ndo the best katika maswala ya Biashara, Ila kama unataka kufanya biashara for Survive wewe fanya individualy, Ila for sustainability ni lazima utumie kampuni,
Chasha idadi kubwa ya kampuni za ukaguzi na ushauri wa kibiashara ni siyo "corporate entity" ni "name register" tuu
 
Last edited by a moderator:
Chasha idadi kubwa ya kampuni za ukaguzi na ushauri wa kibiashara ni siyo "corporate entity" ni "name register" tuu

Ya najua kuna hilo la kuregster Jina, tu na ukawa una oparate bila shinda yoyote ile, Ila narudia kusema Limited Company do huwa inanafasi nzuri kibiashara, kwenye maswala ya Mikopo na kwenye Kodi pia
 

Mkuu kanyagio na Wanajamvi kwa ujumla, Pamoja na michango mizuri, nami napenda kuchangia kama ifuatavyo:

Kuna aina kadhaa za umasikini, mojawapo ni umasikini wa fikra/ mawazo. Tukiuondoa kwanza umasikini huu wa mawazo, ni rahisi kuondokana na umasikini wa kipato. Hakuna njia ya mkato zaidi ya kupenda kujisomea/ kusikiliza vitabu / machapisho au cd mbalimbali zinazungumzia maisha ya watu waliofanikiwa au kanuni za mafanikio. Hakuna mbadala.

Kuhusu faida ya kusajili kampuni kama sole proprietor au limited company katika masuala ya aina na kiwango cha kodi na upatikanaji wa mkopo bank, Ndugu Wanajamvi, tafuteni vitabu hivi na kuvisoma kwa kuanzia, mapema iwezekanavyo;
  1. THE CASHFLOW QUADRANT
  2. THE BUSINESS SCHOOL &
  3. THE BUSINESS OF THE 21ST CENTURY vyote vikiwa vimeandikwa na Robert T. Kiyosaki.
Vinapatikana kwenye maduka yafuatayo: Scholastic Bookshop (Mlimani City & Posta), Dar es Salaam Printers, Saramanda, n.k. Pia, kwa wauza vitabu stand ya mabasi ubungo vinapatikana.

Ninasema kwa kuanzia, kwa maana kwamba kuna vitabu vingi vizuri (sio vya Robert Kiyosaki peke yake) lakini vitabu hivi vitakusaidia kukupa mwanga zaidi juu ya Biashara na Ujasiriamali katika karne hii ya 21 katika mambo yafuatayo:

  • Tofauti (Faida na Hasara) kati ya Sole Prorietor (Small business), Limited Company (Business Owners), Wawekezaji (Investors), na Waajiliwa (Employees)
  • Utaratibu wa kodi uliopo kati ya Sole proprietor (Small busines) na Limited Company (Big Business / Corporations)
  • Fursa za mikopo zilizopo kati ya Sole proprietor (Small busines) na Limited Company (Big Business / Corporations)
  • Fursa / Uwezekano wa kukua hivyo kuajiri watu wengi zaidi na kusaidia tatizo la ukosefu wa ajira nchini, uliopo kati ya Sole proprietor (Small busines) na Limited Company (Big Business / Corporations)
  • Nafasi zilizopo ya biashara kukua vizazi hadi vizazi (business sustainability) kati ya Sole proprietor (Small busines) na Limited Company (Big Business / Corporations)
  • Nguvu ya mtandao / mfumo (kuwa na watu wanaokufanyia kazi) inayopatikana kwenye Limited Company ukilinganisha na Sole proprietor ambaye kimsingi, unakuwa ni mtumwa wa hela (working for money) kitu ambacho hakina tofauti na Kuajiriwa.
  • Zaidi, vitakupa muongozo mzuri namna unavyoweza kuutumia muda wako wa ziada (part time) kujenga TIMU ya watu watakaokuwa wanakufanyia kazi (SYSTEM/ NETWORK) kama ambavyo Bakheresa, Mengi, Manji, Bill Gates, Donald Trump, n.k walivyo na wanavyoendelea kufanya.

Kwa mawasiliano zaidi, piga 0713 366 473 au 0767 277 223.

KILA LA KHERI WAKUU.
 
nawashukuru sana kwwa maelezo yenu mliyotoa. naona nazidi kupata mwanga kuhusiana na aina ya kampuni ya kuanzisha. It seems kuwa na limited company kuwa nzuri zaidi lakini requirements za kodi zipo juu kidogo unlike proprietorship.

my last questions to Ndachuwa, Chasa na wengineo-- je ukiwa na sole proprietor company je unaweza kufanya biashara zaidi ya moja.. matarajio yangu ni kuanzisha pharmacy, children games na video studio businesses. je biashara hizi unaweza kuzifanya chini ya mwamvuli wa kampuni moja ambayo ni sole proprietorship?
 

mkuu kanyagio .... hiyo inawezekana .... wakati wa kufungua business name kwenye fomu utakayojaza itabidi u-list shughuli hizo za biashara utakazo zifanya lakini itakapokuja kwenye kupata business licence manispaa itabidi upate business licence zaidi ya moja kulingana na group iliyoangukia biashara .... mfano huwezi kupewa business licence ya farmacy ikiwa pamoja na photography kwani shughuli hizi ni tofauti na zipo kwenye group tofauti za business type, kwa manufaa zaidi nenda manispaa ya kinondoni watakupa forms ambazo zinamaelekezo ya business types and groups
 
Last edited by a moderator:
je kuna faida nyingine inafahamika?
 

Shukran Ndachuwa, mm ni mjasiriamali/mfanyabiashara kwa zaidi ya miaka 25 nimeshatumia mifumo hy yote, kampuni yangu ya kwanza illisajiliwa 1992 inaendelea, ni kweli kabisa kila moja ina uzuri na hasara zake, nadhani kilicho bora kabisa ili uweze kuamua ni ipi utumie pana mambo muhimu ya kuyatambua kama ifuatavyo;
1. Masoko yako - unalenga wateja wa aina gani kama ni public Institution, corporates lazima kampuni.
2. Mtaji uliopo - mara nyingi kampuni inahitaji mtaji mkubwa zaidi
3. Mfumo wa kodi - hii inategemea na mambo kadhaa ili kulipa kdg au zaidi, lkn kampuni inahitaji maandalizi makubwa.
4. Umiliki - wamiliki zaidi ya mmoja itabidi partinarship aidha sole proprietor
5. Aina ya Biashara - Trading zote ni sawa, Tenders aina nyingi zinahitaji Kampuni.
6.Malengo yako kwa muda huo - kama unaanza na lengo lako ni faida (kukua, ukomae kwa kupitia faida) na kama rasiliamali zingine ni haba, pia hakuna pingamizi la soko lako(wateja) nadhani sole proprietor is the best. lakini kama malengo ni kupanua masoko kwanza, goodwill kubwa, well advertised, aim large scale by all means either by sourcing capital from suplliers, Banks, even customers like Gvmnts, Investors - nadhani kampuni ni mahala pake....
hii ni kwa mazingira yetu ya TZ, ukweli ni kwamba kampuni inavutia walaji wengi sana hasa TRA , Municipals levy, n.k kwa uzoefu wangu sishauri mtu anayeanza biashara.....
 

Umeeleza vizuri sana mkuu, nimenufaika na mafundisho yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…