Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Kuna haya mambo machache kuhusu 5w na 20wGari yangu ina cc 1300 na kwa maelezo ya kwenye manual yake inasema kuwa Engine oil inayotakiwa kununuliwa ni 5W-30
Yeye ananambia kuwa kwa kuwa gari yangu engine yake imeshatembea zaidi ya kms 100,000 anashauri ninunue 20W-50
Kuna haya mambo machache kuhusu 5w na 20w
- 5w ni nyepesi ukilinganisha na 20w
- Kwa nchi zenye baridi sana na kwa matumizi ya gari ya kawaida (huendi masafa marefu - engine haipati joto sana) waweza kutumia 5w kwa sababu bado engine oil haitokuwa nyepesi sana kutokana na joto la engine hivyo viscosity yake haito badilika sana, na itakidhi mahitaji.
- Kwa nchi zenye joto; na iwapo ni mtu wa safari ndefu, ni vyema ukatumia 20w
- Kingine iwapo huwa unabadili oil kwa kila 3500km kwa 5w-30, basi iwapo utatumia 20w-50 waweza kuwa unabadili oil kwa kila 4500KM kutegemea na matumizi yako ya gari.
Hivyo ushauri uliopewa wa kutumia 20w-50 ni sawa na ni vyema ukauzingatia.
Mimi binafsi natumia 20w-50 kwa gari ya cc1300
View attachment 758659
NB: Mimi sio mtaalamu wa magari, Maelezo haya ni kutokana na ufahamu wangu mdogo nilio nao, Naomba na wengine wachangie, ili nijifunze pia.
Ahsante
Hii ndo mtaalamu aliyoshauri. Kuwa tena hamna haja ya kununua sythentic kwa kuwa gari imeshatembea sana so ni cost za bure tu pia kwa kuwa haitumii sana umeme kama gari za miaka hii.Kuna haya mambo machache kuhusu 5w
Ahsante
Gari yangu ya 2001, niliweka hiyo oil ya 20w-50, gari ikawa nzito, inavuma sana asubuhi, mbaya zaidi, fuel, consumption ikaongezeka sana. Gari ni 1800cc. Niliimwaga oil hiyo kabla ya wakati. Sasa natumia 5w-30 kulingana na specs za engine (1ZZ-FE).Nashukuru kwa maelezo yako mazuri. Gari naitumia kwa mizunguko ya hapa hapa mjini. Kazini home na sijawahi toka nayo nje ya mkoa.
So unashauri kuwa 20W-50 itakuwa nzuri kwa engine hii ? Na kwenye suala la mafuta na gari kuwa smooth huwa haliathiriki ?
Gari yangu ya 2001, niliweka hiyo oil ya 20w-50, gari ikawa nzito, inavuma sana asubuhi, mbaya zaidi, fuel, consumption ikaongezeka sana. Gari ni 1800cc. Niliimwaga oil hiyo kabla ya wakati. Sasa natumia 5w-30 kulingana na specs za engine (1ZZ-FE).
Ilikuja imetembea roughly 160,000km, hapa nimeitumia toka 2015. Nilipoweka 20w-50, nilienda 250km full tank likaisha. Nilipotoa hiyo oil nikaweka 5w-30, full tank nikaenda 430km. Hapa ishatembea roughly km elfu 35.Baada ya kurudisha 5W30 imekuaje? Na pia imeshatembea kms ngap mpaka sasa?Jumla ya kms zote tangu iundwe
Ilikuja imetembea roughly 160,000km, hapa nimeitumia toka 2015. Nilipoweka 20w-50, nilienda 250km full tank likaisha. Nilipotoa hiyo oil nikaweka 5w-30, full tank nikaenda 430km. Hapa ishatembea roughly km elfu 35.
Natumia FUCHS oil, synthetic, natumia kwa 3000km.Thanks. This is very good information. Sijui ni ainw gan ya oil unaweka yaani ni mineral au synthetic?brand gan? Unatumia kwa km ngapi?
Kwa nini na ni kama ipi ili umsaidie jamaa... Kwa mfano 20W50 na 5W30 ipi ni nzito? Kwa mfano wa jamaa alichoandika?Oil yenye ute ute mzito zaidi (high coefficient of viscosity) ni bora zaidi kwa gari yako.
Gari yangu ina cc 1300 na kwa maelezo ya kwenye manual yake inasema kuwa Engine oil inayotakiwa kununuliwa ni 5W-30
Yeye ananambia kuwa kwa kuwa gari yangu engine yake imeshatembea zaidi ya kms 100,000 anashauri ninunue 20W-50 na anasema kwa hii gari haina haja ya kununua sythentic kutokana na kuwa engine yake imeshatumika sana na si gari ya umeme sana. Gari ni ya mwaka 2000. Toyota.
Sasa najiuliza nifanye nini....maaana muuzaji anasema kwa kuwa engine imeshatumika sana hiyo 5W-30 ni nyepesi sana.
Wataalamu tusaidiane katika hili.
Always, tumia Oil iliyokuwa recommended kwenye Manual, achana na propaganda zingine kabisa..!! nlishawahi fata ushauri huo wa "kitaalam" na nikaishia kuwa na maumivu na matokeo kama ya jamaa hapo juu (Ilonga), from 20w-50 nikatoa nikaweka hiyo 5W-30 recommended mizunguko ya kawaida tu hapa mjini, Gari Honda CR-V total Mileage now ni 145K, changes ni amazing
Kwenye bonnet kuna sehemu huwa wanaandika ina ya engine oil ya kutumia kwenye gari lako. Ukikosa nenda google andika aina ya gari na toleo lake wakutajie aina ya oil zinazotumika watakutajia.Na mimi nina x trail ina mileage 170000km hua natumia castro 20w-50 .... je nipo sahihi kutumia oil hiyo au ndo niludi kwa full synthetic...sina user manual gari nilipata kwa mtu
Siku zote zingatia oil iliyokuwa recommended na car manufacturer. Mimi nami gari yangu nilishauriwa nitumie w50 tena mineral badala ya w30 tena fully synthetic we najutaaaa kwa yaliyonikuta! ila baada ya kuchange na kutumia w30 fully synthetic we gari nyepesi na haina vikelele kingine nunua oil kwa genuine dealer na sio kwenye viduka mfano toyota tanzania ana duka lake msimbazi kariakoo nunua hapo au kwa petrol station za total nunua hapo. Hizo valvoline au havoline kuwa makini nazo kuna kuna mtu namfahamu anafyatulia huko arabuni analeta bongo na anapiga pesa kama kawa!! na ndo zimejaa kwenye maduka meeeengi we ukiziona kwenye vidumu vyake na malabel ya havoline na valvoline unajua og! kumbe feki tupu! Kingine oil nunua mwenyewe usimpe hela fundi akununulie hata kama unamuamini vipi!!Gari yangu ina cc 1300 na kwa maelezo ya kwenye manual yake inasema kuwa Engine oil inayotakiwa kununuliwa ni 5W-30
Yeye ananambia kuwa kwa kuwa gari yangu engine yake imeshatembea zaidi ya kms 100,000 anashauri ninunue 20W-50 na anasema kwa hii gari haina haja ya kununua sythentic kutokana na kuwa engine yake imeshatumika sana na si gari ya umeme sana. Gari ni ya mwaka 2000. Toyota.
Sasa najiuliza nifanye nini....maaana muuzaji anasema kwa kuwa engine imeshatumika sana hiyo 5W-30 ni nyepesi sana.
Wataalamu tusaidiane katika hili.
hakika uzi huu umenibariki sana...mimi nilikuwa natumia SAE 40 kwenye nissan cc 1500...kwa kuwa km zake zimefikia mwisho naenda kununua 5w 30. Pia nilikuja kugundua baadae sana kuwa 5w 30 ndiyo oil recommended..Siku zote zingatia oil iliyokuwa recommended na car manufacturer. Mimi nami gari yangu nilishauriwa nitumie w50 tena mineral badala ya w30 tena fully synthetic we najutaaaa kwa yaliyonikuta! ila baada ya kuchange na kutumia w30 fully synthetic we gari nyepesi na haina vikelele kingine nunua oil kwa genuine dealer na sio kwenye viduka mfano toyota tanzania ana duka lake msimbazi kariakoo nunua hapo au kwa petrol station za total nunua hapo. Hizo valvoline au havoline kuwa makini nazo kuna kuna mtu namfahamu anafyatulia huko arabuni analeta bongo na anapiga pesa kama kawa!! na ndo zimejaa kwenye maduka meeeengi we ukiziona kwenye vidumu vyake na malabel ya havoline na valvoline unajua og! kumbe feki tupu! Kingine oil nunua mwenyewe usimpe hela fundi akununulie hata kama unamuamini vipi!!
Engines za Rav 4 (3S FE na 3S GE) zina range kubwa ya oil specs. 5W-30, 5W-40, 5W-50, 10W-30, 10W-40, 10W-50, 10W-60, 15W-40, 15W-50, na 20W-20.Msaada no oil IPI inafaa kw a rav4 model ya 1999 injini cc1990 beems vvti?
Wanakwambia weka yotote ile provided unabadili kwa wakati, kumbe wanakosea sana.hakika uzi huu umenibariki sana...mimi nilikuwa natumia SAE 40 kwenye nissan cc 1500...kwa kuwa km zake zimefikia mwisho naenda kununua 5w 30. Pia nilikuja kugundua baadae sana kuwa 5w 30 ndiyo oil recommended..
nikichojifunza mafundi wetu wakibongo hawapendi kusoma na kujifunza engine za kisasa.
wanaweza kukushauri jambo ukajuta.
Hii SAE40 nikiwasha gari asubuhi engine inavuma sana