Maelezo ya Mtaalam muuzaji na Maelezo ya waliotengeneza gari Yananichanganya sana. Msaada.

Mkuu
Mkuu pasipo kumung,unya maneno mafundi wengi teknolojia imewaacha sana na hii ni kwa sababu hawapendi kujiendeleza hivyo bado wana maarifa ya zamani sana! Kingine kwa kuwa kiingereza ni shida hivyo wanakosa kupata maarifa mengi sana kwa mfano kuna mtu anaitwa peter finn yupo youtube ana video nyingi namna ya kutatua ubovu wa magari ya toyota ila ndo hivyo tena english kwa mafundi wengi kituo cha polisi!
 
Wanakwambia weka yotote ile provided unabadili kwa wakati, kumbe wanakosea sana.
We acha tu...leo nimenunua total synthetic 5w 30 nimeweka nimeona gari imekuwa nyepesi sana..
Engine ina run very smoothly..nataka nisafiri nayo japo umbali w KM 50 Hivi nione consumption ya mafuta itakuwaje..
 
Kwa sasa ninaanza kupoteza imani na mafindi wa bongo hasa kwenye hizi injini za siku hizi ambazo zinatumia umeme mwingi..hawataki kuumiza vichwa wanakupa jibu simple tu injini imekufa nunua nyingine.

Mafundi wetu msiposoma tutawaamini kwenye kuziba pancha tu.
 

] 5W-30 for all around climate, maisha safi sana now, hiyo ni imetoka kwenye Manual ya Honda CR-V 2.0L 4 cylinder... ambayo ndiyo gari ninayotumia kwa sasa, mafundi wetu wa kibongo wanatuua sana wakati mwingine ukiwategemea
 
Gari yangu ya 2001, niliweka hiyo oil ya 20w-50, gari ikawa nzito, inavuma sana asubuhi, mbaya zaidi, fuel, consumption ikaongezeka sana. Gari ni 1800cc. Niliimwaga oil hiyo kabla ya wakati. Sasa natumia 5w-30 kulingana na specs za engine (1ZZ-FE).
Hiyo ndio sahihi hata manual za hayo magari zime specify. Nashangaa jamaa anamuamini fundi baadala ya kuwaamini waliounda hilo gari.
 
Ilikuja imetembea roughly 160,000km, hapa nimeitumia toka 2015. Nilipoweka 20w-50, nilienda 250km full tank likaisha. Nilipotoa hiyo oil nikaweka 5w-30, full tank nikaenda 430km. Hapa ishatembea roughly km elfu 35.
Ulinganisho mzuri sana huu
 
Mafundi wa sasa pasua kichwa sana wao watakwambia tu gari yoyote ya aluminium tumia oil no 50 ukimuuliza kwann no 50 na sio 40 atakwambia 40 inagandisha engine sasa unabaki unashangaa tu iweje 40 igandishe engine na 50 isigandishe engine wakati hiyo ambayo haigandishi engine ina viscosity kubwa kuliko 40? Kuweni makini sana na mafundi jaribuni kutumia manual za watengenezaji wa magari wenyewe
 
Hili nimeliona pia. Wengi hawajui chochote kuhusu oil. Wao ni "weka ile ya SAE 40 au 20w50, nzuri sana". Huku mteja ana gari dogo. Wiki iliyopita nimeona mtu mwenye Vitz kawekewa SAE40.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…