Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,805
- 17,850
Naweza kusema haya sasa ndiyo maelezo sahihi ambayo yana make sense, maana kama umemaliza form 4 naamini umesoma Geography, na hizi mambo za Mass Wasting na Mud Slides ni vitu tulivyosoma kwenye Physical Geography.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Dr. Derick Magoma, Ph.Dambaye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Manyara na aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Hanang (2020) akimueleza Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kilichotokea na kusababisha mafuriko tope (mudslides) Wilaya ya Hanang.
NB: Mambo ya Hanang ni vizuri ukaelezwa na watu wa Hanang (maana wanaijua Hanang yao vizuri zaidi) kuliko kupewa simulizi na Jenista Mhagama na Bashungwa waliokuwa Dar es Salaam siku ya tukio. Mwisho, wataunda tume kuchunguza mafuriko tope.
Poleni sana watu wa Hanang, tupo pamoja katika wakati huu mgumu kwa maombi na kwa kutoa nguvu kazi kusaidia kurejesha hali ya Hanang katika utimamu wake wa awali. Tunafahamu, siyo rahisi lakini tujitie nguvu na wote tumshukuru Mungu.