Maelfu waandamana Ubelgiji kupinga Mageuzi ya Serikali ya kubanwa kwa Matumizi

Maelfu waandamana Ubelgiji kupinga Mageuzi ya Serikali ya kubanwa kwa Matumizi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Maelfu ya watu wamejitokeza barabarani jijini Brussels, Ubelgiji, wakishiriki katika mgomo wa kitaifa kupinga mageuzi ya serikali na hatua za kupunguza matumizi, ambazo zimepelekea usafiri wa anga na wa umma kusimama

Vyama vikubwa vitatu vya wafanyakazi nchini humo vimeungana kulalamikia sera za Waziri Mkuu Bart de Wever na serikali yake ya mrengo wa kulia, ambazo zinahusisha mabadiliko ya pensheni na mipango mingine ya kupunguza nakisi ya bajeti ya taifa

Shughuli za usafiri zilisimama katika uwanja wa ndege wa Charleroi, ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini, ulifungwa kabisa, huku safari nyingi zikiwa zimefutwa katika Uwanja wa Ndege wa Brussels

Ingawa treni ziliendelea kufanya kazi, usafiri wa mabasi, tram na treni za chini ya ardhi ilisimama jijini Brussels

Bandari ya Antwerp bandari ya pili kwa ukubwa barani Ulaya nayo ilisimamisha shughuli hadi Jumatano kutokana na upungufu wa wafanyakazi. Takribani meli 100 zilisubiri ruhusa ya kutia nanga katika bandari tatu nchini humo, kwa mujibu wa huduma za baharini na pwani za MDK

Tangu Bart de Wever, mwanasiasa wa chama cha kitaifa cha Kiflemish, alipoingia madarakani Februari mwaka huu, Ubelgiji imekuwa ikikumbwa na migomo kadhaa

Polisi walisema takribani watu 80,000 walikuwa wamejiunga na maandamano hayo mjini Brussels. Wafanyakazi wa sekta ya umma waliandamana kupinga sera za kubana matumizi na kile wanachokiona kama mwelekeo wa serikali kuelekea mrengo wa kulia kisiasa

Waandamanaji walijaa mitaani wakiwa wamevalia rangi nyekundu na kijani — rangi za vyama vikuu vya wafanyakazi

Moja ya hoja kuu za vyama hivyo ni mpango wa serikali kuongeza idadi ya siku ambazo Wabelgiji wanatakiwa kufanya kazi kabla ya kustahili pensheni, pamoja na kufutwa kwa mipango maalum ya sekta kama jeshi na reli

Serikali ya De Wever pia imependekeza hatua mpya, ikiwemo kuweka ukomo wa miaka miwili kwa mtu kudai posho ya ukosefu wa ajira. Aidha, imepanga kupunguza zaidi matumizi katika bajeti ijayo, huku mapendekezo kama kupunguza posho za watoto au kuongeza kodi ya VAT yakichunguzwa.

Kuingizwa kwa umri wa juu wa kustaafu kulipitishwa miaka 10 iliyopita kabla ya serikali ya De Wever, lakini bado wananchi wengi hawakubaliani nayo. Serikali inataka kulinda hatua hiyo na kufanya kustaafu mapema kuwa ghali zaidi

Si serikali ya Ubelgiji pekee inayolazimika kupunguza matumizi. Mfumo tata wa utawala wa Ubelgiji pia hat serikali za maeneo mengine zinachukua hatua kama hizo

Katika eneo la Wallonia, ambalo lina wazungumzaji wengi wa Kifaransa, serikali ya muungano imetangaza kuwa walimu wa sekondari watapaswa kufanya kazi saa mbili zaidi kwa wiki. Walimu wengi waliungana na maandamano hayo

Ingawa maandamano yalikuwa kwa kiasi kikubwa ya amani, kuliripotiwa matukio kadhaa ya uharibifu wa mali na uchomaji moto asubuhi, huku baadhi ya watu waliovaa barakoa wakirushiana mawe na polisi baadaye mchana



Chanzo: BBC
 
Dunia Tambarale, kumbe ugumu uko dunia nzima, mi nilitake niende huko kukwepa ugumu wa hapa kwetu kumbe huko nako kuna maandamano.
 
Back
Top Bottom