Maelfu ya 'Jobless Graduates' wanaishije mtaani miaka yote?

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Habarini ndugu zangu.

Ukiwa Chuo unawezeshwa na wazazi au Bodi ya Mikopo kwa ajili ya malazi, chakula, mavazi na mengineyo mengi, na hivyo kupata hadhi/status ya kuonekana kweli kijana wa Kitanzania.Kuna vijana hujibana na kununua mpaka simu, vitu vidogo vya ndani na mwishowe wengine hupata mpaka wachumba chuoni.

Ukimaliza chuo, unarudi nyumbani. Hupewi posho yoyote kwa ajili ya kukuwezesha kuishi mtaani. Kuna vitu vidogo mfano Bundle za Dakika, Internet ni muhimu sana kwa vijana kwa ajili ya kuperuzi huko duniani ili kujua yanayoendelea.

Kuna vijana wana miaka 12, 8, 7, 5, 2 mtaani bila kazi yoyote. Hawaingizi chochote na still wana mahitaji yaleyale ya siku zote (vocha, nguo, malazi, kuhudumia wenza wao n.k). Mbaya zaidi wanapoomba kazi wanaambiwa ni lazima wawe na uzoefu wa angalau miaka 3 ama 5. Mtu anapataje uzoefu kwa situations kama hizi?

Vijana waliomaliza vyuo mtaani wanaishije mtaani bila ajira miaka nenda rudi?
 
Habarini ndugu zangu.

Ukiwa Chuo unawezeshwa na wazazi au Bodi ya Mikopo kwa ajili ya malazi, chakula, mavazi na mengineyo mengi, na hivyo kupata hadhi/status ya kuonekana kweli kijana wa Kitanzania.Kuna vijana hujibana na kununua mpaka simu, vitu vidogo vya ndani na mwishowe wengine hupata mpaka wachumba chuoni.

Ukimaliza chuo, unarudi nyumbani. Hupewi posho yoyote kwa ajili ya kukuwezesha kuishi mtaani. Kuna vitu vidogo mfano Bundle za Dakika, Internet ni muhimu sana kwa vijana....kwa ajili ya kuperuzi huko duniani ili kujua yanayoendelea...

Na hiyo mikopo itarudushwaje wakati mikopo pia inatolewa Zaidi Kwa wale waliosoma shule za serikali kuanzia la 1 mpk kidato Cha 6, wanasema waliosoma private hawatakiwi kupewa mkopo wao wanajiweza , sasa hapo itakuwaje? Wakati Pengine na waliosoma shule za private wangepata ingesaidia ulipaji pia.
 
Hiyo Mikopo ya loan body Ni janga jingine zito
 
Maisha ya kutokuwa na kazi kama umesoma ukitegemea kuajiriwa yanaumiza sana,ila kama ulijiandaa kisaikolojia kuwa ukimaliza chochote kitakachokuja mbele yako katika maisha utafanya,basi maisha ni rahisi sana...
"... kama ulijiandaa kisaikolojia..."[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]nimekuelewa hapo!
 
Habarini ndugu zangu.

Ukiwa Chuo unawezeshwa na wazazi au Bodi ya Mikopo kwa ajili ya malazi, chakula, mavazi na mengineyo mengi, na hivyo kupata hadhi/status ya kuonekana kweli kijana wa Kitanzania.Kuna vijana hujibana na kununua mpaka simu, vitu vidogo vya ndani na mwishowe wengine hupata mpaka wachumba chuoni.

Ukimaliza chuo, unarudi nyumbani. Hupewi posho yoyote kwa ajili ya kukuwezesha kuishi mtaani. Kuna vitu vidogo mfano Bundle za Dakika, Internet ni muhimu sana kwa vijana....kwa ajili ya kuperuzi huko duniani ili kujua yanayoendelea...

Kuna vijana wana miaka 12, 8, 7, 5, 2 mtaani bila kazi yoyote. Hawaingizi chochote na still wana mahitaji yaleyale ya siku zote (vocha, nguo, malazi, kuhudumia wenza wao n.k). Mbaya zaidi wanapoomba kazi wanaambiwa ni lazima wawe na uzoefu wa angalau miaka 3 ama 5. Mtu anapataje uzoefu kwa situations kama hizi?

Vijana waliomaliza vyuo mtaani wanaishije mtaani bila ajira miaka nenda rudi?
Mungu ndio kimbilio letu
 
Wanaishi kwa kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao.
 
Mtaani huwa wanajifunza ujuzi mpya, nina rafiki yangu sahivi ni dereva wa magari ya mizigo anaenda Malawi,congo,Rwanda,Burundi, Mwingine ni kondakta wa bus za mikoani Dar-Bukoba anamaisha poa kiasi fulan posho kila nwisho wa Safar anasema hakosi 40k

Mwingine ni fundi seat cover wa magari huyu sahiv anamaisha poa hataki tena hata ajira, kajenga nyumba yake ndogo yenye hadhi ya kisasa na kaboresha sana ofisi amekua na wateja wengi kwa siku anasema hakosi 30k akifanya marekebisho madogomadogo na akifanya kaz kubwa siku nyingine hadi 200k

Mwingine alianza na bajaji kamaliza mkataba ni yake kwa sasa.

Wengi waliomaliza chuo kwa kipind cha karibun sijaona wakiajiriwa ila wanapiga mishe za kujiajiri
 
Tumejiongeza Mkuu wewe unadhani tutakaa tu tusubirie ajira miaka yote hiyo bila kufanya chochote.

Ila kuna watu wanatoka katika mazingira magumu kiasi kwamba wanashindwa kujiingiza katika shughuli zozote kutokana na kukosa kipato au mtaji na kazi zenyewe ni za shida.

Maisha haya tunapambana tu na kumuomba Mungu azidi kutusimamia na kutuongoza.
 
Wanaishi vizuri km wapo Mamtoni hata sisi wenye vibarua Tunasubiri.

. Wezi wa mitandaoni
. Fursa zote za kitapeli waasisi ni wao
. Ndio wale wanakosea kutuma pesa inaingia kwenye namba yako
. Kuna wengine hawataki hata kuajiriwa kwa Sababu ya Madili.
. Wanaonisikitisha ni wale jamaa wameolewa.
 
Ukimaliza elimu ya shule unaingia rasmi kupata elimu ya mtaa. Ili uipate hiyo ya mtaa inabidi ifike a point ambayo hata kula ni kwa manati, hapo ndo ubongo unafunguka.

Pia over expectations zinapungua. Unatoka kwenye ndoto za maghorofa unarudi kuwa humble na kuanzia chini kabisa ambapo unaanza na ndoto za kuweza kula tu for that day. Then you build from there taratibu mpka unakua don if you are lucky.
 
Back
Top Bottom