- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumeibuka chapisho la tangazo linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, likiwa na kipande cha video kinachomuonesha Abubakari Bakhresa akidai kuwa kampuni yake ya Azam inatoa fedha kwa Watanzania kuanzia TSh 4,000,000 hadi 6,500,000, huku usajili ukidaiwa kufanyika ndani ya siku tisa.
Katika chapisho hilo, pia kuna kiungo kinachoonekana kuhusiana na tovuti ya The Citizen, kikiwa na ujumbe unaosema: “Serikali mpya, fursa mpya: Maelfu ya Watanzania tayari wanatumia fursa hii kupata zaidi ya TSh 4,000,000 ndani ya siku 30.”
Je ni upi ukweli wa Tangazo hilo?
Katika chapisho hilo, pia kuna kiungo kinachoonekana kuhusiana na tovuti ya The Citizen, kikiwa na ujumbe unaosema: “Serikali mpya, fursa mpya: Maelfu ya Watanzania tayari wanatumia fursa hii kupata zaidi ya TSh 4,000,000 ndani ya siku 30.”
Je ni upi ukweli wa Tangazo hilo?
- Tunachokijua
- Kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na kipande cha video kinachomuonesha mtangazaji wa kituo cha runinga cha CGTN akieleza kuwa wananchi kwa sasa wanaweza kupata hadi Shilingi Milioni 4, huku mnufaika akitakiwa kuchangia kiasi cha shilingi laki sita na elfu hamsini kwa ajili ya usajili na ni ndani ya siku saba tu.
Taarifa hiyo ilidai kuwa kiasi hiko na utaratibu huo umetangazwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa, kupitia kwa Abubakar Bakhresa.
Uhalisia wa madai hayo ni upi?
JamiiCheck imefuatilia n akujirirdhisha kuwa video hiyo imehaririwa kwa kutumia kwa teknolojia ya Akili Unde.
Ufuatiliaji umebaini kuwa video hiyo imeharirirwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde aina ya DeepFake kwa kuhariri na kumuwekea maneno mtangazaji wa CGTN pamoja na Abubakar Bakhresa.
Video imehaririwa kutoka katika video halisi ya CGTN iliyochapishwa katika kituo chaneli yao ya Youtube December 29, 2025. Video hiyo ni ya kipindi chenye jina AFRICA IN 2025 kilichokuwa kikitangazwa na Penina Karibe.
Lakini pia Bakhresha group walikanusha kuhusika na tangazo hilo.
Hivyo video potoshi ilitumia Teknolojia ya DeepFake kwa kuhariri video halisi kwa kuondoa maneno halisi na kuweka maneno hayo ya ulaghai akieleza kuwa kila mwananchi wa Tanzania anaweza kupata kiasi hiko cha fedha.