AlexOnesmo
New Member
- Jul 22, 2023
- 2
- 1
Ili maendeleo yawepo ndani ya nchi viongozi wanatakiwa wawe kitu kimoja bila kujali siasa, udini, ukabila, pia upendeleo.
Nchi inapaswa kuwa na viongozi waliowadilifu, wenye kujituma na wenye chachu ya maendeleo ya nchi yao, na ili kupata hayo yote wananchi wanatakiwa waweze kuchagua kiongozi aliebora ambae amekidhi vigezo vyoote vya kuwa kiongozi na siyo wale wanaotoa rushwa au hongo ya aina yoyote ili kupata uongozi, au bila kujali vyama kuwa tuchague huyu kwakuwa ni chama flani kwakuwa unamapenzi na chama hicho.
Tukifata hayo yote kwenye uchaguzi wa viongozi wetu lazima tukapata viongozi shupavu na wenye kuipenda nchi yao na wasiopenda hongo au rushwa na nchi itajengeka vizuri.
Pia viongozi wenyewe wanapaswa kujadili kwa pamoja kuhusu miondombinu iliyopo ndani ya nchi yao kwa pamoja bila kupingana ili kuweza kuisimamia bila kuhalibiwa na wanaopenda rushwa au wenye tamaa na mali za serikali.
Na wanachi wanapaswa kuwa na ushirikiano na viongozi wa nchi wanaowaongoza kwa kuwapa taarifa mbalimbali kwa uharibifu wa miundo mbinu ya nchi kwani siyo kila jambo la uharibifu linafanywa na viongozi pekeake hata wananchi wapo wengine ambao siyo waadilifu kwenye nchi yao.
Kuwa na ulinzi imara kila Kona ya nchi, serikali inatakiwa kuweka ulinzi kila sehemu ya nchi ili kusaidia wizi na uharibifu wowote ndani ya nchi Kama vile upolaji wa mali za wananchi pia mali za serikali na kulinda umomonyoko wa maadili ndani ya nchi, na kulinda mipaka ya nchi kwa kuzuia laia ambaye siyo wa nchi kuingia ovyo ovyo kwani wengine wanaweza kuwa si wazuri ndani ya nchi.
Pia serikali iwe na mikutano mara kwa mara na wananchi wake ili kupata changamoto wanazozipitia za maendeleo ya nchi, kuwasikiliza wananchi ni sehemu gani ya nchi panapaswa kurekebishwa au kutengenezwa na kushirikishana namna gani uongozi unapaswa kuwa imara ili kuijenga nchi.
Yote kwa yote, Uimara wa nchi unaanzia kwa viongozi kushikamana bila kujali vyama vya siasa, kukaa kwa pamoja kuijenga nchi, kuwa na ulinzi ulioimara, uchaguzi wa viongozi wa nchi kwa kufata utenda kazi, na serikali kuwa karibu na wananchi wake kujua kelo za wananchi wake, kuwapa wanachi wake miundombinu ya kudumu mfano maji, barabara nzuri, umeme na vingine vyenye kujenga nchi kwa ujumla.

Upvote
1