SoC04 Maendeleo katika elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kitukula

Member
Joined
Jul 2, 2022
Posts
6
Reaction score
5
Sekta ya elimu ni sehemu kubwa katika maendeleo ya taifa, elimu inasaidia kwa asilimia kubwa maendeleo ya taifa katika uongozaji na jpandaji wa uchumi.

Elimu yetu kwakiasi kikubwa imekuwa ni elimu ya mtu kujinasua katika ngazi ya kifamilia na huku asilimia chache ikitumika katika maendeleo ya taifa.

Maendeleo yanayoitajika miaka ijayo
1. Upatikanaji wa elimu yenye kujikita katika kutoa ujuzi kuliko kufaulisha.

Elimu yetu imejikita katika utoaji wa ufaulu kwa kiasi kikubwa na wala sio maarifa au ujuzi ambapo inapelekea upatikanaji wa wasomi ambao awajaelimika nikimaanisha kwa asilimia kubwa watu wanasoma vitu ambavyo awavipendi na awawezi kuvitumia na wachache wakisomea ndoto zao.


Picha ikionesha watu wanapata ujuzi
chanzo cha picha : mtandaoni


2. Upatikanaji wa vifaa vya kujifunza kwa vitendo.
Kwa salimia kubwa vifaa vya kujifunzia kwa vitendo avipatikani kwa kiwango kinachoitajika unakuta taasisi ya elimu ina wanafunzi wengi kuliko vifaa ambapo wachache watapata kujifunza vizuri kwa vitendo, hii itasaidia kupata wataalamu zaidi nchini na kuacha kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchi mfano madaktari.


Chanzo cha picha: mtandaoni

3. Uanzishaji wa shule zingine za vipaji. Ambapo itasaidia kutengeneza mazingira mazuri ya mtoto kukua katika anachokipenda wanasema "ukitembea kwenye ndoto zako we ni siraha" kuna vipaji ambavyo vimezikwa mitaani na vingine kupotea kabisa, mfano mitaani tuna watoto wa mtaani, wezi na wengine waliopoteza dira ya maisha na sio kwamba maisha yao ni yakutaka kuwa wezi au kuishia mitaani hapana ni kutokana na mifumo yetu imekandamiza ndoto zao mitaani tuna waendesha magari ya mashindano, kuna wacheza kikapu, wanamuziki na wengine wengi lakini kutokana na mifumo yetu kujali utoaji wa elimu ya darasani.


mfano wa picha ikionesha wanufaika wa mafunzo ya magari aina ya formula one
Chanzo cha picha: mtandaoni


4. Utoaji wa wanafunzi kwenda kujifunza nje ya nchi.

Wa nchi zingine wana mfumo wa kutoa wanafunzi kuwapeleka nchi nyingine kwa lengo la kujifunza na kuongeza ujuzi mfano nchi za magharibi huwa zinatoa wanafunzi wanaosomea mambo ya afya kuja kufanya masomo ya field nchi za afrika hii inawasaidia kuongeza ujuzi katika kile wanachosomea.


chanzo cha picha: mtandaoni

5. Kwa miaka ijayo elimu isaidie kutetea taifa na wananchi wake.
Tunaidadi kubwa ya watu ambao awajasoma ambao haki zao wanategemea kutetewa na waliosoma na wengi awazijui haki zao binafsi kiasi wanashindwa kutoa mchango katika hali zinazoamuliwa katika nchi wnashindwa kupaza sauti kutokana na kutozijua haki zao binafsi katika maendeleo ya nchi.

6. Upatikanaji wa mazingira rafiki ya kielimu .
Kwenye swala la mazingira nayo yana mchango mkubwa wa kujifunza mfano miundombinu inayosaidia upatikanaji wa elimu hususani miundombinu ya shule za vijijini


Chanzo cha picha: mtandaoni

Kwa kumalizia uboresha wa elimu ukiwa mzuri itasaidia upatikanaji wa wataalamu na kuacha kutegemea nchi zingine kwa ajili ya wataalam, pia utoaji wa ujuzi zaidi utasaidia upungufu wa watu wanaotaka kuajiliwa huku wakitumia ujuzi wao kama kipato. Na maendeleo haya nikwa shule za kata kwa sababu ndio kimbilio na tegemeo la wananchi walio wengi katika jamii zetu.
 
Upvote 2
Kwa kumalizia uboresha wa elimu ukiwa mzuri itasaidia upatikanaji wa wataalamu na kuacha kutegemea nchi zingine kwa ajili ya wataalam, pia utoaji wa ujuzi zaidi utasaidia upungufu wa watu wanaotaka kuajiliwa huku wakitumia ujuzi wao kama kipato.
Sawa sawia. Elimu, elimi, elimu stahiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…