mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
wakati wa kuanza ni sasa mpaka ujifunge kibwebwe utakuwa umeachwa, tumfunge paka kengere sasa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni upotoshaji kusema kuwa madai ya katiba mpya ni harakati za chadema. Ieleweke kuwa watanzania walianza kudai katiba mpya tangu zamani. Actually, mmoja wa wanasiasa wa kwanza kudai katiba mpya alikuwa ni christoper mtikila wa dp ambaye alisema way back baada ya vyama vingi kuruhusiwa in 1992 kuwa asingeshiriki kwenye uchaguzi wa 1995 bila kuwepo kwa katiba mpya kwa kuwa iliyopo ilitungwa na makada wa ccm mwaka 1977 chini ya utawala wa chama kimoja. Laiti vyama vyote vya upinzani vingesimama pamoja tangu 1995 na kukataa kushiriki kwenye uchagizi mkuu basi tungekuwa na katiba mpya sasa hivi.
Chadema kimetoa msukumo mpya kudai katiba mpya, lakini kamwe harakati hii haikuasisiwa na chadema. Ni wananchi wenyewe wa tanzania wanaodai katiba mpya, pia ngo zote zinaunga mkono wazo hili.
acha kudanganya umma madai ya katiba mpya kwa kizazi tulicho nacho ni madai ya msingi na yamesimamiwa wakati wote na chadema ila katiba mpya ni demand ya kihistoria toka enzi za mwalimu and u cant identify crzy mtikila as the mwamzilishi yeye ni kibaraka tuu na hayo madai ameyakuta,hata ndani ya ccm wapo watu 1960"s walishapinga katiba ya jamhuri wa muungano wa tz.
rais mstaafu wa awamu ya tatu, benjamin mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa jumuia ya afrika mashariki, zinahitaji kuwa na katiba mpya, ikiwemo tanzania."nakubaliana na harakati za chadema na vyama vingine vya upinzani kudai katiba mpya ni wakati sasa ccm ifikiri juu ya kuwapa wa tanzania katiba mpya kwani kelele zimekuwa nyingi sana"
mkapa alisema hayo katika mkutano mkuu wa chama cha wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini bujumbura nchini burundi, mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya rais mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na balozi liberata mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.
Alisema kama nchi wanachama zikiwa na katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.
Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye katiba zilizopo.
Alisema katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.
Alisema uundwaji wa katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa.
"tunakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuunganisha umoja wetu wa kitaifa… kuna baadhi wamegusia juu ya matatizo yetu ya kisiasa na baadhi yetu tunafikiri kuwa siku ya kuadhimisha uhuru ni kilele cha kujenga umoja wetu wa kitaifa… uhuru wetu wa katiba tulizonazo ni ushahidi wa dhuluma hii.
"…hatuna katiba zingine zaidi ya zile ambazo tumezirithi kutoka kwa wakoloni, katiba ambazo hazina umakini, tunahitaji mpya," alisema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo tanzania daima imefanikiwa kupata nakala yake, rais mkapa alisema chaguzi nyingi zitakuwa huru na haki endapo kutakuwa na katiba bora.
Akinukuu maneno ya mwandishi wa vitabu duniani (hakumtaja), ambaye pia ni mwanafalsafa aliyesema, ‘chaguzi za haki ni muhimu kwa katiba bora.'
alisema katika uundaji wa katiba mpya, ni lazima kuwepo makubaliano maalum, kwa pande zote za kisiasa, kijamii na kijiografia, huku kanuni pamoja na mambo muhimu yakizingatiwa.
Alisema malumbano na migororo ndani ya nchi, yanasababishwa na muundo wa katiba zinazoonekana kutokidhi haki na usawa.
"katiba ndiyo moyo wa nchi, moyo wa mwanadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi… hivyo kwa kuangalia mbele tunahitaji kuundwa kwa katiba na mihimili yote ya nchi, tunahitaji katiba huru itakayotulinda katika hatari," alisema mkapa.
Akitoa mfano, rais mkapa alisema kumekuwa na sakata la uanzishaji wa mahakama ya kadhi katika nchi za tanzania na kenya, huku akisistiza kama lingekuwa ndani ya katiba isingesababisha malumbano makubwa.
Kauli ya rais mkapa, imekuja wakati watu wa kada mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wasomi na wanaharakati wakiishinikiza serikali kufanya marekebisho ya katiba iliyopo, kwa madai kuwa haikidhi matakwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, waziri wa sheria na mambo ya katiba, celina kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na katiba mpya, kitendo kilichoonekana kupingwa na watu wengi.
Waziri kombani alisema katiba iliyopo itaendelea kutumika kwani, serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha katiba hiyo.
Jaji mkuu mstaafu mark bomani naye juzi alivunja ukimya na kusema kinachoisumbua serikali iliyoko madarakani ni woga ambao hauna msingi wowote.
Alisema katiba iliyopo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati, kwani wakati huu inakinzana katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora.
Naye profesa wa chuo kikuu cha dar es salaam na mwanaharakati maarufu, issa shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1998 kamati ya white paper iliyoundwa chini ya jaji robert kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya rais mkapa.
Yale maneno mekundu naona son of peasant kachomekea tu. Madai ya katiba mpya ni ya muda mrefu na ni ya watanzania! Wanaharakati, CHADEMA na vyama vingine vya siasa vinawawakilisha tu wananchi. Moja ya madai ya msingi ya CHADEMA ni katiba mpya itakayopelekea sio tume huru ya uchaguzi bali inayokidhi haja ya watanzania wote kwa mazingira ya sasa na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi ikiwa ni pamoja na kuondoa sheria zote kandamizi.Du kumbe madai ya katiba mpya ni harakati za CHADEMA na sio watanzania na haswa wanaharakati walioanzisha mapambano haya kabla ya mwaka 1992 ilipoanzishwa Chadema...By the way, kila ninapomsikiliza Mbowe na hata Slaa huwa nasikia maombi ya mabadiliko ya katiba na sio Katiba mpya......
unafiki mtupu !!!!!!!!!hana uthubutu wa kuongea mbele ya kikwete.he is more of international figure and a coward ,traitor in his homeland.
YOTE YANA MWISHO,IKO SKU TUTAPATA UHURU WETU NA KATIBA MPYA.
Mkuu umesahau Mh. Waziri Mkuu mstaafu Sumaye hakujua kwanini Tanzania ni masikini kwa miaka yote kumi aliyokuwa madarakani MPAKA alipoenda kusoma Marekani ndipo alipogundua kwanini watanzania ni masikini!!
labda pengine viongozi na wanasiasa wetu wanahitaji refresher course kila baada ya miezi sita!!
Mkapa sio kwamba hawezi kuongea mbele ya Kikwete la hasha, tatizo hapa ni system inayomuzunguka kikwete ni chafu sio kawaida hivyo naona hata akishauri kitu kizuri ataonekana kama yuko against..Mkapa ni jasiri na akiamua anaweza sana,kwani yeye ahajui kuwa uchaguzi ulikuwa wa kisanii?? anajua sana?