Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

wakati wa kuanza ni sasa mpaka ujifunge kibwebwe utakuwa umeachwa, tumfunge paka kengere sasa
 

acha kudanganya umma madai ya katiba mpya kwa kizazi tulicho nacho ni madai ya msingi na yamesimamiwa wakati wote na chadema ila katiba mpya ni demand ya kihistoria toka enzi za mwalimu and u cant identify crzy mtikila as the mwamzilishi yeye ni kibaraka tuu na hayo madai ameyakuta,hata ndani ya ccm wapo watu 1960"s walishapinga katiba ya jamhuri wa muungano wa tz.
 
Du kumbe madai ya katiba mpya ni harakati za CHADEMA na sio watanzania na haswa wanaharakati walioanzisha mapambano haya kabla ya mwaka 1992 ilipoanzishwa Chadema...By the way, kila ninapomsikiliza Mbowe na hata Slaa huwa nasikia maombi ya mabadiliko ya katiba na sio Katiba mpya......
 

katiba ya tanzania ni ya mwaka 1977 huo mwaka 1960 umetoa wapi wewe au unajiandikia tuuu hata mambo huyajui??
 
Hoja ni katiba mpya mimi ninafurahi moto unazidi kuwaka kudai katiba kazi ya wana jf ni kutoa elim ya uraia na kupeleka habari hii tanzania nzima. Ninajua chadema wana kipaumbele cha kudai katiba which is great, lakini tunajua pia chadema peke yao haitoshi tunahitaji watanzania wote, na chadema ipo teyari kusimamia hili kwa nguvu zote. Tusonge mbele bila unafiki pamoja tunaweza.
 
Tunahitaji katiba mpya yenye kuzingatia yafuatayo:-

1. Rais wa JMT uwe wa kupokezana Bara na Zanzibar kila baada ya miaka kumi- kulinda muungano wetu, how? kila chama kitatakiwa kikatiba kumsimamisha mbara/mzenj ikiwa ni wakati wao...hivi watakuwa wanachuana wenyewe kwa wenyewe i.e. wabara vs. wabara, wazenj vs. wazenj

2. Mawaziri wasiwe wabunge na wabunge wasiwe mawaziri

3. Kusiwe na wabunge wa viti maalum, wala wakuteuliwa na Rais

4. Wizara ziwe kwa mujibu wa katiba na shughuli zake ziwe ndani ya Katiba..Rais asiwe na uwezo wa kuongeza wizara hata moja mpaka aliombe bunge...wizara ziwe 13 tu..

5. Cheo cha ukuu wa mkoa na wilaya ifutwe wabakizwe wakurugenzi

6. Cheo cha katibu mkuu wizarani ifutwe waziri anatosha (ikiwa kipnegele 2) itakubaliwa..
7...
Tujadili!
 
katiba mpya sio dili sana kwa sasa tuna matatizo mengine yapewe kipaumbele jamani katiba gharama sana
 
yote sawa ila la rais atoke bara au zenj haina tija kubebana kusikokuwa na maslahi ya taifa, weka private candidate aruhusiwe, na hayo mengine yote na mengine mengi tulishajadala hapa JF
 

hongera kwa kutuletea hii hapa wengine hatuna muda na magazeti ila tuna muda sana na jf big up
 
Yale maneno mekundu naona son of peasant kachomekea tu. Madai ya katiba mpya ni ya muda mrefu na ni ya watanzania! Wanaharakati, CHADEMA na vyama vingine vya siasa vinawawakilisha tu wananchi. Moja ya madai ya msingi ya CHADEMA ni katiba mpya itakayopelekea sio tume huru ya uchaguzi bali inayokidhi haja ya watanzania wote kwa mazingira ya sasa na demokrasia ya mfumo wa vyama vingi ikiwa ni pamoja na kuondoa sheria zote kandamizi.
 
Mkapa sio kwamba hawezi kuongea mbele ya Kikwete la hasha, tatizo hapa ni system inayomuzunguka kikwete ni chafu sio kawaida hivyo naona hata akishauri kitu kizuri ataonekana kama yuko against..Mkapa ni jasiri na akiamua anaweza sana,kwani yeye ahajui kuwa uchaguzi ulikuwa wa kisanii?? anajua sana?
unafiki mtupu !!!!!!!!!hana uthubutu wa kuongea mbele ya kikwete.he is more of international figure and a coward ,traitor in his homeland.
YOTE YANA MWISHO,IKO SKU TUTAPATA UHURU WETU NA KATIBA MPYA.
 
Kinanifuhisha kuwa hata wale walopinga katiba mpya sasa wanaanza kuwa waumini. Heko wapiganaji Dr Slaa, Prof Lipumba, Prof Shivji, Prof Chrid Maina.
Naamini safari si ndefu watu wataelewa maana ya katiba mpya na faida zake.
 
Kinanifuhisha kuwa hata wale walopinga katiba mpya sasa wanaanza kuwa waumini. Heko wapiganaji Dr Slaa, Prof Lipumba, Prof Shivji, Prof Chrid Maina.
Naamini safari si ndefu watu wataelewa maana ya katiba mpya na faida zake.
 
....Tume huru ya uchaguzi
....Madaraka ya ki-mungu mdogo ya urais yapunguzwe.
 

Wallah nakuunga mkono na i am so serious.
 

Mkuu naona hapa kujaelewa tatizo au maada ya waheshimiwa. he might be jasiri or whatever we call him. but he was the president of this poor tz for the period of ten yearz. kwa KISANGA iliweka wazi yote haya!?
 
Hiyo kauli imemtoka mdomoni au moyoni? Nahisi kama anachoongea sicho anachofikiri moyoni.
 
Si amini kama haya yanatoka kwa bro. Nkapa. Anyway kanena. Nashauri tu jk aliweke hili kwenye ilani ya 2015. Ila mchakato wake uanze sasa.
Kwasasa tufikirie kujenga nchi.
 
Ni kweli nchi nyingi za Afrika, Tanzania ikiwemo zinahitaji katiba mpya. Lakini hili tamko la Mkapa ni la kushangaa kwani alikuja juu za pale tume yake mwenyewe iliposhauri umuhimu wa kuwa na katiba mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…