Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

misukumo, migomo na maandamano ya kila kukicha ndio itakayoleta Katiba mpya.

Lakini kama mambo yenyewe ndo yanazungumziwa JF tu kisha huko mitaani watu wanachofuatilia ni kombe la Chalenge na mashindano ya Tusker Project Fame basi tutakuwa tunajidanganya tu.

CCM mtaji wao mkubwa ni umbumbumbu wa baadhi ya watanzania walio wengi.
Hivyo hata ktk swala hili hawana wasiwasi coz waliowengi ni mbumbumbu so hawaelewi hata hiyo katiba ina ganda la rangi gani.

SO Kila mmoja wetu mwenye uchungu na ajitahidi kuingia mtaani na kuamsha mbumbumbu ambao ni mtaji wa CCM.

Mfano:
Tazama maeneo ambayo Chadema wameshinda kisha matokeo yakataka kuchakachuliwa, nguvu ya wananchi ilisimama imara na kuweza kutoa shinikizo kwa tume mpk matokeo yaliyo halali yakatangazwa.
Lakini kama wananchi wa maeneo hayo wangekuwa kimyaaa kama sisi tunavyodai katiba basi hakika majimbo ya Chadema leo hii yasingefika hata 10.
 
Ndugu BongoTz,
Hoja yangu ni - tutafanya makosa kuwa na wataalamu wa katiba wakati hata hatujui watanganyika wanataka nini...
. Umesema ---"kuwashirikisha wananchi wote mijini na vijijini katika zoezi hili......." Kwa petition link uliyotuelekeza sioni vipi utamhusisha kaka Karumanzila ambaye hata simu ya mkononi hana uwezo wa kuipata kujiunga na kupeana mawazo kupitia njia uliyotuelekeza..
Naomba kusahihishwa.......
Mkuu, Adili: Kuhusu kuwashirikisha wananchi wa vijijini (akiwemo kaka Karumanzila), napenda kukuhakikishia kuwa taratibu nzuri za kufanikisha zoezi hilo tayari ziko mahala pake. Mfano, tunajiandaa kuchapa nakala nyingi (2 million+), ambazo tutazisambaza kwenye mashule ya sekondari, vyuo vikuu, na tasisi mbalimbali za umma. Zaidi ya hilo,tumepanga pia kuzungukia sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko mikubwa ya watu (makanisani/misikitini/masinagogini), kwenye mechi mbalimbali za mpira wa miguu, kikapu, pete, ili kuwahamasisha wananchi wazalendo washiriki kikamilifu kwenye zoezi hili. Plus, in the next few days, nitapost another copy here (PDF), ambayo inaweza kuwa downloaded, then copies nyingi zikatolewa na hivyo kuwafikia wananchi wengi wasio na access ya internet. Ila nitatoa maelezo ya namna ya kuzituma hizo forms mara tu baada ya kuwa zimejazwa kwasababu tutahitaji kuweka kumbukumbu ya idadi halisi ya watu waliokwisha saini Petition. Hope nimejibu swali lako. Thank you.
 
Yaani Mkapa alipokuwa madarakani hakuona tatizo hilo, baada ya kufaidika na katiba hiyo sasa ndipo anafungua macho na kuiona ina udhaifu? si ajabu kuwa hata Kikwete atakapoondoka madarakani ndipo atakaposema kuwa Tanzania inahitaji Katiba mpya
Mkuu, kichuguuu kuna msemo usemao, adui wa adui yako ni rafiki yako: Of course, Mkapa alikaa kimya na kushindwa kuzungumzia umuhimu wa katiba mpya kipindi cha utawala wake, lakini hiyo sio sababu tosha ya kupingana na kila anachosema (especially anaposema jambo zuri kama hili). Watu hujifunza kutokana na makosa. Sasa kama leo hii mzee Ben amepata maono na kuamua hatimaye ku-join kwenye haya mapambano ya kudai katiba mpya, then mpe credit.
 
Kichuguu, simtetei Mkapa na wala hanipi hamu ya kumtetea. Ila kwa hili la katiba mpya, nitasimama na watu kama Mkapa kwa muda wote kuliko manafiki kama Mwinyi.

Mwalimu alileta msukumo wa katiba Mpya wakati anaondoka madarakani baada ya kuitumia katiba kwa zaidi ya miaka 22. Hayo mabadiliko aliyoyaleta Mwalimu ndiyo kidogo yanatupa ahueni sasa na kujua kuwa watu kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawatadumu zaidi ya vipindi viwili vya utawala wao. Mwinyi hakupenda, na alinung'unika sana.

Mkapa kaona faida na hasara ya katiba iliyopo, na kwa kiasi fulani (kama kweli anasema haya kwa nia njema) yuko katika nafasi nzuri sana ya kusukuma na kuleta mabadiliko. Angependa iendelee hii Katiba iliyopo angeweza kukaa kimya kama Mwinyi, au hata kupinga mabadiliko kama Moi alivyofanya Kenya.

Mkapa aungane na wale wote wanaolilia Katiba Mpya......kwa nia njema.

Baada ya Nyerere kuona ubovu wa katiba ile katika mtazamo wake wa chama kimoja wakati huo, alifanya mabadiliko ya Katiba kabla hajaondoka madarakani. Ingekuwa ni vyema kwa Mkapa naye kufanya mabadiliko ya Katiba ile katika mtazamo wa vyama vingi kabla hajaondoka madarakani. Kwa nini hakufanya hivyo? huo ni unafiki tu. Badala yake wamekuwa wanajza viraka hapa na pale hadi kufikia kuwa na vifungu ambavyo ni vinajipinga. Kuna kifungu kinachosema kuwa mahakama ya rufaa ndiyo chombo cha mwisho kinachosimamia haki kwa raia wote bila kujali nafasi zao katika jamii, halafu kuna kifungu kinachosema Tume ikimtangaza mtu kuwa kashinda uraisi basi hakuna mahakama iunayoruhusiwa kusikiliza malalamiko dhidi ya uchaguzi wake! yaani hata Mahakama ya rufaa!!!
 
Mkapa anayo haki kama mtanzania yeyote kusema kile anachofikiri ni safi kwa nchi yake. Nampongeza angalau kwa kukubali kuona umuhimu wa katiba mpya kuliko wale ambao mpaka sasa wanatwambia hakuna umuhimu wa katiba mpya!

Kwa pamoja tanzania itapata katiba mpya. TAFAKARI!

Yes! I agree, Mkapa as a Citizen has the right to speak like any other Citizen,unfortunate Mkapa's tenure of leadrship does not support his propound iota. His libertine doesn't qualify him as a statesman the likes of Nyerere the least to say. Mkapa is one of those Africa leaders who are morally decayed hence not deserve a room to make the public statement. As of today the tax payers are coughing out hefty money to pay for his many dubious contracts.
Mkapa was in reign for ten years, the issue of new constitution came up numerous times. The best he did was to quick propose the retirement benefits for himself, allies and cronies. Where does he get the courage to speak for what he never dared to. We gonna fight for the new constitution own our own, we need him to tell us about Kiwira.
 
WATANZANIA TUSIONE AIBU KUDAI KATIBA MPYA KWA KASI ZAIDI HIVI SASA

Asante sana Mzee Mkapa kwa kuongeza sauti yako, kwa MUDA MWAFAKA KABISA, juu ya madai yetu ya Tume Huru ya Uchaguzi na Katibapya!! Nasema asante kwa kila sauti inayozungumza HAKI ZAIDI kwa wananchi wote wa taifa letu.

Kwa umakini mkubwa na subiri na bado sijajua kwa nini sautti za waheshimiwa hawa bado kusikika: Juu ya mahitaji yetu ya mabadiliko ya kweli na mchakato kuanza mara moja, je Balozi Salim Ahmed Salim yeye anasemaje? Bob Makani, Prof Sarungi, Mzee Mwinyi, Mzee George Kahama, Asha-Rose Migiro, Prof Tibaijuka, Dr Magufuli, Dr Mwakyembe, Mzee Edwin Mtei, Imman Simba, Askofu Pengo,Salim Amur, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Prof Luhanga, Fredrick Msuya, Fredrick Sumaye, John Samuel Malecela wao wanasemaje juu ya dhuluma za KATIBA ya sasa hivi na Madai yetu kuandika kipya bila viraka zaidi??? Jaja Samata yuko wapi, Augustino Ramadhani bado hatujamsikia, mbona Mzee Mkono bado kimya??

Vijana tunataka mabadiliko ya kweli sasa hivi bila kusubiri zaidi!!!
 
misukumo, migomo na maandamano ya kila kukicha ndio itakayoleta Katiba mpya.

Lakini kama mambo yenyewe ndo yanazungumziwa JF tu kisha huko mitaani watu wanachofuatilia ni kombe la Chalenge na mashindano ya Tusker Project Fame basi tutakuwa tunajidanganya tu.

CCM mtaji wao mkubwa ni umbumbumbu wa baadhi ya watanzania walio wengi.
Hivyo hata ktk swala hili hawana wasiwasi coz waliowengi ni mbumbumbu so hawaelewi hata hiyo katiba ina ganda la rangi gani.

SO Kila mmoja wetu mwenye uchungu na ajitahidi kuingia mtaani na kuamsha mbumbumbu ambao ni mtaji wa CCM.

Mfano:
Tazama maeneo ambayo Chadema wameshinda kisha matokeo yakataka kuchakachuliwa, nguvu ya wananchi ilisimama imara na kuweza kutoa shinikizo kwa tume mpk matokeo yaliyo halali yakatangazwa.
Lakini kama wananchi wa maeneo hayo wangekuwa kimyaaa kama sisi tunavyodai katiba basi hakika majimbo ya Chadema leo hii yasingefika hata 10.

u r right 100%, nikuchekeshe, sabasaba 2007 nilifika banda la wizara ya sheria nikaomba katiba, ilikuwa JK Nyerere temeke grounds, watumishi wakanipa, wakasema ficha usimwoneshe mtu, hatugawi hovyo, nikachukua katiba yangu, nilishangaa kweli, yaani hata kutoa nakala to citizens ya hii katiba mzee hawataki, ni baada ya ku press hard ndio nilipewa, wakati umefika tunataka katiba mpya, ila mm nashangaa JK jamani kwanini watu wanalia mno kila jambo ww kimya hapa unaniboa sana JK, kila jambo kubwa ww kimya, hata la Dowans ww kimya, aiseeee
watu wakiandamana ndio mpaka ujue kuna shida? nachoka kabisa
 
CHADEMA Sasa Ratibuni Sauti Hizo Mbalimbali Zinazodai KATIBA Mpya ili Kuunda Chombo cha Taifa

CHADEMA anzeni kuratibu sauti mbalimbali ambazo zinaendelea kujitokeza kwa sasa na kukubaliana zaidi na madai yetu ya ya MSINGI juu ya kudai kuandikwa upya KATIBA MPYA na kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Mara baada ya kuratibu sauti hizo mbali mbali, undeni National Constitutional Assembly of Tanzania (NACAT). Kazi ya kwanza ya hiki chombo cha NACAT ni kwamba watoe RATIBA KAMILIFU inayoonyesha mambo gani yatafanyika lini, na kitengo gani chini yake ili kazi ya kuandika upya (1) KATIBA, (2) kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na pia (3) kutunga sheria mbalimbali walau miaka miwili kabla ya 2015, tayari kwa uchaguzi mkuu wa wakati huo.
 
Ni kweli hamasa ya CHADEMA kwa Wananchi kudai (1) Katiba Mpya na (2) Tume Huru ya Uchaguzi umeshika kasi ajabu miongoni mwetu wananchi. Wengi zaidi sasa hujitokeza hadharani, bila woga wala kificho kudai kilicho chao.

Lakini sasa kadri sauti hizo zinavyoendelea kuongezeka, ni vema CHADEMA kuendelea kuziratibu kwa kasi hiyo hiyo ili tusije tukawacheleweshia wananchi MABADILIKO YA KWELI wanayoihitaji hivi sasa.

Kwa mantiki hiyo, CHADEMA anzeni kuratibu sauti mbalimbali ambazo zinaendelea kujitokeza kwa sasa na kukubaliana zaidi na madai yetu ya ya MSINGI juu ya kudai kuandikwa upya KATIBA MPYA na kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi.

Mara baada ya kuratibu sauti hizo mbali mbali, undeni National Constitutional Assembly of Tanzania (NACAT). Kazi ya kwanza ya hiki chombo cha NACAT ni kwamba watoe RATIBA KAMILIFU inayoonyesha mambo gani yatafanyika lini, na kitengo gani chini yake ili kazi ya kuandika upya (1) KATIBA, (2) kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na pia (3) kutunga sheria mbalimbali walau miaka miwili kabla ya 2015, tayari kwa uchaguzi mkuu wa wakati huo.
 
Nadhani katika mambo yanayotuangusha hapa nchini ni pamoja na ku-personalize mambo ya msingi. Unapozungumzia katiba you are talking about the whole nation. Wajibu wa vyama vya siasa sio wao kuandaa au kuratibu uundaji wa katiba mpya bali kudai combo cha kuratibu na kusimamia uundaji wa katiba mpya. Unapozungumzia CDM au CCM how many are there among the total population of Tanzanians?. Ukitaka kujua their number is not very significant just check how many people turned out to vote for their parties?. And remember not all voters were from specific party some were only exercising their right to vote nothing more.
 
mkapa ni mnafiki mkubwa baada ya kustaafu ndio anakumbuka kuwa hii katiba yetu ni bomu! Alipokuwa madarakani aliona akae kimya ili kula kuku na nyama za kuchoma bila bugdha yoyote sio?

Apotelee mbali huyu mchawi aliesababisha nchi yetu kuwa na wakimbizi ktk nchi za nje baada ya kufanya mauaji ya halaiki huko zanzibar na iko siku itafika huyu mzee atafikishwa ktk mahakama ya kimataifa kwa mauaji ya raia zake ili yeye na chama chake wabaki madarakani!

Mkuu huyu jamaa tuombe tu siku moja akubali watu watoe maoni yao mbele yake ndio atajaua hasira zetu. Aliichukua nchi kwenye hali mbali akabadilisha na kuifanya iwe decent kidogo, then katika siku za mwisho akaanza kuivuruga na kuitupa kabisa jalalani. The mess that we are in is mainly because of him, he knew waht was Tanzania going to face before he left the office and he kept quite and even blessed it.

Even worse alijua kabisa kuwa katiaba yetu famba halafu akaiacha famba bila hata kufanya effort ya kuibadilisha, then leo anasema hivyo, so pathetic.
 
Mkapa ataka Katiba mpya
• Asema ndiyo njia ya kuondoa mifarakano

na Datus Boniface

amka2.gif
RAIS mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, amevunja ukimya baada ya kusema ili kuzuia mifarakano ya kisiasa kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki, zinahitaji kuwa na Katiba mpya, ikiwemo Tanzania. Mkapa alisema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wanasheria wa jumuiya uliofanyika mjini Bujumbura nchini Burundi, mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Mkapa, iliyosomwa kwa niaba yake na Balozi Liberata Mulamula, njia pekee ya kuondokana na migogoro ya kisiasa kila nchi inapaswa kuwa na Katiba mpya ambayo itaainisha mambo yote ya msingi.
Alisema kama nchi wanachama zikiwa na Katiba mpya mambo mengi yanaweza kufanikiwa, lakini yameshindikana kutokana na nchi hizo kuendelea kutumia Katiba zilizorithi kutoka kwa wakoloni.
Alisema kumekuwa na malalamiko mengi kutokana na chaguzi nyingi toka kwa wanachama jinsi zinavyoendeshwa, huku shutuma na lawama nyingi zikielekezwa kwenye Katiba zilizopo.
Alisema Katiba zilizopo zimekuwa zikipendelea zaidi upande mmoja ambao unampa uhuru rais kuamua kila kitu.
Alisema uundwaji wa Katiba, lazima uendane na hali halisi, mahitaji ya kijiografia, kijamii na kisiasa.
“Tunakabiliwa na mtihani mkubwa wa kuunganisha umoja wetu wa kitaifa… kuna baadhi wamegusia juu ya matatizo yetu ya kisiasa na baadhi yetu tunafikiri kuwa siku ya kuadhimisha uhuru ni kilele cha kujenga umoja wetu wa kitaifa… uhuru wetu wa Katiba tulizonazo ni ushahidi wa dhuluma hii.
“…hatuna Katiba zingine zaidi ya zile ambazo tumezirithi kutoka kwa wakoloni, Katiba ambazo hazina umakini, tunahitaji mpya,” alisema.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ambayo Tanzania Daima imefanikiwa kupata nakala yake, Rais Mkapa alisema chaguzi nyingi zitakuwa huru na haki endapo kutakuwa na Katiba bora.
Akinukuu maneno ya mwandishi wa vitabu duniani (hakumtaja), ambaye pia ni mwanafalsafa aliyesema, ‘Chaguzi za Haki ni muhimu kwa Katiba bora.’
Alisema katika uundaji wa Katiba mpya, ni lazima kuwepo makubaliano maalum, kwa pande zote za kisiasa, kijamii na kijiografia, huku kanuni pamoja na mambo muhimu yakizingatiwa.
Alisema malumbano na migororo ndani ya nchi, yanasababishwa na muundo wa Katiba zinazoonekana kutokidhi haki na usawa.
“Katiba ndiyo moyo wa nchi, moyo wa mwanadamu unaofanya mwili mzima ufanye kazi… hivyo kwa kuangalia mbele tunahitaji kuundwa kwa Katiba na mihimili yote ya nchi, tunahitaji Katiba huru itakayotulinda katika hatari,” alisema Mkapa.
Akitoa mfano, Rais Mkapa alisema kumekuwa na sakata la uanzishaji wa Mahakama ya Kadhi katika nchi za Tanzania na Kenya, huku akisistiza kama lingekuwa ndani ya Katiba isingesababisha malumbano makubwa.
Kauli ya Rais Mkapa, imekuja wakati watu wa kada mbalimbali wakiwemo, wanasiasa, wasomi na wanaharakati wakiishinikiza serikali kufanya marekebisho ya Katiba iliyopo, kwa madai kuwa haikidhi matakwa.
Mwanzoni mwa wiki hii, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Celina Kombani, alisema hakuna haja ya kuwa na Katiba mpya, kitendo kilichoonekana kupingwa na watu wengi.
Waziri Kombani alisema Katiba iliyopo itaendelea kutumika kwani, serikali haina fedha za kufanya maandalizi ya kubadilisha Katiba hiyo.
Jaji Mkuu mstaafu Mark Bomani naye juzi alivunja ukimya na kusema kinachoisumbua serikali iliyoko madarakani ni woga ambao hauna msingi wowote.
Alisema Katiba iliyopo kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati, kwani wakati huu inakinzana katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora.
Naye Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati maarufu, Issa Shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe Katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.
 
Sauti ya mwanzo imetoka CDM kama chama kinachopigania mabadiliko hayo, kimewaamsha watu. Lazima sauti iongezwe upazwaji wake ili kufikia malengo. Siku zote CDM wamekuwa wakiongelea mambo ya kitaifa kama vile CCM imekuwa iki
yapinga. Hii hoja iko pake na isipotoshwe hata CCM ikikubali leo ila founders wa uombaji wa katiba mpya kwa kasi na kufanikiwa CDM itaandikwa ktk historia maana vingine vimeongoza upinzani miaka na miaka ila hawajaweza kushawishi jamii kama ilivyo sasa. Chadema piganieni haki zetu bila kuchoka ndio wajibu wenu
 
Mkapa ataka Katiba mpya
• Asema ndiyo njia ya kuondoa mifarakano

na Datus Boniface

Naye Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mwanaharakati maarufu, Issa Shivji, amekuwa mstari wa mbele kupiga kelele mara kwa mara kutaka serikali ibadilishe Katiba iliyopo kwa manufaa ya taifa.
Mwaka 1998 Kamati ya White Paper iliyoundwa chini ya Jaji Robert Kisanga ilipendekeza umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, lakini ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa kwa kile kilichodaiwa ilivuka mipaka kwa sababu ilikuwa kamati na si tume. Na hiyo ilikuwa awamu ya Rais Mkapa.

Hapo ndipo viongozi wetu wanaponichefua. Wakati wake Mkapa nakumbuka sana alivyomkaanga Jaji Kisanga kwa ushauri wake wa katiba mpya. Kwa kuwa naye alikuwa mwoga akiogopa makucha ya katiba mpya na sasa hataguswa maguvu yake anasingizia kipofu kaona mwezi. Wizi mtupu. Kumbe sasa naye kakubali kuwa na wivu wa kijinga na ufinyu wa kufikiri kama alivyokuwa anaelekeza tuhuma hizo kwa kila mtanzania aliyetofautiana naye kwa kutaka mambo mapya akidaiwa ni mvivu wa kufikiri??? Anazeeka vibaya.
 
Mhhh kama kweli BWM anaamini katika hayo aliyoyasema huko Burundi, basi twamuomba aje ayatamke hayo hapa Tanzania. Kwa wadhifa wake anaweza ishawishi kamati kuu ya CCM isogope na pia kama raia mwema anaweza itisha press conference akatoa mawazo yake tukayasikia.. Isijeikawa akiwa nje ya TZ anaongea tofauti na akiwa ndani ya TZ.
 
THUBUTUUU....... Kwa Ruhusa ya nani??? JK??? Hakubali Ng'o?????? Atamuuliza mbona yeye Hakuitaka kipindi chake?????
 
Weekend nilisoma gazeti moja likiwa na picha ya Shivji akitoa mada kuhusu mabadiliko ya katiba nilifarijika sana kwa vile aliweza kuaininsha sehemu za katiba ambazo zina utata wa kisheria. Baadae nikasikia tena kwamba hata Mkapa anataka matiba mpya.
Mjadala huu niliukuta kwenye club moja ya jioni ambapo jamaa kama wanne hivi walikuwa wanajadili issue ya katiba. ... Tunataka katiba mya bwana. Mimi nikaingilia kwa maswali yafuatayo.
1. Je ni katiba yote au ni sehemu fulani fulani ndani ya katiba??
2. Je, ni wananchi wangapi wameshaiona na kuimiliki katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania?
3. Je, ni wananchi wangapi wanajua inapouzwa na je maduka yanayouza katiba yapo hata kule kwetu Katavi na hata huku kwangu Kibaha mkoa wa pwani?

Jamaa aliyekuwa anadai tunataka katiba mpya aliniangalia mara kadhaa na kubaki mdomo wazi. hajui katiba inamapungufu gani; hajawahi kuisoma (licha ya kuielewa); Hata kama ana haja ya kuinunua, hajui inauzwa na nani na wapi.
 
Mhhh kama kweli BWM anaamini katika hayo aliyoyasema huko Burundi, basi twamuomba aje ayatamke hayo hapa Tanzania. Kwa wadhifa wake anaweza ishawishi kamati kuu ya CCM isogope na pia kama raia mwema anaweza itisha press conference akatoa mawazo yake tukayasikia.. Isijeikawa akiwa nje ya TZ anaongea tofauti na akiwa ndani ya TZ.

Kila jambo lina mwanzo, hekima na busara zinaweza kuanzia nje ya nchi na kisha zikatiririka ndani ya nchi. ama kuanzia moyoni zikatiririka hadi kichwani kwa binadamu ni jambo la kawaida kwa wazo jema kuanzia mahala fulani na kusambaa kwa jamii nzima. Hakuna kati yetu ajuae kwamba maneno hayo hajaongea ndani ya vikao vya CCM kutokana na mahitaji ya wakati. Shinikizo la sasa kuhusiana na madai katiba yamkini yataweza kuzungumzwa ndani ya CCM
 
Back
Top Bottom