Zakumi,
Mkuu wangu binafsi sikuiona hii toka zamani unajua tena sisi wengine tuko hooked up na Siasa..Mimi nadhani kuna maneno ya Nyerere aloyasema kuhusu Azimio la Arusha na muhimu sana sisi kujitambua na kuyatazama haya. Na kabla sijayagusia ningependa kujua tu ktk hali hii tutaweza vipi kuurudisha UZALENDO. hali ya kwamba kila Mtanzania atajivunia Utanzania wake na kuwa sehemu ya taifa hili ktk raha na taabu. Ni lazima kwanza tumalize swala la MUUNGANO kabla ya Katiba uwe vipi hivyo kura za maoni lazima zipigwe kwa sehemu zote mbili..Wazanzibar wanataka muugano gani na wabara wanataka muungano gani kisha kamati itaundwa kupata muafaka mpya iwe serikali tatu, moja au hivi hivi tulivyo..
Mambo nayotaka kuzungumzia ni sehemu mbili:- Kwanza ni vita yetu ktk kuondoa UMJASKINI,UJINGA na MARADHI maana haya maswala ndio sisi Watanzania, tusiyaonee aibu maana ndivyo tulivyo, hivyo katiba lazima itazame watu hawa kuunda DIRA ya Taifa. Katiba mpya itatokana na kipimo cha kufufua taifa linaloangamia..
Halafu Azimio linasema tena -Ili Tuendelee tunahitaji vitu vinne -1. ARDHI, 2.WATU, 3. SIASA SAFI na 4. UONGOZI BORA..
Katika haya ni lazima katiba ilinde mipaka ya Ardhi yetu kwa kuweka sheria zinazotambua sovereignty na nchi yetu kwa rasilimali na maliasili zake kuwa sehemu ya Utajiri wetu.
2. Watu wake ni kama hivyo tuwaondoe ktk Umaskini, Ujinga na Maradhi.
3. Siasa safi ni lazima vyama vya siasa viwe na itikadi infact kama ingewezekana tungeunda vyama viwili au vitatu tu halafu tukatoa mwanya kwa viongozi na wanachama wengine kujiunga na vyama hivyo kutokana na kile wanachoamini..
4. Uongozi bora hapa ndipo napopapenda zaidi maana kutokana na hali halisi ningeshauri tuwe na Rais ambaye ana mamlaka machache tu na pengine kuwa mtu wa mwisho kuchaguliwa ktk uchaguzi mkuu huyu atachaguliwa kama anavyochaguliwa Speaker bungeni kwa kura za imani - if possible.
Rais hatakuwa na role ktk kuongoza serikali, mahakama wala Bunge isipokuwa atakuwa na mamlaka juu ya vyombo hivyo. Kama Head of the state na Commanding in Chief, kuiwakilisha nchi yetu nje ya Nchi yetu ndani na nje ktk sherehe na maadhimisho yasokuwa ya kiserikali. Atakuwa rais wa Bara na visiwani na hana mshirika wala vice President..
Kisha tutakuwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ambaye atapigiwa kura kama tunavyomchagua rais sasa hivi. Huyu atashika madaraka yote ya rais yaliyobakia na yale ya waziri mkuu isipokuwa Bungeni na mahakamani. Hatakuwa na kinga isipokuwa kwa amri ya rais na anaweza kuondolewa madarakani kwa kuitisha uchaguzi mpya miaka miwili baada ya uchaguzi kama itathibitika kufanya kinyume cha miiko na maadili. Vile vile tutakuwa na mawaziri wakuu wa Zanzibar na Bara badala ya rasi wa Zanzibar, makamu wa rais, waziri kiongozi na kadhalika.
Kama tutaafiki kuwa na serikali tatu tutakuwa na mabunge matatu, La bara, visiwani, na la Muungano. Mdaraka mikoani yarudishwe kila mkoa utachagua RC na DC wake, wabunge wataendelea kuchaguliwa na Halmashuri za miji zitapewa mamlaka kamili ya kukusanya kodi na kuweka mipango miji na kupewa mamlaka ya kuendesha nyuma zote za seriklali iwe msajili wa majumba au NHC ili zikodishwe kulingana na market rate na sio kuuzwa..
kwa leo nadhani nimeandika mengi sana inatosha...