Picha kutoka shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania.
Mungu hajakosea kumfanya kila mmoja wetu jinsi alivyo,japo kati yetu kuna walemavu ambao huwa na matatizo au upungufu wa kimwili ,kiakili au kihisia ambao huwafanya kushindwa kufanya baadhi ya shughuli kwa njia ya kawaida kama wale wasio walemavu , ulemavu waweza kuzaliwa nao au kuupata maishani , kutokana na maumbile ,ajali au matatizo ya kiafya, huku ukiweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia , kabila au dini yake, na mifano ya ulemavu ni ule wa ngozi ,viwete na vipofu, na waweza kuwa wa muda au wa kudumu na tukumbuke sio kila ulemavu unaonekana kwa macho.
Takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inaonyesha watanzania milioni 5.4 sawa na asilimia 9.3% wana ulemavu wa aina fulani ,wengi wao ni tegemezi hasa kiuchumi,wakiishi kwa kutegemea misaada na kuomba omba mitaani ,imani hasi ya jamii imepelekea walemavu wawe wakibaguliwa na kuuliwa kutokana na imani za kishirikina ,huku wengi wao wakikosa elimu na fursa za ajira mambo ambayo upelekea umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi kitaifa na kukosa maamuzi juu ya maisha yao ,ambapo juhudi za makusudi hazina budi kuchukuliwa ili miaka kumi ijayo waweze kuwa wamepata maendeleo na uchumi imara.
Serikali na mashirika mbalimbali wanalitambua kwa ukaribu kundi hili , na juhudi zimekuwepo kulisaidia kama vile uwepo wa sera ya walemavu ya mwaka 2004 na sheria ya walemavu ya mwaka 2010, elimu jumuishi kwa watu wenye ulemavu ,kuanzishwa na kuvisaidia vyama na shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu,kutoa elimu ya ulemavu ili kukuza uelewa wa jamii,uwepo wa tuzo mbalimbali kwa walemavu waliofanya makubwa katika jamii kama vile Tanzania child award na huku baadhi ya walemavu wakiwa mfano wa kuigwa kama mwanadada Akwilina Akwiline ,lakini pamoj na hayo yote hayajaweza kumaliza changamoto zilizopo.
Hatua za kuchukua:
- Kukusanya takwimu za walemavu;taarifa za kina hazina budi kuchukuliwa kwa usahihi na hii yawezwa fanywa na serikali au mashirika binafsi kote nchini kwa kuingia kwenye jamii na kuhoji changamoto na yote yahusiyo walemavu na hapo ndipo tutajua chanzo na njia za kutatua changamoto zao.
- Kupatikana kwa sera na sheria mpya; sera inayoendana na wakati huu inaitajika haraka kwani ile ya mwaka 2004 imekuwa na mapungufu mengi ikiwemo suala la ruzuku kwa vyama vya watu wenye ulemavu na udogo wa mfuko wa uwezeshwaji walemavu uku idadi ya walemavu ikizidi kuwa kubwa.
-
Kukuza bajeti na rasilimali;fedha inayotengwa kupitia bajeti kwa ajili ya mambo yanayohusu walemavu inabidi kuongezeka mara dufu na hapo ndipo programu na huduma za watu wenye ulemavu zitawezekana.
- Uwezeshwaji kimtaji na elimu ya ujasiriamali;ni wajibu wa serikali na wadau wa maendeleo kuandaa mfumo utakaoweza kuwafikia walemavu wengi kupata mitaji na elimu ya ujasiriamali kama vile mikopo ya riba nafuu na jinsi ya kuitumia.
- Kupanua na kukuza njia za kuelimisha jamii; jamii bado kwa maeneo mengi hasa vijijini inakosa uelewa wa kutosha kuhusu walemavu na hapo ndipo kupitia mitahara ya elimu ,vyombo vya habari ,majukwaa na matamasha mbalimbali hasa ya kimichezo na burudani kukuza uelewa wa jamii.
-Ubunifu,ukuzaji na usambazaji wa teknolojia ;teknolojia mbalimbali za kusaidia walemavu zinabidi kuzidi kubuniwa na kusambazwa kama vile skana inayobadilisha maandishi kuwa sauti kwa walemavu wa kuona , vifaa vya kusaidia kusikia ,programu za usaidizi wa kumbukumbu na ufahamu mfano evernote na my lifeorganized ambavyo ni muhimu huku wabunifu wa ndani wazidi kupewa usaidizi kwani watatuletea kitu kinachoendana na mazingira yetu.
- Kukuza ushirikiano; ushirikiano na mashirika mbalimbali na mataifa yaliyoendelea hasa yale yanayohusika moja kwa moja na watu wenye ulemavu kama WHO ili kukuza uzoefu na maarifa katika masuala yanayohusu walemavu.
- Adhabu kali kutekelezwa;pamoja na uwepo wa sheria lakin utekelezaji wake umekuwa na kigugumizi hasa pale kunapotokea mauaji ya walemavu ambapo adhabu kali zinabidi kuchukuliwa haraka ili kutoa ujumbe kwa wengine wenye nia mbaya za namna hiyo na haki kwa waliotendewa sivyo.
Matokeo yake
- Mabadiliko ya mitazamo ya jamii; kupitia elimu na uhamasishaji huku sheria na adhabu kali zikichukuliwa tutaweza kupunguza mitazamo hasi ya wanajamii kuhusu watu wenye ulemavu itasaidia kujenga jamii inayowakubali na kuwasaisia watu wenye ulemavu.
- Kupungua migogoro kwenye jamii;kuna uwepo wa migogoro mingi kwenye jamii ikiwemo ya mauaji ,unyanyasaji na imani potofu ambayo yote itaweza kuondoka na kujenga jamii bora.
- Uzalishaji utaongezeka ; kwa kupunguza kundi la wategemezi ambao nao watashiriki kuzalisha mali na kutoa huduma tofauti katika jamii.
- Umasikini utapungua na uchumi kukua;kuanzia ngazi ya mtu binafsi, kifamilia kwenda mpaka ngazi ya kitaifa tutaweza kupungiza umasikini na
Kukuza uchumi wa nchi yetu kama watanzania kwa pamoja.
- Mchangamano;ambapo walemavu watashiriki ipasavyo na wanajamii wengine katika shughuli za kiuchumi,kisiasa na kijamii
- Utengamao;watu wenye ulemavu watapata utulivu wa maisha katika jamii kutokana na kutimizika kwa mahitaji yao muhimu.
Kwa ujumla utekelezaji wa hatua hizi utaleta maendeleo makubwa katika kuborsha hali ya watu wenye ulemavu nchini na kusaidia kujenga jamii yenye usawa na ustawi kwa wote ambalo ndilo lengo letu.
Upvote
4