Best home tutor
Senior Member
- May 8, 2026
- 194
- 268
Lucas na Tlatlah kuna ujumbe wenu huku,njooni mseme neno.Habari ya hasubuhi
Ili Tanzania ipate maendeleo ya kweli kuna mambo yanatakiwa yafanyike.Mfano kipindi cha miaka tu tumekopa zaidi ya Trioni 54 lakini ukiangalia miradi ya utekelezaji unaona kama hazishabihani.Ushauri wangu ili tupate maendeleo ni ufuatao
1.Viongozi tunaowachagua tusichague kwa mlengo wa kisiasa wawe wamesoma kweli atleast Masters degree 2 sio za heshima .
2.Life style audit kiongozi lazima kabla hajateuliwa afuatiliwe mali zake na familia na ajaze fomu na afanyiwe analysis. Haiwezekani ndani ya miaka 5 mtu waziri anamiliki magari ya dola za kimarekani billioni 3 na wakati anaingia alikua ana spacio.
3.Muhimu sana viongozi wapewe action plan yenye time frame kwamba wewe kwenye uongozi utafanya hiki na hiki na hiki kwa miaka hii 3 au 5 na tutataka matokeo baada ya miezi 3 au 6 na yasipoonekana ujiuzuru
4.Tupunguze mamlaka ya Raisi ,amepewa mamlaka makubwa sana akija mtu ambaye ni mzilankende anaweza kuyatumia vibaya na ikatuletea shida.
5.Baada ya uchaguzi tuite vyama vya upinzani tuunde serikali moja kwa kushirikiana na vyama vyote ili tuweze kusaidiana kuongoza Taifa.
Kwa machache hayo tunaweza kupata maendeleo ya kweli.