Maendeleo ya kisasa ya China yatoa mfano mzuri kwa maendeleo ya Afrika

Maendeleo ya kisasa ya China yatoa mfano mzuri kwa maendeleo ya Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,310
Reaction score
1,265
1743670641354.png


China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na pia ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi ikiifuata Marekani. Maendeleo ya China yamekuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingi zinazoendelea duniani, zikiwemo za Afrika. Mfumo wa kisiasa wa nchini China pia unachukua nafasi kubwa katika mchakato wa maendeleo ya kisasa wa nchi hiyo, na kufanikiwa kuwaondoa watu wake kwenye umasikini uliokithiri, miaka 10 kabla ya muda uliopangwa katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030.

Momar Diongue, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Habari la Senegal anasema, Afrika inaweza kupata mifano mizuri ya maendeleo kutokana na usasa wa China, na inahitaji kujifunza kutoka uamuzi wa kimkakati wa China. Kupitia maamuzi ya kimkakati na nia thabiti, China imepiga hatua kubwa katika kuwa nchi kubwa inayoendelea ya kisasa duniani.

Bw. Diongue anasema, Mikutano Miwili Mikuu ya China iliyomalizika hivi karibuni, imeionyesha dunia jinsi nchi hii inayoendelea yenye watu bilioni 1.4 inavyoweza kutumiza maendeleo endelevu kupitia mipango ya kisayansi.

Bw. Diongue, ambaye alifuatilia kwa karibu Mikutano hiyo Miwili Mikuu ya China, anasema alivutiwa sana na mkakati wa ufuaji wa maeneo ya vijijini, uvumbuzi wa kiteknolojia, nguvu mpya za ubora za uzalishaji na masuala kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Barani Afrika, watu zaidi ya asilimia 40 wanaishi chini ya mstari wa umasikini, na njia ya kukabiliana na tatizo hili ni kufanyia mageuzi hazina ya rasilimali zilizopo na kuzifanya kuwa chachu ya maendeleo. China imefanikiwa kukabiliana na hali hii kwa kuendeleza miundombinu mikuu ya msingi, kuunga mkono viwanda, na uwezeshaji wa kiteknolojia, mambo ambayo ni mfano mzuri kwa nchi za Afrika.

Jambo linginge linaoathiri maendeleo ya nchi za Afrika ni mabadiliko ya tabianchi, ambapo majanga ya kimaumbile na yale yanayosababishwa na binadamu yamekuwa kikwazo kikubwa katika kuleta maendeleo. Maendeleo ya kijani ni moja ya suluhisho la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na China imepiga hatua kubwa katika uchumi na maendeleo ya kijani, jambo ambalo linapaswa kuigwa na nchi za Afrika.

Bw. Diongue anasema, uzoefu wa China katika uchumi wa kijani una thamani kubwa kwa nchi za Afrika, na ushirikiano kati ya China na Afrika unaweza kuchukua nafasi kubwa zaidi katika maeneo kama ulinzi wa mazingira na maendeleo endelevu. Anasema ingawa Afrika ina hazina kubwa ya rasilimali za nishati ya jua, lakini inakabiliwa na changamoto kubwa katika kuendeleza sekta hiyo. Mkurugenzi huyo anasema, utaalamu wa China katika maeneo ya photovoltaics, uhifadhi wa nishati na mikongo ya umeme ya kisasa vinaweza kuzisaidia nchi za Afrika kubadili fursa zake za asili kuwa ukuaji wa uchumi huku ikichangia usimamizi wa mabadiliko ya tabianchi duniani.

China siku zote inaichukulia Afrika kama mwenzi muhimu, na hivyo nchi za Afrika zimefaidika na teknolojia za China, na mnyororo wa kiviwanda wa nchi hiyo ambao unasaidia kuongeza fursa za rasilimali na soko la Afrika, na hivyo kuimarisha zaidi ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo mageuzi ya kilimo, mafunzo ya ufundistadi kupitia Karakana za Luban, na afya ya umma.
 
Back
Top Bottom