SoC01 Maendeleo ya nchi huitaji uwepo wa watu wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika jamii

SoC01 Maendeleo ya nchi huitaji uwepo wa watu wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika jamii

Stories of Change - 2021 Competition

Sydy

New Member
Joined
Sep 14, 2021
Posts
1
Reaction score
2
ELIMU NA MAENDELEO

Maendeleo ya nchi huitaji uwepo wa watu wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika jamii. Rasilimali watu inahusisha uwepo wa watu wenye ELIMU bora, afya bora na mitazamo chanya katika jamii husika.

Serikali ya nchi inajukumu Sana katika kuwajenga watu wake katika nchi katika nyanja zote za maisha yani kielimu, kiafya, kiuchumi na kisiasa. Serikali ikizembea au kushindwa kuwatengeneza watu wake Basi nchi huyo unaweza kwenda kombo kwani serikali ndio mdau Mkubwa wa maendeleo katika nchi.

MFUMO WA ELIMU TANZANIA
Elimu ya Tanzania imeegemea Sana katika mfumo ya kielimu za kikoloni barani afrika, kwani hata mitaala yake haijabadilishwa bali hufanyiwa marekebisho madogomadogo tu, mimi naona Hali ndio ipo hivyo. Waandishi na wadau wengi wa elimu wanalia kila machweo kuomba mitaala ya kielimu ibadilishwe lakini serikali umekua na kugugumizi kufanya ivyo bado najiuliza kwanini inakua ivi lakini nahisi ni uoga wa viongozi wetu wa kufanya jambo jipya.

Serikali inajukumu la kuwaelimisha watu wake kwa kiwango bora cha elimu ili wawe na athari chanya katika jamii. Serikali inatakiwa kuweka mazingira wezeshi. Mitaala ya elimu katika lazima lazima iendane na mazingira ya jamii husika. Elimu inajukumu mtu kuwatengeneza watu wake ili wajitegemee wenyewe kwa kutumia elimu kwa kutatua matatizo na kuboresha Maisha yao. Elimu haikupatii pesa bali tumia elimu kutengeneza pesa.

Nchi nyingi za kiafrika elimu hazina nafasi kubwa kusaidia watu wake, bali bado zipo kusafisha ubongo na kuwakweza watu weupe elimu ipo kikoloni zaidi, hatusomi zaidi mazingira yetu vile ipasavyo ivyo hupelekea kuzalisha wasomi ambao ni mizigo katika jamii. Elimu zetu huwatengeneza Sana wanasiasa wabongo waongo kuliko kutengeneza wataalamu wa maendeleo katika jamii

Lego kuu la elimu ya Tanzania tangu uhuru ilikua ni kuondoka ujinga na kuhakikisha kila mtanzania anajua kusoma na kuandika. Hivyo hata sasà elimu ya Tanzania bado inalenga lengo lilelile la kuondoa ujinga katika jamii zetu licha ya mabadiliko mengi ya dunia na tiknologia duniani na kupelekea watu kushindwa kuendana na mabadiliko ya dunia kwa sasà kwani kusoma na kuandika pekee hakumsaidii mtu kufanikiwa kimaisha katika jamii. Elimu yetu bado ipo kwenye msingi ivyo serikali hainabudi kuendeleza hatua zinazofata katika elimu ili kukamilisha ujenzi wa elimu bora.

NINI KIFANYIKE KWA ELIMU YA TANZANIA
Mifumo ya elimu lazima ibadilishwe, wat wafundishwe vitu ambavyo vipo katika mazingira yao ambapo wataweza kuvifanyia kazi katika kutatua matatizo yao katika jamii bila kutegemea msaada kutoka serikalini. Wanafunzi wafundishwe jinsi gani wanatumia ujuzi kutatua matatizo na kufanya uzalishaji na si kuwafundisha kufaulu mitahani Kama ifanyikavyo mashuleni kwa sasa.

Kwa mfano watu wafundishwe jinsi gani unatumia vifaa vya kisasa katika Kilimo, jinsi gani u atengeneza ivyo vifaa, mbinu mbalimbali za ujasiliamali, ufundi wa nguo, ufundi wa vifaa vya viwandani, kufanya ugunduzi wa vitu vya kiteknolojia mbalimbali hivi ni vitu ambavyo watu watake au wasitake lazima wavikute mtaani apo elimu itakua inasaidia watu.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom