Achman kilangi
New Member
- Aug 23, 2019
- 2
- 2
Ndoa Kama Ilivyo tafsiri yake kuwa muungano wa watu wawili mwanamke na mwanaume waliokubaliana kuishi pamoja wakishirikishana Kila kitu katika nyanja zote Kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.
Ili Kufikia hatua hii ya ndoa lazima watu huanzia Kwenye Mahusiano hivyo ni muhimu tukagusa Kuanzia hatua hii mpaka Kufikia ndoa.
Tunalazimika kuitazama ndoa Kwa upana sababu ni huko ndiko mwanzo wa maisha ya Binadamu unakoanzia hivyo ukuaji wake na aina ya Binadamu huyu lazima ichangiwe na aina ya familia aliyotokea.
Dunia imefanikiwa kusonga Mbele katika upande wa teknolojia Kwani mfumo wa maisha umebadilika Kwa Kiasi Kikubwa kutoka kuishi kianalogia na kubadilika kuwa digitali. Hivyo Mambo Mengi Yamebadilishwa Ikiwemo Ndoa.
Maendeleo ya teknolojia yameziathiri ndoa Kwa namna Mbalimbali kama ilivyoelezwa hapa chini;
1)Mahusiano yanatengenezwa na kuendeshwa Kwenye mitandao.
Asilimia kubwa ya vijana wameamua Kutumia mitandao Kutafuta wenza wao ambapo Kwa namna hii kuvutiwa na wanachokiona Kwa macho tu Pasipo kuelewa undani na uhalisia wa watu hao tofauti na ilivyokua ambapo mtu aliamua Kuanza safari ya Mahusiano na mtu anayemfahamu vyema yeye na atokeapo hii ikifanikisha kujua vigezo ulivyotarajia. Hivyo Kwa Kutumia mahusiano ya mitandaoni wengi wamejikuta wakiangukia mikononi mwa watu wanaowajutia sana na hata kupelekea wasifurahie Ndoa zao.
2)Kuyachukua maisha ya Mahusiano/Ndoa za watu wengine yaliyopo mitandaoni Pasipo Kuyachuja na kuyaishi.
Watu wengi wamekuwa wakivutiwa na maisha ya Mahusiano au Ndoa za Wengine zilizowekwa mitandaoni na kuziingia Kwenye maisha yao Pasipo Kutambua kuwa waliowaona walikuwa na makubaliano Yao, mfumo wao na Muelekeo wao ambao haviwezi Kufanana na wao hivyo wakajikuta wakipambana na ugumu waliouleta Pasipo Kufahamu.
3)Kutanguliza hitaji la Kuwaonesha watu Jinsi unavyoendesha Mahusiano/Ndoa Yako na kusahau kuwa ndoa ni yako na mwenzako .
Hapa Hasa vijana hupenda ulimwengu Uone Jinsi wanavyoendesha Mahusiano au Ndoa zao hasa Ikiwa wanafurahia nyakati hizo Pasipo kujua yaweza kuwa si salama kwa kuwakaribisha wanaoweza kuwa waharibifu ambao wanawaonesha Kila kitu kuhusu wao.
4)Mawasiliano ya wanandoa kuwa ya kidigitali zaidi Hata yalipohitaji mazungumzo ya ana Kwa ana.
Sababu ya urahisi wa mawasiliano Kupitia vyombo vya kimawasiliano wanandoa wengi wameona hakuna haja ya Kutumia muda wao Hata pale nafasi inapowaruhusu kuketi chini Kuzungumza kama wanandoa hivyo wamekuwa wakitumia zaidi simu, jumbe na mitandao ya kijamii kuwasiliana kama tu Watu wasio na ukaribu huo pasipo Kutambua kuwa Kwa Kufanya hivyo Kuna ufa unaojengeka Kati Yao na hata unaoruhusu mambo mengine yenye kuzidi kuwaweka mbali.
5)Utunzaji wa ujauzito na unyonyeshaji.
Kwa upande wa kina mama wengi Kutokana na maendeleo haya ya kidigitali Pasipo hata kuwa na sababu za kiafya hawahitaji Kutumia muda mwingi kulea mimba ipasavyo, hawapendelei kujifungua Tena Kwa njia ya kawaida na kupendelea njia ya upasuaji na hata kunyonyesha watoto wao maziwa yasiyo yao kama wamama wakihofia baadhi ya dhana duni zinazowazunguka nao Pasipo kuelewa umbali wa kibailojia Wanaouweka Kati yao watoto wao na hata baba zao.
6)Malezi ya watoto
Wazazi wengi wamekubali kuwalea watoto wao Kwa Kufuata mifumo ya kidigitali ilihali wakiwa ndani ya mamlaka yao kuweza kuwadhibiti na kuwaelimisha. Watoto wengi wamejikuta hawafahamu kabisa aina ya asili zao hata kiutamaduni katika mambo Mbalimbali kwa kuwa wanakua wakiruhusiwa na pengine kupewa urahisi wa kufikia kila Kilicho cha kidigitali pasipo kutofautishiwa Chenye manufaa na kisichofaa kwao katika kila kitu mavazi, vifaa vya umeme, vyakula,lugha,elimu,nidhamu na hata uwajibikaji kama raia.
7)Mifumo ya Huduma za elimu.
Kwa kuwa Wazazi wamekuwa wakihitaji elimu bora kwa watoto wao Lakini wanasahau kufuatilia namna au kinachokuja na Ubora wa elimu hizo wanazowatafutia watoto wao Hasa ukizingatia ni Mifumo ya kigeni iliyobeba kila aina ya mafunzo na hata kupelekea watoto hawa kujikuta wakichukua na vingine zaidi ya elimu bora waliyokusudia. Mathalani mazingira wanayoishi huko mashuleni na wanachojifunza kati yao au kati yao na watu wengine walio katika mazingira ya huko mashuleni.
8)Upatikanaji rahisi wa mambo ya kigeni kuliko maadili na mafunzo ya Jamii zetu.
Wanandoa wengi wamejikuta wakijifunza na Kutafuta masuluhisho ya Changamoto zao katika ulimwengu wa digitali na kuacha kufikiria njia nyingine Zilizo bora ikiwemo kumshirikisha Mungu na wazee wao husika kupata mwongozo na mawazo ya namna sahihi ya kutatua matatizo Yao.
9)Mitandao kuwa Sehemu Ya kuvunja Ndoa.
Kupitia Mitandao hii watu wamejikuta wakiharibu ndoa zao sababu tu ya kuhusiana kirafiki na watu wengine wanaofahamiana nao kupitia mitandao hii ambapo wamejikuta wakitumia muda wao na watu baki kuliko kujenga ndoa zao na familia zao.
10)Urahisi wa kusaliti na kuhatarisha ndoa.
Wanandoa wengi wamejikuta wakiwa karibu na usaliti au kuwemo kabisa Kutokana na kuwa na urahisi wa kufanya maamuzi ya nini wafanye na nani wawe nao sababu tu ya urahisi wa kuingia kwenye Ulimwengu wa digitali wenye kuwaonesha kila wanachokihitaji.
Hivyo, Kama taifa lazima tuendelee ikiwemo kutokwepa matumizi ya mifumo ya digitali katika nyanza zote lakini isiwe kigezo cha wanandoa au watu walio kwenye mahusiano kuamua kukitumia au kukiishi kila kilicho kidigitali wanachokiona lazima wakumbuke wanatakiwa kuwa walimu na wakufunzi wa kizazi kipya wanachokileta ambacho ili kitokee lazima ndoa zao ziwe salama na imara.
Kama taifa tunahitaji kutengeneza kizazi kilichokabidhiwa maadili Sahihi, chenye kujua wajibu wake na kinachoheshimu na kuthamini miiko yetu, tamaduni zetu na hata Imani zetu. Kazi ambayo Hufanywa na wazazi kwanza kabla ya kuifikia jamii ambayo nayo inategemea ijifunze kutoka kwa wanandoa wanaoishi ndani yake.
Lazima tufahamu kuwa ndoa ni jambo jema kiimani hivyo kuilinda ni jukumu la wahusika ili idumu na kuleta kizazi chenye manufaa kwa maendeleo binafsi, Jamii husika na taifa kwa ujumla.
Tutumie maendeleo ya teknolojia pale tu yanayohitajika kwa umuhimu na kutoyapokea wala kuyatumia pale yasipohitajika ili tudumishe jumuiya hizi takatifu.

Upvote
1