Uchaguzi 2020 Maendeleo yanawauma CHADEMA ndio maana wanamchafua Dkt. Magufuli

Hakuna kuiba safari hii,mtashangaa
Afadhali. Wimbo uliozoeleka wa kuibiwa mwaka huu hatutausikia.

Sijawahi kushuhudia kampeni za amani kama za mwaka huu ukiondoa matukio mawili ya kijana wa UVCCM aliyeuwawa Njombe na wahuni waliolazimisha Polisi kutumia mabomu ya machozi Tarime.
 
Vijana hamjui vizuri historia ya Tanzania. Watanzania kuanzia wakati wa Nyerere wanapenda uhuru na haki kuliko maendeleo ya vitu. Magu angekuwa ametoa uhuru Lissu asingekuwa anawatesa hivi na kupendwa kiasi hiki. Watanzania hawapendi uonevu kabisa.
 
mimi sipo chama chochote ila kitendo cha wafanyabiashara wengi kusema "mzee amebana sana vitu vinapatikana kwa bei ya ghali" ni dhahiri kwamba wahujumu uchumi wa nchi wataisapoti sana CHADEMA ili waweze kufanya biashara na kupata mizigo kijanjajanja.

CHADEMA kwa wafanya biashara wasiopenda kulipa kodi inaonekana kama kimbilio.
 
Twende na Magufuli
Tunakuombea usiku na mchana
Na Mungu atazidi kukulinda siku ZOTE za maisha yako mheshimiwa Rais wetu
Wanga wamechemkaaaaa
 
Mwaka tutaelewana ..
Pimbi nyinyi

 
kama kwa kipindi cha miaka mitano amefanya mambo makubwa sana kwa nini anaomba kura kwa kupiga magoti?

Wewe unaweza kufanya mambo makubwa sana kwa wananchi kisha ukaombe tena kibali cha kuendelea kuwatumikia kwa kupiga magoti?Kwanza mtu aliewafanyia mambo makubwa sana wananchi wala hana haja ya kufanya kampeni kwa sababu hayo mambo makubwa aliyofanya yanatoshi kumnadi.

Unapofanya mambo makubwa sana wananchi wanatakiwa wakuhitaji wewe kuliko unavyowahitaji wao.Iweje leo hii Magufuli ahitaji wananchi tena kwa kupiga magoti kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye kama alifanya mambo makubwa sana kama unavyojinasibu hapa?

Kitendo cha Magufuli kuomba kura kwa kupiga magoti ni ushahidi kuwa hakuna lolote la maana alilofanya kwa kipindi cha miaka mitano na kwa hiyo amekosa kibali cha wananchi kuendelea kuwa kiongozi wao,anachofanya sasa hivi ni kupiga magoti ili kulaghai watu.

Magufuli kwa sasa hivi ni tapeli anaetaka kurudi ikulu kwa njia za hila na kwa kulaghai watu baada ya kutumia miaka mitano kufanya ujinga na kujinufaisha yeye mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…