Uchaguzi 2020 Maendeleo yanawauma CHADEMA ndio maana wanamchafua Dkt. Magufuli

Uchaguzi 2020 Maendeleo yanawauma CHADEMA ndio maana wanamchafua Dkt. Magufuli

Hakuna kuiba safari hii,mtashangaa
Afadhali. Wimbo uliozoeleka wa kuibiwa mwaka huu hatutausikia.

Sijawahi kushuhudia kampeni za amani kama za mwaka huu ukiondoa matukio mawili ya kijana wa UVCCM aliyeuwawa Njombe na wahuni waliolazimisha Polisi kutumia mabomu ya machozi Tarime.
 
Vijana hamjui vizuri historia ya Tanzania. Watanzania kuanzia wakati wa Nyerere wanapenda uhuru na haki kuliko maendeleo ya vitu. Magu angekuwa ametoa uhuru Lissu asingekuwa anawatesa hivi na kupendwa kiasi hiki. Watanzania hawapendi uonevu kabisa.
 
mimi sipo chama chochote ila kitendo cha wafanyabiashara wengi kusema "mzee amebana sana vitu vinapatikana kwa bei ya ghali" ni dhahiri kwamba wahujumu uchumi wa nchi wataisapoti sana CHADEMA ili waweze kufanya biashara na kupata mizigo kijanjajanja.

CHADEMA kwa wafanya biashara wasiopenda kulipa kodi inaonekana kama kimbilio.
 
Twende na Magufuli
Tunakuombea usiku na mchana
Na Mungu atazidi kukulinda siku ZOTE za maisha yako mheshimiwa Rais wetu
Wanga wamechemkaaaaa
 
Ukweli uwekwe wazi.

Kazi kubwa aliyoifanya Magufuli kuiongoza Serikali kufikia malengo yenye mafanikio ikiwemo la kufika Uchumi wa Kati kabla ya 2025 ni wazi amejitengenezea maadui wengi waa ndani na nje ya nchi. Hebu ongozana nami kwa ufupi kwenye maeneo muhimu

1. UGENISHAJI KATIKA RASILIMALI
Magufuli alikataa rasilimali za nchi kumilikiwa kwa sehemu kubwa na makampuni ya kigeni ambapo Serikali yake imepeleka sheria bungeni na kuibadili ili nchi iweze kunufaika na rasilimali zake.

Ukiangalia uamuzi wa kujenga ukuta kuzunguka eneo la machimbo ya Tanzanite Mererani imepelekea Tanzania kuingia kwenye orodha ya vinara wa biashara ya Tanzanite duniani ambapo awali India, Kenya na SA walikuwa wameshika soko.

Kuanzisha masoko ya madini ya ndani imesaidia kupunguza utoroshwaji wa madini yetu na kuingizwa kwenye black market.

2. MIUNDOMBINU
Rais Magufuli amesimamia nankutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja nchini, sambamba na kufungua reli kuelekea Tanga, Moshi na Arusha huku akiimarisha reli kongwe ya Kigoma kuwa ktk SGR hivyo kufanikisha upanuaji wa huduma za Bandari ya Dar es Salaam kwa nchi zilizo land locked. Miradi hii mikubwa ilibuniwa na hata awamu zilizopita lakini haikutekelezwa kutokana na kukosekana rasilimali fedha.

Ingewezekana kukopa kutoka kwa nchi wahisani lakini JPM alizingatia mzigo mkubwa wa madeni na kuamua kujiondoa kwenye unyonge wa masharti magumu hatimaye miradi hii imetekelezwa kwa fedha zitokanazo na makusanyo ya kodi.

Ujenzi na upauaji wa viwanja vya ndege mikoa mingi umeenda sambamba na kununua ndege mpya 11 ambapo pamoja na kufufua ATCL lakini unaipa nafasi sekta ya utalii kutumia fursa hii kuleta watalii wengi nchini.

Bandari zimeongezewa ubora hata ununuzi/ujenzi wa meli mpya za abiria na mizigo ni mambo yaliyofanyika ndani ya miaka 5 yake ya kwanza. Ujenzi wa ICDs Dodoma na mikoa ya jirani ni wazi connection ya SGR na Bandari utafanikisha ukuaji mkubwa wa uchumi na kuyasukuma maendeleo ya Taifa mbele zaidi

3. VITAMBULISHO VYA WAJASIRIAMALI
Hii ni haueni kubwa kwa wafanyamiashara almaarufu wamachinga kwani walionekana hawana mchango wowote kwenye jamii na walionekana ni wasumbufu. Vitambulisho hivi vimesaidia micro-business kuchangiia pato la Taifa na hata kuwajengea mazingira ya kutosumbuliwa na wamepunguza ugumu au mfumuko wa bei mitaani.

Wajasiriamali wadogo wamekiwa wakitozwa ushuru Tshs 500 kutwa ambazo haziingii serikalini na ukiangalia wanatoa zaidi ya Tsha20,00 kwa mwaka kwa ushuru huo. Hivyo tozo ya Tshs 20,000 kwa mwaka ni faraja kwa wamachinga na wenye mitaji midogo.

4. UFISADI

5. ULINZI NA USALAMA

6. KUINUA KILIMO

7. UBORESHAJI SEKTA YA AFYA

8. KUPAMBANA NA RUSHWA

9. MISHAHARA HEWA

10. MAHAKAMA YA MAFISADI

11. VYETI FEKI

12. KULIPA MALIMBIKIZO YA WAALIMU

13. KUPAMBANA NA CORONA.

14....


Nimeorodhesha na kudadavua maeneo kadhaa ya maendeleo yaliyofikiwa na serikali ya awamu ya tano, ni wazi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hawafurahii haya maendeleo.

Katika kampeni za mgombea wao wa urais amekuwa akitumia jukwaa la siasa kutukana na kubeza maendeleo hadi kufikia kusema kwamba ununuzi wa ndege ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Kuna wakati anawaambia wananchi kwamba kama Magufuli kajenga mabarabara na madaraja basi hayo yampigie kura.

Zaidi sana Chadema wamejipambanua kupitia kampeni za mwaka huu kwamba ni maadui wa maendeleo ya nchi.

Mgombea wao ameshasema kwamba, ataweka dhamana madini na rasiilimali za nchi ilikujenga miundombinu na kadhalika. Pia wamejinasibu kutaka kubadili katiba kama takwa la kwanza lakini wanajisahau kwamba sisi wananchi tunajua namna walivyobadili katiba ya CHADEMA ili kumpa uenyekiti wa maisha Mbowe. Sisi tuna akili na tunatambua hila zao wanazotuhadaa kwenye kampeni zao.

CHADEMA wanamtukana sana Magufulina kumbeza kwa sababu amesimama imara kuiletea nchi maendeleo na kukataa ghiliba za mabeberu ambao wanataka kuifanya Tanzania kuwa nchi yao ya kinyonyaji.

Mwaka tutaelewana ..
Pimbi nyinyi

 
kama kwa kipindi cha miaka mitano amefanya mambo makubwa sana kwa nini anaomba kura kwa kupiga magoti?

Wewe unaweza kufanya mambo makubwa sana kwa wananchi kisha ukaombe tena kibali cha kuendelea kuwatumikia kwa kupiga magoti?Kwanza mtu aliewafanyia mambo makubwa sana wananchi wala hana haja ya kufanya kampeni kwa sababu hayo mambo makubwa aliyofanya yanatoshi kumnadi.

Unapofanya mambo makubwa sana wananchi wanatakiwa wakuhitaji wewe kuliko unavyowahitaji wao.Iweje leo hii Magufuli ahitaji wananchi tena kwa kupiga magoti kuliko wananchi wanavyomuhitaji yeye kama alifanya mambo makubwa sana kama unavyojinasibu hapa?

Kitendo cha Magufuli kuomba kura kwa kupiga magoti ni ushahidi kuwa hakuna lolote la maana alilofanya kwa kipindi cha miaka mitano na kwa hiyo amekosa kibali cha wananchi kuendelea kuwa kiongozi wao,anachofanya sasa hivi ni kupiga magoti ili kulaghai watu.

Magufuli kwa sasa hivi ni tapeli anaetaka kurudi ikulu kwa njia za hila na kwa kulaghai watu baada ya kutumia miaka mitano kufanya ujinga na kujinufaisha yeye mwenyewe.
JamiiForums312469786.jpg
 
Back
Top Bottom