BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Mapema leo Jumamosi Agosti 28, 2021 Msemaji wa Serikali Ndugu Gerson Msigwa- amezungumza na Waandishi wa habarih katika Ofisi za Habari-Maelezo Jijini Dodoma. Haya ndiyo aliyoyazungumza Ndugu Msigwa wakati akitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Serikali. Haya ni sehemu ya maeneo aliyoyatolea ufafanuzi.
"Kauli, uamuzi na msimamo rasmi wa Serikali kuhusu suala la sintofahamu ya tozo ya miamala ya simu utatolewa Agosti 31, 2021 baada ya taratibu za ndani kukamilika baada ya ripoti ya ukusanyaji maoni kutoka kwa wananchi kupelekwa kwa Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa."
"Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 149 kwa ajili ya kuanzah kutekeleza mpango wa Bima kwa wote. Serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Bima kwa Wote katikah Kikao cha Bunge la Septemba mwaka huu na kwamba kiasi kilichotengwa ni cha awali na kitaanza kwa makundi maalumu."
"Ujenzi wa mradi wa kimkakati wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) unaendelea vizuri na ujenzi wake umefikia 57%. Serikali kupitia TANESCO inaendelea kununua vifaa mbalimbali vya ujenzi vya kukamilisha ujenzi huo.”
"Serikali tayari imefanya malipo ya awali ya ndege mpya 5, ikiwepo ndege kubwa 1 ya mizigo na zinatarajiwa kuwasili mwaka 2023."
"Kumekuwa na malalamiko ya vifurushi vimepanda lakini niwaambie sisi ni kati ya nchi 5 Afrika zenye gharama za chini za bando. Ziko baadhi ya nchi za Ulaya ambazo gharama zake ni kubwa, ninafahamu iko nchi ambayo unanunua GB 1 kwa Dola 15".
"Serikali imewekeza Bilioni 600 katika mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ili kutoa huduma na kuleta nafuu kwa watumiaji wa huduma za simu ikiwemo kupiga na data."
"Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 Barani Afrika ambazo zina gharama ndogo na nafuu katika mawasiliano. Licha ya changamoto za kupanda kwa gharama hizi, lakini bado gharama hizi ni nafuu. Kuna mfano wa nchi moja huko nje, gharama ya GB moja ni dola za kimarekani 15.”
"Serikali imetoa Shilingi bilioni 50 kuipa TTCL ili kupeleka huduma ya mawasiliano katika maeneo ambayo hayana mawasiliano hapa nchini.”
"Mapato kutokana na Bandari yameongezeka kutoka shilingi bilioni 525.4 hadi shilingi bilioni 531, bandari zetu zimeendelea kufanya vizuri licha ya changamoto za Ugonjwa wa Uviko-19 duniani.”
"Bandari yetu ya Dar es Salaam wiki tatu zilizopita imeandika rekodi kubwa kwa Bara la Afrika, ambapo kupitia gati maalumu ilifanikiwa kupokea magari 3,743, na asilimia 65 ya magari hayo (magari 2945) yalikuwa yanapelekewa nje ya nchi.”
"Hadi kufikia mwezi Machi, 2022 Bandari ya Karema itaanza kufanya kazi, hali itakayopelekea kupanua wigo wa usafirishaji mizigo kwenda nje ya nchi.”

"Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 149 kwa ajili ya kuanzan kutekeleza mpango wa Bima kwa wote. Serikali itawasilisha Muswada wa Sheria ya Huduma ya Bima kwa Wote katika Kikao cha Bunge la Septemba mwaka huu na kwamba kiasi kilichotengwa ni cha awali na kitaanza kwa makundi maalumu."
"Serikali imeshaweka oda ya vichwa 10 vya Treni ya( umeme ambavyo majaribio yake yanatarajiwa kuanza wakati wowote kati ya Dar es salaam na Morogoro,kila kichwa kimoja kitabeba mabehewa nane hivyo kutakuwa na mabehewa 80."
#KaziInaendelea