Maeneo hatari kutembelea duniani, hasa kwa watalii

vivaforever

Senior Member
Joined
May 30, 2016
Posts
113
Reaction score
165
Duniani kuna baadhi ya maeneo ukiyafikiria tuu huwa yanakutamanisha sana kiasi ukatamani siku uende kuyatembelea.. lakini kiuhalisia ni maeneo hatarishi zaidi hapa Duniani. Kiuhalisia Dunia ina maeneo mengi ambayo ni hatari kuyatembelea lakini kwenye uzi huu nitayaongelea machache tuu ambayo yamejizolea umaharufu.

Kama kuna maeneo mengineyo unayoyafahamu, usisite kuyaongezea ili tupate kujifunza.
Karibuni. [emoji4]

01. DEATH VALLEY NATIONAL PARK, USA (HIFADHI YA TAIFA YA BONDE LA KIFO, MAREKANI)

Ni sahihi kusema kuwa hili eneo ni miongoni mwa maeneo yaliyoangamia, Bonde la kifo ni moja kati ya mabonde hatari zaidi Duniani ingawa muonekano wake unatamanisha kulitembelea. Bonde hili linapatikana kati ya jimbo la Nevada na California, Bonde la kifo ni eneo la chini kabisa huko Amerika Kaskazini huku likiwa na ardhi mbaya sana.

Hili bonde limeshawahi kurekodiwa likiwa na joto la hali ya juu kabisa kuwahi kutokea hapa Duniani kiasili ambalo lilifikia hadi 134 °F (56.7 °C). Muigizaji wa filamu ya Harry Potter ajulikanaye kama Dave Legeno ni moja kati ya wahanga waliopoteza maisha yao kutokana na joto kali sana la bonde hili.

Pia bonde hili lina maajabu yake ambapo nyakati tofauti mawe mazito yanayofikia hadi paundi 700 huwa yanaonekana yakiwa yanajongea yenyewe.
Baadhi ya watu wanaripoti kuwa kuna nyakati mchanga wa bonde hilo huwa unaimba ukiusikiliza kwa ukaribu huku wakiwa wamejenga imani kuwa hilo ni eneo ambalo Shetani huwa anacheza gofu (golf).. teh teh teh... [emoji23]

02. VOLKANO TOURS, HAWAII, USA (VOLKANO ZA VISIWA VYA HAWAII, MAREKANI).

Kwa wale wapenda bata wenye pesa ndefu hapa Duniani wengi wao hupendelea kwenda vacation maeneo yenye beach nzuri, hotel za ufukweni n.k, maeneo mengi kama vile Zanzibar, Jeju Islands, Comoros n.k huwa ni vivutio vya watalii hawa... miongoni mwa maeneo ambayo huvutia zaidi Duniani ni visiwa vya Hawaii. Mbali na kuwa na maji safi, beach nzuri na hewa safi kabisa bado visiwa vya Hawaii ni eneo hatari kulitembelea hapa Duniani.

Hakuna eneo jingine lolote Duniani unaloweza shuhudia Volkano ikiwa inaripuka kwa ukaribu zaidi kama Visiwa vya Hawaii. Volkeno inayoripuka hapa ni Volkeno hai huku nyingi ikiwa inatokea kwenye mlima Kilauea ambao unaripuka mara kwa mara tangu mwaka 1983, pia Volkano hai kubwa zaidi Duniani ijulikanayo kama Mauna Loa ambayo inapanda hadi futi 13,680 juu ya usawa wa Bahari inapatikana huku.

Volkano ya Hawaii inatisha kiasi kwamba kuna wakati unaweza shuhudia maporomoko ya maji ambayo kinachoporomoka ni Volkano badala ya Maji, maji yanayochemka sana kiasi ukiingia unaiva hapohapo, mawe na miamba inayoruka kwa umbali mrefu kutokana na milipuko n.k.

03. SNAKE ISLAND, BRAZIL (KISIWA CHA NYOKA, BRAZILI).

Moja kati ya maeneo hatarishi zaidi Duniani kiasi kwamba hata Serikali ya Brazil imepiga marufuku mtu yeyote kutembelea.

Hili eneo linapatikana maili 90 kutoka jiji la Sao Paulo, hiki kisiwa ndio makazi ya idadi kubwa sana ya nyoka Duniani.. inatosha kusema kuwa hakuna eneo lenye mkusanyiko mkubwa wa Nyoka Duniani kama kisiwa hiki.

Kutokana na tafiti mbalimbali, kisiwa hiki ( pia kinajulikana kama Ilha da Queimada Grande ) kina nyoka si chini ya Watano kwa kila mita moja ya mraba. Jambo baya zaidi kuhusu nyoka wa kisiwa hiki ni kuwa wana sumu kali sana inayoweza kuifanya nyama za mwili wa Binadamu ziyeyuke.

Hiki kisiwa ndio eneo pekee ambapo nyoka wenye sumu kali sana kama Golden lancehead viper anapatikana pamoja na nyoka aina ya Bothrops.

04. SKELLIG MICHAEL MOUNTAIN, IRELAND. (MLIMA WA SKELLIG MICHAEL, IRELAND)

Mlima wenye muundo mbaya, ulio mbali kufikiwa pamoja na njia hatarishi ndani yake. Unapatikana ukanda wa Magharibi wa Ireland na ni moja kati ya mafikio ya hatari kwa watalii Duniani.

Huu mlima una ngazi zipatazo 600 ambazo zote hazipo sawa (steps zake zimepishana pia ndefu) ambazo zinaelekea kwenye Nyumba za Watawa za Kale.

Kuufikia huu mlima ni changamoto sana kwa sababu watalii wanatakiwa kupanda boti ambazo zinatumia masaa mengi hadi zipite kwenye mikondo ya maji yaliyovurugika pia mara nyingi boti hizi haziwezi hata kutia nanga kwa sababu ya mawimbi makubwa sana yanayopiga ufukweni.

Wakati utalii unaongezea kutokana na eneo hili kuhusishwa ndani ya filamu ya Star Wars The Force Awakens, bado Serikali inatoa tahadhari kutokana na kuanguka kwa mawe, hali mbaya ya hewa na sababu nyinginezo za kiusalama.

05. ZIWA NATRON, TANZANIA. (LAKE NATRON, TANZANIA)

Yeah, tupo ndani ya list au mnasemaje? [emoji23][emoji378]

Ziwa lenye kiwango kikubwa cha chumvi linalopatikana Kaskazini ya Tanzania ni moja kati ya maeneo hatari Duniani ambayo ikiwa mnyama atadumbukia, basi anagandishwa hapohapo na kuwa kama Jiwe (Calcification).

Maji ya ziwa hili ni mazito, huchemkaga sana hadi kufikia nyuzijoto 60 na kitu (>60°C), pia yanaakisi mwanga kiasi kwamba yanakuwa kama kioo.. picha ya angahewa huakisiwa na maji ya ziwa hii hivyo ndege wanaoruka hudhania wanaruka kwenye eneo lililo wazi kama mlango wa kioo, mwishowe hudumbukia ndani yake.

Kipindi wakishatua tuu ndani ya maji ya ziwa hili, miili yao huaribiwa ndani ya dakika chache tuu.

Miaka michache hapo nyuma rubani ya helicopter alipumbazwa kwa style hii hii na helicopter yake ikaingia ndani ya hilo ziwa baada ya muda mfupi ikaharibiwa na maji yenye kiwango kikubwa cha alkali ya ziwa hili.

06. JANGWA LA DANAKIL, ETHIOPIA. (DANAKIL DESERT, ETHIOPIA)

Eneo lenye joto zaidi Duniani ni hili jangwa la Danakil huko Ethiopia na ni moja kati ya eneo ambalo kavu mno na la chini zaidi Duniani, yaani kama Ardhi ya kuzimu.

Mtu anaweza shuhudia Ardhi ya Volkano ikiwa inatapika Volkano kizembe, rangi mbalimbali zinazoashiria tofauti ya joto na madonge makubwa ya chumvi.

Hili eneo limefunikwa na tani karibia laki moja za chumvi.

Hili eneo linapatikana mwishoni mwa bonde kuu la ufa. Kulifikia eneo hili inahitajika uendeshe gari kupitia barabara mbaya na yenye vumbi kutoka eneo linalojulikana kama Makele. Hili eneo lina Volkeno nyingi hai zinazovuja gesi zenye sumu.

08. UKANDA WA MAFUVU, NAMIBIA. (SKELETONS COAST, NAMIBIA)

Eneo hili lililotengwa na halikaliki linapatikana pale Ardhi inapoishia. Huu ukanda umeenea kilomita 500 kati ya mji wa zamani wa Koloni la Ujerumani (Swakopmund) na mpaka wa Angola.

Jina pekee linaonyesha jinsi gani hili eneo lilivyo si rafiki, hili jina limetokana na muonekano wa eneo husika kwani limefunikwa na mafuvu mengi ya wanyama pamoja na mabaki ya meli zilizopinduka hapo zamani.

Mimea haistawi hapa, maji masafi hakuna na mchana ni joto sana. Ardhi yake haina mimea kama nilivyosema hapo hivyo ni kame kwa muda mrefu.

09. MLIMA WASHINGTON, MAREKANI. (MOUNT WASHINGTON, U.S.A)

Mojawapo ya maeneo hatarishi huko Marekani ni hili, eneo hili lina rekodi ya kuwa na upepo unaovuma kwa speed kali zaidi hapa Duniani huku likiwa lishawahi kuwa na upepo wenye speed karibia maili 203 kwa saa.

Sio tuu kuhusu upepo lakini pia baridi linatesa, baridi lake linaweza dondoka hadi nyuz -40°C jambo linalofanya kulitembelea eneo hili iwe ni ngumu. Pia mlima huu unajulikana kama mlima hatari zaidi mdogo Duniani.

Sasa fikiria unaepuka kifo kwa kupigwa na upepo mkali kwa wakati flani ili baadae uweze kujiokoa ghafla baridi kali linakuja kukugandisha. [emoji32]

10. MILANGO YA KUZIMU, TURKIMENISTAN (GATES OF HELL, TURKIMENSTAN).

Kreta kubwa ya kutengenezwa na binadamu imekuwa ikiunguza gesi aina ya Methane kwa miongo kadhaa sasa na ni moja kati ya janga lililosababishwa na hesabu mbovu za wanasayansi ambapo wameamua kufungua mlango wa kuzimu.

Wakati gesi ilipoanza kuvuja eneo hili Wanasayansi walikuwa na shaka huenda itasababisha uchafuzi wa hewa tunayopumua, hivyo wakaamua waiwashe moto wakiamini kiwa baada ya wiki kadhaa itaungua yote na kuzima, lakini cha ajabu hadi leo hii (nusu karne sasa) bado inaungua tuu.

Eneo hili ni hatari kwani lina hewa chafu, joto pia gesi inayoungua inazidi kufanya joto lipande zaidi.

11. KISIWA CHA KASKAZINI YA SENTINEL, ANDAMANS (NORTH SENTINEL ISLAND, ANDAMANS)

Marufuku kukisogelea, hatari na kina maajabu mengi ambayo hayaelezeki. Kisiwa hiki kinakaliwa na wakazi ambao ni bora tuu kusema wao ni watu wa kale, maana hadi sasa bado hawajaendelea.

Sasa shida kubwa ya kisiwa hiki ni hawa wakazi wake, wao huwa hawaulizi wala nini, yeyote yule anayekikaribia kisiwa hiki wanamkaribisha na mvua ya mishale yenye sumu.

Baadhi ya watu waliojaribu kwenda kukitembelea kisiwa hiki au wale ambao meli zao zinapata tatizo wanajikuta wanatia nanga hapa.. hawaponi.

Zaidi ya watu 90% walikumbana na mauti hapa. Jamii ya watu wa kisiwa hiki (Sentinelese) ni wawindaji wa makundi, wamegoma aina yoyote ya muingiliano na jamii za watu wa nje na hadi sasa idadi yao halisi haijulikani. Serikali imepiga marufuku mtu yoyote kukikaribia kisiwa hiki.

12. HIFADHI YA TAIFA YA MADIDI, BOLIVIA (MADIDI NATIONAL PARK, BOLIVIA)

Ushawahi sikia msemo wa Pori Peponi ?? Basi eneo hili ni mfano mzuri wa msemo huu. Eneo hili ndo lina aina nyingi na jamii kubwa zaidi ya mimea, wadudu na baadhi ya wanyama Duniani lakini pia ndio eneo lenye mimea yenye sumu zaidi Duniani, hili eneo ni hatari sana kwa watu kulitembelea.

Kugusana tuu na aina yoyote ya mimea inayoota ndani ya hifadhi hii kunasababisha mtu apate uwasho, uvimbe mwilini pamoja na kizunguzungu. Jeraha dogo tuu au kidonda kinaweza kupata maambukizi ya vimelea vya ukanda wa kitropiki.

Yeah, sasa sijui ni upupu au la ila inasemekana kuwa kwa zaidi ya robo tatu za mimea ya pori hili inadhuru, watalii wanashauliwa kubeba viboksi vya huduma ya kwanza au waongozane na mtaalamu wa Sumu za mimea hiyo.

Ni sawa na kusema hifadhi hii ni bustani ya Sumu, ingawa Bustani ya Sumu halisi haipatikani hapo.

13. OYMYAKON, SIBERIA

Siberia, ni eneo ambalo lina historia ya kuwa na baridi la muda mrefu sana Duniani. Oymyakon ni kijiji kilichopo mashariki ya Siberia, Russia.

Kinachofanya eneo hili liwe hatari ni baridi kali la muda wote wa Mwaka pia ndio kijiji chenye baridi kali zaidi Duniani. Mwaka 1924, joto lake lilidondoka chini ya 0°C hadi kufikia -96°C rekodi ambayo hakuna eneo lolote Duniani lishawahi kuiweka.

Baridi la eneo hili linagandisha mate hadi machozi kiasi yanakuwa kama sindano ambazo zinachoma mdomoni na machoni.

Haya, nani ataweza kusihi eneo hili [emoji16][emoji3480]... msije mkasema hakuna maana kuna wakazi wapatao chini ya 500 wanaoishi hapa sema wanahama mara kwa mara.

14. ALAGOAS, BRAZILI

Fikiria unaishi kwenye eneo ambalo hujui ni lini na ni nani atakuja kukukata mapanga na kukulazimisha uiache Dunia hii., yeah.. karibu Pwani ya Alagoas ujionee kabla hujafa [emoji38].

Ni moja kati ya majiji machache muhimu sana ya Brazil ikiwemo Rio de Janeiro na Sao Paulo, ndio yanasemekana kuwa na kiwango cha juu zaidi cha uhalifu pale Brazil.

Lakini mbali na jiji hili kuwa dogo kijiografia huku pia likiwa sio maharufu sana, jiji hili ndio lenye kiwango cha juu zaidi cha mauaji pale Brazil (inawezekana pia ni kwa Dunia nzima).

Hili jiji lina wakazi wapatao karibia milioni 3 tuu lakini zaidi ya watu 2,000 huuliwa kila mwaka.

15. MONROVIA, LIBERIA

Mara nyingi niliamini kuwa Nchi hii ni moja kati ya Nchi zilizoendelea zaidi Duniani huku ikiwa na Amani ya hali ya juu, nyimbo ya Michael Jackson - Liberian girl ikagongelea msumari kuniaminisha hivyo... eh! Kumbe kujifunza muhimu bwana...

Hii nchi ndio yenye eneo lenye mkusanyiko mkubwa zaidi wa mabanda ya kuishi watu (Slums) hapa Africa, ambapo hupatikana eneo lijulikanalo kama The West Point ndani ya mji mkuu wa Liberia (Monrovia). Lakini cha ajabu ni kuwa, mbali na eneo hili kuwa na hali mbaya sana kiasi kwamba hapafai watu kuishi lakini bado watu wapatao 75,000 wanaishi ndani ya mabanda hayo.

Magonjwa ya mripuko ya mara kwa mara (hasa Kipindupindu), uhalifu usioisha, matumizi ya dawa za kulevya, ukahaba hasa kwa vijana wadogo na mfumo mbaya wa kudhibiti taka, the West Point ni eneo baya zaidi kuishi ndani ya Liberia.

Monrovia inatishiwa na maafa mengi ya kimazingira kama vile Mafuriko na Uchafuzi wa mazingira. Karibia kila punzi unayovuta hapa yaani inachosha kutokana na hali mbaya ya kimazingira.

16. MLIMA SINABUNG, INDONESIA. (MOUNT SINABUNG, INDONESIA)

Mlima huu unapatikana kwenye kisiwa kilichopo Indonesia kijulikanacho kama Sumatra. Huu ni mlima ambao una Volkano hai hadi sasa. Ni hatari sana kuishi au kuutembelea mlima huu kutokana na miripuko ya Volkano ya mara kwa mara inayoendelea pale.

Miripuko hii inapotokea, maelfu ya watu huachwa bila makazi huku vijiji mbalimbali vilivyopo kilomita kadhaa huwa vinaathiriwa kwa kufunikwa na vumbi zito la volkano pamoja na uji wake.

Miripuko ya hivi karibuni zaidi ilitokea mwaka 2010, 2013, 2014, 2015 pamoja na mwaka 2016. Miripuko hii ilisababisha vifo kadhaa pamoja na uharibifu mkubwa wa makazi ya watu.

17. NORTH KOREA (KOREA YA KASKAZINI)

Nchi hii inachukuliwa kuwa ni ya Kidikteta (totalitarian dictatorship), Korea Kaskazini ni Nchi iliyopo Asia ya Mashariki. Inaaminika kuwa ina ukiukwaji mkubwa wa haki za Binadamu.

Wenyeji na watalii wote kwa pamoja wanaweza kujikuta matatizoni hata kukamatwa kwa kujihusisha na mambo ambayo ni ya kawaida sana kwenye Nchi za kidemokrasia.

Nchi hii ina aina 15 tuu za mitindo ya kunyoa iliyopitishwa na Serikali huku pia ikiwa na Channel 3 tuu za TV. Korea kaskazini ndiyo Nchi ambayo kinyesi cha Binadamu kinatumika kama Mbolea. [emoji23][emoji23]

Pia adhabu ya makosa mbalimbali hata kama yamefanywa na mwanafamilia mmoja tuu huwatia wanafamilia wote hatiani na huadhibiwa kwa vizazi vyote vitatu vijavyo.

18. BURKINA FASO, MAGHARIBI YA AFRIKA

Ni Nchi ndogo, imepakana na Nchi jirani kila pande inayopatikana huko Magharibi ya Africa, Burkina Faso inajulikana sana kutokana na rekodi yake ya mashambulizi ya kigaidi kila uchwao. Pia kiwango kikubwa cha utekaji nyara watu.

Mashambulizi kadhaa ya kinyama yamefanyika kwenye migahawa, mahoteli, vituo vya mabasi n.k huku maeneo yanayolengwa zaidi yakiwa ni yale yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.

Pia mashambulizi kadhaa machache yalifanywa na makundi ya kigaidi yanayotoka Nchi jirani hasa Niger na Mali.

Hii Nchi kiuhalisia ipo huru kutokana na majanga ya kiasili ila upande wa pili ni tumwa kwa vurugu za kibinadamu.

19. HAITI

Moja kati ya Nchi ambazo zipo kwenye ukanda wa vimbunga, Haiti ndio Nchi ya tatu kwa ukubwa katika ukanda wa Carribean baada ya Cuba na Jamhuri ya Dominic.

Vimbunga vinavyopiga hapa kiuhalisia ni hatari sana, lakini hatari zaidi ni kuwa Nchi hii ipo kwenye wimbi kubwa la Umasikini. Nyumba nyingi hapa zimejengwa ndani ya ukanda wa maporomoko au mafuriko jambo ambalo linahatarisha Afya za wakazi wa Nchi hii.

Misitu na mapori ambayo ndio msingi mkuu wa kulinda ardhi isiharibiwe na majanga ya asili imevunwa kiholela ma kuiacha ardhi uchi. Uchumi wa Nchi hii pia kama nilivyosema juu hapo ni mbaya kiasi kwamba hawana hata uwezo wa kuweka Teknolojia inayoweza kutambua mabadiliko ya tabia ya Nchi au majanga yaliyo karibuni kutokea (Mf: Mafuriko, Tetemeko la Ardhi n.k).

Michael Jackson - We are the World. aliimba kuhamasisha utoaji wa misaada baada ya Nchi hii kupigwa na tetemeko kubwa la Ardhi.

NB; Pia kuna version ya kuchangia Sudan.

20. FUKUSHIMA, JAPAN

Fukushima, mtambo wa kufua nishati ya Nyuklia unaopatikana kwenye kisiwa cha Honshu huko Japan ulikumbwa na aina mbaya zaidi ya ajali ya Nyuklia kuwahi kutokea Duniani mwezi March mwaka 2011.

Baada ya tetemeko baya zaidi la Ardhi kutokea ndani ya Bahari ya Hindi kiasi likasababisha kutokea kwa Tsunami, mtambo huu (Kinu) wa Nyuklia uliripuka na kusababisha kuvuja kwa mionzi hatari ya Nyuklia katika eneo kubwa lililo karibu na kinu hiki. Hata leo hii (muongo mmoja tangu ajali hii itokee) bado kiwango cha mionzi ya Nyuklia kinarekodiwa kuwa cha juu zaidi katika eneo hili.

Mionzi hii inaathiri maisha ya viumbe hai katika eneo hili kwa kuwasababishia ulemavu hasa kwa Binadamu na Wanyama.

21. MAILU SUU, KYRGYZSTAN

Kusini mwa Kyrgyzstan , Mailu Suu ni moja kati ya miji yenye kiwango kikubwa cha mionzi yenye Sumu Duniani.

Eneo hili lina wakazi wapatao 23,000, eneo hili ni hatari sana kwa wakazi waishio hapo. Mailu Suu ndio eneo ambalo Tani 10,000 za madini ya Uranium zilichakatwa kwa ajili ya mradi wa Nyuklia wa Usoviet (Soviet’s nuclear programs).

Kuendelea kuishi ndani ya eneo hili kunasababisha ulemavu wa viungo na hasa kutokukua vizuri na hali hii itapitishwa vizazi hadi vizazi kwa wanaoishi hapa.

Pia hatari ya kuathiriwa na kemikali pamoja na mionzi inayotokana na madini haya y Uranium inaongezeka kila siku kutokana na matetemeko ya ardhi, maporomoko ya ardhi na mafuriko yanayolikumba eneo hili.

22. MANAUS, BRAZIL

Eneo linalochukua wakazi wapatao milioni 2, Manaus ni jiji linalopatikana Brazil.

Tofauti na majiji mengineyo ya Brazil, eneo hili halina uhalifu sana ukilinganisha na majiji makubwa mengine lakini hatari yake ni kuwa Hili jiji linapatikana katikati ya msitu mzito wa Amazon jambo linalozidisha hatari ya kuishi hapa.

Msitu wa Amazon ndio makazi ya viumbe wengi hatari pia mbaya zaidi hili jiji lipo kando ya Mto Amazon (Mto mnene na mkubwa zaidi Duniani). Kuwa na mto ni jambo zuri ila shida ni viumbe waliopo ndani yake.
Mfano:

01. Piranhas,
Hawa samaki wana meno makali pia wanakula nyama, ukimtupa mtoto ndani ya mto wenye hawa samaki ndani ya dakika moja tuu anabaki mifupa tupu.

02. Anacondas,
Hawa tunawafahamu ila kiufupi wanaua kwa kukubana hadi mbavu zipishane halafu wanakumeza.

03. Candiru,
Yeah.. huyu ndo hafai hasa kwa Wanaume, huyu samaki hana rangi (transparent) na anaingia kwenye njia ya mkojo anapitia hapo hadi aufikie mshipa mkubwa wa damu wowote halafu anajisevia hapo.

23. DALLOL, ETHIOPIA.

Eneo hili linapatikana Kaskazini ya Ethiopia, Dallol ni moja kati ya maeneo yaliyojitenga na ya chini kabisa Duniani. Wastani wa joto lake kwa mwaka ni 34.6 °C (94.3 °F), hili jiji ndio eneo lenye joto zaidi linalokaliwa na watu.

Maji yaliyopo kwenye ardhi hii hayawezi kutumiwa kwa shughuli yoyote ile kutokana na kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha tindikali (Acid) pamoja na Chumvi.

Pia eneo hili lina visima vya maji moto ambavyo hutoa gesi zenye sumu. Kutokana na kuwa ni eneo lililojitenga zaidi, hili eneo linajulikana kama Jiji lililokufa (Ghost Town).

Eneo hili linafanana sana na Jangwa la Danakil.

24. PEMBETATU YA BERMUDA. (THE BERMUDA TRIANGLE, NORTH ATLANTIC)

Moja kati ya maeneo hatari mashuhuri zaidi hapa Duniani ni Pembetatu ya Bermuda (pia wanaiita Pembetatu ya Shetani)., hili eneo linaogopwa sana na wachukuzi. Eneo hili limeenea kuanzia Florida kwenda Puerto Rico na kuishia visiwa vya Bermuda. Pembetatu hii imekuwa maharufu kutokana na matukio ya kutoweka kwa vyombo vya usafiri kama vile ndege na meli zinapokatiza ndani ya eneo lake.

Kutoweka huku kumehusishwa na nadharia mbalimbali ikiwepo nguvu ya uga sumaku iliyopo baharini hadi uwepo wa viumbe toka sayari nyinginezo (Aliens).

Ingawa hizi kesi zimekuwa na mantiki na kutoa baadhi ya fafanuzi zinazoeleweka lakini bado kutoweka kwa hivi vyombo vya usafiri kumeacha maswali mengi yasiyo na majibu.

SWALI KWA WANA JAMII FORUM: Jee! Unadhani kitu gani kipo pale kwenye pembetatu ya Bermuda kinachosababisha maafa yote haya?

25. ZIWA NYOS, CAMEROON. (LAKE NYOS, CAMEROON).

Ziwa hili limekaa kwenye eneo lililochimbika huku chini likiwa na shughuli za volkano hai. Ziwa hili lipo Kaskazini-Magharibi ya Cameroon, hewa ya ukaa (Carbon dioxide) huvuja kutoka chini ya miamba ya Volkano.

Ishu iko hivi, hii gesi ya Ukaa (CO2) hujikusanya nyingi chini ya miamba ya Volkano na kuhifadhiwa pale kama puto, lakini hili ziwa lipo juu ya miamba ya hii volkano. Sasa ikitokea presha ya mkusanyiko wa hii geni imekuwa kubwa (au volkano ikiripuka) hii gesi hutafuta pa kutokea, hivyo hutokea ndani ya maji ya hili ziwa kwa wingi zaidi. Lakini gesi hii ni nzito kuliko hewa (wale wa Chemistry watakumbuka hii) hivyo ikiingia kwenye mazingira husika husukuma Oksijeni yote inapanda juu na yenyewe (Carbondioxide) inachukua eneo lote ambalo ilikuwepo Oksijeni (displaces Oxygen).

Viumbe hai havivuti Carbondioxide, hivyo basi vitakufa kwa kukosa hewa ya oksijeni._

Miripuko miwili ya Gesi ya Ukaa ilitokea miaka ya 1980s, inakadiriwa kuwa vifo vya watu wapatao 1,700 vilitokea huku mifugo ipatayo 3,500 ikifa.

26. GUATEMALA, AMERIKA YA KATI (CENTRAL AMERICA).

Nchi hii inapatikana America ya kati, kusini mwa Mexico, Guatemala ina vollano nyingi sana, misitu mizito ya mvua, na maeneo ya kale ya watu wa jamii ya Maya (Wale waliwahi kuiona filamu ya APOCALYPTO, nadhani wanawakumbuka wale jamaa wanaowatoa kafara watu. Sasa wale ndio MAYANS wenyewe).

Hii Nchi inajulikana sana kwa kiwango kikubwa cha uhalifu. Lakini sio hivyo tuu, zipo sababu nyinginezo zinazoifanya hii Nchi iwe hatari kuishi na kuitembelea.

Eneo Nchi hii ilipo pamoja na hali yake ya ki-topojrafia inalifanya hili eneo liwe katika hatari ya kupigwa na Vimbunga, Maporomoko ya Matope pamoja na Matetemeko ya Ardhi. Mwaka 1976, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 7.5-magnitude lilitokea hapa na kusababisha kupoteza maisha kwa watu wapatao 23,000 wanaoishi hapa.

27. NAPLES, ITALIA

Jiji lililojizolea umaarufu kutokana na urembo wa mitaani karibia katika kila kuta ya nyumba, vyakula vitamu vya mitaani n.k... jiji hili ni moja kati ya majiji makubwa pale Italia.

Mbali na sifa zake nzuri, bado pia ina shida moja. Hili jiji limekaa kwenye eneo ambalo ni mtego wa kifo mkubwa pale Italia, hili jiji lipo juu ya volkano hai kubwa iliyopewa jina la ‘Campi Flegri’.

Wanasayansi kadhaa waliobobea wanaamini kuwa mripuko wowote hata kama ni mdogo wa volkano hii itakuwa ni kama Cheche iliyodondokea kwenye tanki la petrol (kwamba volkano yote iliyopo chini ya miamba ya mji huu itapitia hapo kwa presha kubwa na kufumua mji wote) na kuua wakazi wote wa mji huu.

Asee... kuishi hapa kila siku ni sawa na kusema umekanyaga bomu la kutega ardhini (Landmine), mda wowote kitu kitaripuka. Lakini cha ajabu bado watu wanaishi fresh tuu kana kwamba hakuna chochote cha hatari pale. [emoji23]

27. SANAA, YEMEN

Moja ya majiji ya zamani zaidi na yasiyokalika Duniani, Sanaa ni mji mkuu wa Yemen. Upo katika muinuko wa mita 2,300, ndio unaaminika kuwa mji mkuu ulioinuka zaidi Duniani.

Kutokana na uwepo wa vurugu za mara kwa mara, eneo lolote kwenye mji huu linaweza kugeuzwa uwanja wa vita wakati wowote ule.

Hii ndio historia ya Sanaa, eneo lililofunikwa na Hofu, kupigwa mabomu mara kwa mara, matukio ya ugaidi yasiyotabirika n.k.

28. SYRIA

Nchi hii ilikuwa ni mafikio mazuri ya watalii kutokana na kuwa na vivutio mbalimbali za Milki za kale, Utamaduni wao n.k. Shida imeanzia pale walipotaka kumpindua Rais Bashar Al-Assad ambae anapata sapoti kutoka kwa washirika wake (Russia ikiwemo).

Tangu kuibuka kwa Vita ya wenyewe kwa wenyewe, Syria hadi leo hii haikaliki. Mabomu yanarindima kila uchwao, matumizi ya siraha za Kemikali (Mfano: Gesi zenye sumu), mashambulizi kutoka kwa waasi na makundi ya kigaidi (Mfano; ISIL), mashambulizi kutoka Nchi hasimu kama Israel n.k yamedhoofisha amani ya Nchi hii.

"Wanayo pesa kwa ajili ya Vita ila wanashindwa kuwalisha masikini"
- TUPAC AMARU SHAKUR

K A R I B U N I

Picha nitazipanga kwa kufuata kila kipengele, Mf: Ya kwanza (Dealth Valley), Ya pili (Hawaii) n.k

2022-01-17-20-42-10-515930610.jpg
View attachment 2108405
2022-01-17-20-42-17--502830803.jpg
2022-01-17-20-42-21--912249878.jpg
2022-01-17-20-42-25-1820783845.jpg
2022-01-17-20-42-32--790810173.jpg
2022-01-17-20-42-37-2029697902.jpg
2022-01-17-20-42-43--1417450270.jpg
2022-01-17-20-42-48-1259448604.jpg
2022-01-17-20-42-52-874834889.jpg
IMG_20220205_035741_512.jpg
2022-01-17-20-42-28-1679279648.jpg
IMG_20220205_023223_782.jpg
IMG_20220205_023225_081.jpg
IMG_20220205_023227_494.jpg
IMG_20220205_023228_800.jpg
IMG_20220205_023231_287.jpg
IMG_20220205_023232_850.jpg
IMG_20220205_023234_690.jpg
IMG_20220205_023237_026.jpg
IMG_20220205_023238_909.jpg
IMG_20220205_023240_430.jpg
IMG_20220205_023242_966.jpg
IMG_20220205_023244_973.jpg
IMG_20220205_023246_433.jpg
IMG_20220205_023248_288.jpg
IMG_20220205_023250_793.jpg
 
L. Natron kwa sifa hizo nini nafasi au umuhimu wake kwa uchumi wa nchi?
 
Duuh nimeachwa hoi hapo kwenye baridi ya kugandisha mpaka mate na machozi aisee😂😂.

Huwa tunasema wenyeji wamezoea hali hizo na huwa na mbinu zao asili za kupambana na majanga japo mengine hayazuiliki hivyo huambulia kifo ama ulemavu wa kudumu.
 
View attachment 2108406View attachment 2108405View attachment 2108408View attachment 2108407View attachment 2108409View attachment 2108410View attachment 2108411View attachment 2108412View attachment 2108414View attachment 2108413View attachment 2108416View attachment 2108415View attachment 2108418View attachment 2108417View attachment 2108420View attachment 2108419View attachment 2108421View attachment 2108422View attachment 2108423View attachment 2108424View attachment 2108425View attachment 2108428View attachment 2108429View attachment 2108427View attachment 2108431View attachment 2108432View attachment 2108433
very very interesting for sure
 
Back
Top Bottom