Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
1. Sehemu za Kazi: Rushwa ya Ngono kazini ni pamoja na waajiri kutoa ajira kwa Wanawake na faida nyingine kama vile kupandishwa cheo, nyongeza ya mshahara, siku za kupumzika kwa kubalishana na Ngono.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) ulieleza 89% ya Wanawake walioajiriwa katika Sekta ya Umma Nchini wamewahi kuombwa Rushwa ya Ngono.
2. Ofisi za Umma: Ofisi zinazotoa huduma mbalimbali za Usajili wa vyeti, utoaji wa leseni, vitambulisho, pasi za kusafiria nk, baadhi ya watumishi wanaweza kuomba Rushwa ya Ngono kwa kubadilishana na upatikanaji wa haraka wa nyaraka hizo.
3. Taasisi za Elimu. Taasisi za elimu kuanzia ngazi ya shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu ni eneo hatarishi pia kutokea kwa rushwa ya ngono kwa walimu kuomba ngono kwa kubadilishana na alama za ufaulu nk.
Kwa mfano; kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya kuzuwia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU, ukivihusisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma, asilimia 50 ya waliohojiwa walieleza uwepo wa rushwa ya ngono katika vyuo vikuu, huku asilimia 29.9 ya wafanyakazi wakieleza kuwepo kwa ushawishi wa makusudi ili kujipatia huduma kutoka kwa mamlaka
4. Maeneo mengine ya Huduma: Rushwa ya ngono inaweza kutokea katika meneo mengine ya utoaji huduma kama vile mahospitalini, mahakamani nk. Kwa mfano katika mahospitali kumekuwa na kesi kadhaa zikionesha madaktari wakishutumiwa kufanya ngono na wagonjwa ili kuharakisha matibabu yao, au kuwapatia dawa za matibabu.
WiLDAF