Maeneo unayopaswa kuyawekea nidhamu

Maeneo unayopaswa kuyawekea nidhamu

Gwamanga

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2021
Posts
223
Reaction score
434
Je nimaeneo gani naweza yawekea nidhamu?! Maeneo yafuatayo ni miongoni mwa maeneo ambayo mtu yoyote anatakiwa ayape kipaumbele kwenye kuyawekea nidhamu!!

#Eneo la kujiwekea malengo binafsi kila mwaka.
Kujiwekea malengo na kuyapa vipaumbele hii itakufanya kujua nitaanza na hili na kwa nini nianze nalo lipi nilitilie mkazo sana, lipi niliwekee mda wangu mwingi. mfano. mwaka huu nitafanya a, b, c
Mtu mwenye malengo anajua kule anakoenda, mtu asiye na malengo hawezi kwenda na hajui anakokwenda.
#Nidhamu ya kutunza muda
Tatizo tulilo nalo ni kutokutunza muda.

Maisha tunayoishi yanawakilishwa na kitu kidogo kinachoitwa muda
Kimsingi maisha yako ni muda wako, na muda wako ni maisha yako.

Jiwekee tathimini ni kwa namna gani unavyotumia mda wako, Tathimini ya siku, wiki, Mwezi na mwaka pia.
#Nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii na Maarifa.

#Nidhamu ya kujitunza kiafya.
#Nidhamu ya kuweka akiba na kuwekeza.

Kuwekeza ni kutumia baadhi ya vitu / kitu ulicho nacho kutengeneza mkondo mwingine wa fedha, Uwekezaji unahitaji nidhamu.

#Nidhamu ya ujasiri na ushujaa
Kila mtu duniani anaogopa kitu fulani, Lakini watu ambao wamefanikiwa ni wale wanaoishinda hofu au woga, Kuna hofu ya kweli na isiyo ya kweli.

Ujasiri unakufanya uwe na uwezo wa kumiliki mambo makubwa au biashara kubwa.

#Nidhamu ya kujifunza.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom