Maeneo ya kishua Dar? Taja eneo lako kama sijataja

Maeneo ya kishua Dar? Taja eneo lako kama sijataja

Nilijenga mwaka 1990 baa ya Club de Masen Kigogo nimeiuza kitambo kwa sasa nipo aidha Italy au Manundu Korogwe na nina cash; je mimi ni poor?
 
Tabutupu,
Kikawaida majina mara nyingi hukupa picha ya eneo kabla hujafika!

Ila nilicho-note ni kwamba sehemu zenye majina ya kizungu au linalovutia huwa za kishua by nature (Masaki, Mikocheni, Sea View, Oysterbay) ila jina likiwa la kiswahili ogopa sana! Pata picha jina kama Njiayang'ombe, Kwafundi Redio, Kwatumbo, Kigogo, daaah 😂😂
Goba, kinyerezi magomeni kwa sheikh yahaya na kijitonyama kwa makinda mbona majina ya kimatumbi!!
 
l
Goba, Kinyerezi, Magomeni kwa Sheikh Yahaya na Kijitonyama kwa Makinda mbona majina ya Kimatumbi!!

Wabongo bana! Nishasema hapo 'nilicho note ni kwamba sehemu zenye majina ya kizungu au yanayovutia'

Huoni kama hiyo sentesi imetoa uhuru kwa majina mengine? Hata mie nimetaja Masaki na Mikocheni kama mfano!
 
Haya maeneo viwanja vyote vimepimwa na vimepangwa na watu wanao ishi huko ni wakueleweka. Kama umejenga au unaishi maaneo haya wewe ni wa kishua.

Baadhi ya maeneo haya:

Masaki
Mbezi beach
Mbweni
Mivumoni
Mikocheni
City center (Dar)
Sinza
Kigamboni
Kariakoo
Msasani peninsula
Etc


Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye hio list zinazostahili ni
Masaki
Mbezi beach
Mbweni(sio yote)
Mikocheni(sio yote)

Kigamboni sio ushuani,nasema hivi nikiwa mkazi wa Kigamboni. Labda Kibada ndio kumepimwa na kuna nyumba za kueleweka.
 
Back
Top Bottom