Maeneo ya Ukraine yaliyokwapuliwa na Urusi kwa mkakati maalumu

Maeneo ya Ukraine yaliyokwapuliwa na Urusi kwa mkakati maalumu

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Haya maeneo ambayo Ukraine hataki kwenda meza ya mazungumzo pasipo kukabidhiwa
download.jpg

.Russia amekwapua maeneo hayo kwa ajili ya mkakati wake wa kuikabili NATO.

Kama Ukraine atang'ang'ana na mpango wake wa kwenda NATO hayo maeneo asahau katika ramani ya Ukraine.
Ukraine ameshupaza shingo na NATO yake acha ashupaze maeneo yamenyakuliwa na hawezi kuyarudisha kamwe.

Meza ya mazungumzo haina mambo magumu ni kwamba achana na NATO ,tukuachie maeneo yako hataki
 
Haya in maeneno ambayo Ukraine hataki kwenda meza ya mazungumzo pasipo kukabidhiwa
.Russia amekwapua maeneo hayo kwa ajili ya mkakati wake was kuikabili NATO....
1. Kama Ukraine ataachana na mpango wake was kwenda NATO hayo maeneo asahau katika ramani ya Ukraine.

2.Meza ya mazungumzo haina mambo magumu no kwamba achana na NATO ,tukuachie maeneo yako hataki
Mkuu, labda hebu fanya editing sentensi hizo 1 & 2 ili ueleweke kwani zinakinzana(Contradicting).
 
Haya maeneo ambayo Ukraine hataki kwenda meza ya mazungumzo pasipo kukabidhiwaView attachment 2474970
.Russia amekwapua maeneo hayo kwa ajili ya mkakati wake wa kuikabili NATO...
Kwa hiyo Mrussi amekwapua na kuyashikilia hayo maeneo ili yatumike kama rehani, poni au "Mzigo" au dhamana/shinikizo la kwamba ili yarudishwe lazima Ukraine aachane na mpango wake wa kujiunga katika ushirika wa NATO?

Kama ndo hivo, manake Urussi anataka naye aunde ka-ushirika fulani kwa nguvu ili kukabiliana na NATO. Ukisikia UBEBERU; huo ndio wenyewe katika uhalisia kamili. Utanichaguliaje rafiki, utanipangiaje nifanye nini ilhali mm ni mtu mzima kiakili na kiroho na niko huru?

Inaonekana Mrussi kuna kitu hakiko sawa huko kichwani mwake.
 
Unapopigana ngumu mojawapo ya sehemu yavkulinda sana ni usoni. Maana ukipigwa ngumi ya uso sawasawa lazima utolewe ulingoni kabla ya wakati(TKO).

Moscow ndio uso wa Russia na njia pekee rahisi kufikia Moscow kutokea Ukrain ilikua Crimea.

Hivyo kwa kuchukua maeneo hayo Urusi imeficha uso wake kwelikweli.

Ndio maana kauli ya Ukraine tunataka Crimea. Mengine jazia
 
Kwa hiyo Mrussi amekwapua na kuyashikilia hayo maeneo ili yatumike kama rehani, poni au "Mzigo" au dhamana/shinikizo la kwamba ili yarudishwe lazima Ukraine aachane na mpango wake wa kujiunga katika ushirika wa NATO?

Kama ndo hivo, manake Urussi anataka naye aunde ka-ushirika fulani kwa nguvu ili kukabiliana na NATO. Ukisikia UBEBERU; huo ndio wenyewe katika uhalisia kamili. Utanichaguliaje rafiki, utanipangiaje nifanye nini ilhali mm ni mtu mzima kiakili na kiroho na niko huru?

Inaonekana Mrussi kuna kitu hakiko sawa huko kichwani mwake.
Wewe ndiye unaumwa unaufananisha mgogoro wa NATO vs RUSSIA na familia au Halmashauri yako ya kichwa nakuomba ukasome upate faida na ukijua hata siku moja hutokuja toa mfano ya kitoto kama ulivyofanya sasa hivi
 
Back
Top Bottom