Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Utangulizi
Kimsingi, maeneo yote ya wazi ni ya umma. Ni maeneo yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya shughuli za kijamii na hata kiserikali. Maeneo haya sii lazima yawe tupu; ni maeneo yasiyokuwa na majengo ya aidha makazi au ya shughuli nyingine za kibiashara. Maeneo haya ni pamoja na viwanja vya michezo; bustani za kupumzikia; makaburi; maeneo ya taasisi mbalimbali za umma kama mahospitali, shule, vyuo; masoko, hifadhi za barabara, hifadhi za misitu, hifadhi ya vyanzo vya maji, fukwe za bahari, maziwa, na kadhalika.
Maeneo ya wazi ni muhimu kwa afya ya mwili na akili
Kwa mujibu wa Blog ya Evergreen, tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, kuwa kwenye maeneo ya asili ni vizuri kwa afya yako, na pia huimarisha kinga ya mwili, huboresha afya ya moyo na afya ya kimetaboliki. Maeneo ya wazi, hufungua fursa ya watu - majirani na wengine kutoka maeneo mengine kukutana na kubadilishana mawazo, ikiwa ni pamoja na kubadilishana fursa mbalimbali. Maeneo ya wazi (hasa yale ya michezo na ya kupumzikia) yanaweza kutumika kama sehemu ya kupata hewa safi na hata kupunguza msongo wa mawazo, jambo ambalo ni muhimu kwa afya ya mwili na afya ya akili.
Kilelezo Na. 1: Eneo la Wazi kwa Ajili ya Kutembea na Kupumzika
Chanzo: Blog ya Evergreen
Maeneo ya Wazi/Umma Yanawezesha Miji kuwa Endelevu
Kwa mujibu wa blog ya Evergreen, maeneo haya yana kiwango kidogo cha hewa ya ukaa na himilivu wa hali ya hewa ambapo huwezesha miji kuwa endelevu. Maeneo ya bustani yana umuhimu mkubwa katika mazingira ya miji, ikiwa ni pamoja na kupunguza uwezekano wa mafuriko, uchafuzi wa hewa na kupunguza joto.
Maeneo ya Wazi/Umma Yanaweza kufanya miji Kuwa Salama.
Mwanaharakati Jane Jacobs aliandika kwamba majirani walijiona wako salama walipoonana mtaani. “Kuna hali ya usalama kuwa nje na kuwa maeneo ya umma,” anasema Massimi. Tunaona kinachoendelea, kama kuna tukio au hali yoyote inayotokea yenye madhara”. Jinsi ambavyo maeneo ya umma yamepangwa yanaweza kuchangia usalama wa umma. Maeneo ya wazi yenye nafasi ya kutosha ya kutembea na mwanga wa kutosha yatasaidia kuona vizuri mtaa
Kama nilivyosema awali, maeneo ya wazi sii tupu. Ni maeneo yanachangia kuongeza thamani ya Maisha, afya na Uchumi wa jamii. Maeneo ya wazi yanachangia kuwa na miundombinu ya kijani ya kusaidia kudhibiti mabadiliko ya tabianchi, kudhibit mafuriko, na kutoa huduma za kiikolojia. Huduma hizi katika miji na vijiji ni muhimu sana kwa ajili ya Maisha endelevu ya baadaye, na zinapaswa kuwa katika mipango ya taifa.
Uvamizi wa Maeneo ya Umma
Ingawa uvamizi wa ardhi ni kosa la jinai chini ya fungu la 177 (3) la Sheria ya Ardhi (Sura 113), bado kuna matukio mengi nchini ya kuvamia maeneo yanayomilikiwa na aidha serikali na/au taasisi zake, taasisi za kiraia, makampuni binafsi na watu binafsi. Baadhi ya Maafisa Ardhi wanatuhumiwa kuuza maeneo ya wazi au ya umma, na hata yanayomilikiwa na watu au taasisi mbalimbali kinyume na sheria/utaratibu, hali ambayo husababisha migogoro isiyoisha baina yao (wanaouziwa) na wamiliki halali.
Ndio maana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula, katika Mkutano Mkuu wa Nane wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji, Machi 29, 2023, amewaagiza Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za mitaa kupima, kulinda na kusimamia maeneo yote ya umma na maeneo ya wazi ili kuondokana na mwenendo mbaya unaoendelea kukithiri wa kuvamia maeneo hayo. Amesema Maeneo hatari kimazingira pamoja na maeneo ya wazi, yakiwemo maeneo maalum kwa matumizi ya baadaye (land bank), yanapaswa kupimwa na kulindwa dhidi ya wavamizi. Alisema ili tuwe na miji nadhifu na iliyopangwa vyema katika nchi yetu hakuna budi kuanza kusimamia upangaji wa miji midogo na vitovu vya vijiji vyetu. Alisema, "Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi 2022 inaonyesha kuwa miji inakuwa kwa asilimia 4.8 na taarifa tulizonazo tuna jumla ya miji midogo inayochipukia 4,310 nchini ambayo isiposimamiwa ipasavyo itakuwa miji holela ya baadae," Alisema.
Ni Muhimu Kupanga Miji na Vijiji
Upangaji mzuri wa miji na vijiji huhakikisha maeneo ya wazi na ya umma yanategwa na kupimwa. Hii itapunguza kama sii kuzuia kabisa uvamizi wa maeneo haya.
Katika Mkutano huo wa Bodi ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji, Machi 29, 2023 Waziri Mabula alisema "Kwa kutambua umuhimu wa miji hiyo na uwepo wa kasi ndogo ya upangaji wa vijiji nchini, Wizara imeandaa mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini ili kuwezesha jamii yetu kuanza kupanga maeneo yao kuanzia vijijini". Aidha alitoa maelekezo kwa Bodi na wanataaluma wote kuweka mkazo zaidi katika namna ya kuzuia miji yetu midogo na vijiji kuwa makazi holela ya baadae kwa kusimamia na kuelimisha jamii matumizi ya mwongozo wa upangaji na ujenzi wa nyumba bora vijijini.
Kwa kawaida, serikali huwa na mipango na ahadi nzuri, lakini changamoto ni utekelezaji. Kwa sababu, matatizo ya ardhi nchi hii hayajawahi kupungua, ingawa kuna wataalamu wengi wa ardhi wanaozalishwa na vyuo vyetu hapa nchini kila mwaka, na naamini kila halmashauri nchini ina wataalam na bajeti ya kutosha kuwezesha udhibiti wa migogoro ya ardhi.
Mapendekezo
Serikali ishirikishe watu na/au taasisi binafsi katika swala la upimaji wa miji na vijiji ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maeneo au viwanja rasmi, ikiwa ni pamoja na maeneo ya umma.
Kwa upande wa vijijini, serikali itenge maeneo ya wafugaji na ya wakulima kuepusha migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji; ikiwa sambamba na kuwezesha na kuhamasisha wafugaji kuacha kufuga kiholela, na badala yake kufuga kisasa, ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya mifugo kulingana na ukubwa wa eneo husika.
Serikali ichukuwe hatua kali za kinidhamu kwa maafisa ardhi wanaouza maeneo ya wazi na/au ya umma kinyume na taratibu na sheria za ardhi.
Hitimisho
Maeneo ya wazi ni muhimu kwa afya mwili na akili, yanaweza kutumika kuboresha hali ya hewa, na hata shughuli za kitalii; hivyo yana faida kwa maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi.
Marejeo
The Benefits of Public Spaces in Cities | Evergreen
Why is Open Space Important? - TEP - The Environment Partnership

Upvote
4