Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Maeneo yenye maisha tofauti Dar es Salaam

Mikoani kuna maisha ya hadhi mara kumi ya dar
Maisha ya hadhi unamaanisha nini?
Mkoa gani hapa Tanzania una maisha ya hadhi mara kumi ya DSM?
Mbeya, Mwanza, Arusha au Katavi?
Unajua idadi ya wabunge wa mikoani wanaoishi DSM?
Unajua idadi ya mawaziri wanaoishi DSM?
Wagombea uraisi mwaka huu ninawafahamu 11 kati ya 13 wanaishi DSM hadi mgombea uraisi Zanzibar.
Wakuu wa majeshi wastaafu.
Kwanini hawa wote wasiende kukaa Mpanda au Katoro au Ngarenanyuki?
 
Mtaa upo ila katerero hakuna sasa hivi.
Katerero imebaki mwananyamala Hosp, sugar ray temeke, tegeta kibo, tabata 40/40, sinza bigbon sheli, conar bar, meeda orodha inaendelea.....
Kwani mkuu sugar ray bado inafanya kazi?
 
Maisha ya hadhi unamaanisha nini?
Mkoa gani hapa Tanzania una maisha ya hadhi mara kumi ya DSM?
Mbeya, Mwanza, Arusha au Katavi?
Unajua idadi ya wabunge wa mikoani wanaoishi DSM?
Unajua idadi ya mawaziri wanaoishi DSM?
Wagombea uraisi mwaka huu ninawafahamu 11 kati ya 13 wanaishi DSM hadi mgombea uraisi Zanzibar.
Wakuu wa majeshi wastaafu.
Kwanini hawa wote wasiende kukaa Mpanda au Katoro au Ngarenanyuki?
Majority ya wakazi wa dar maisha duni, nyumba za hovyo, mlo shida
 
Hii nchi gani iko hivi?ipo ulaya,asia au africa?
Hapo ni Maharashtra India. Hapo chini ni masaki/msasani.
Sosi: Johnny_Miller_Photography
IMG_20201004_092147.jpg
 
Yafuatayo in baadhi ya maeneo yaliyokaribu sana kijeografia ila yana hadhi tofauti kimaisha.

1. Sinza na Tandale
Mitaa hii ipo karibu sana ila hali ya maisha ya watu wake in tofauti kabisa. Tandale watu wengi wana maisha ya chini na uswahili pia.

2. Kawe na mikocheni
Kawe kuna uswazi ila jirani zao mikocheni kwa warioba wanakula upepo

3. Masaki na msasani
Hapa tajiri anakutana na maskini moja kwa moja. Ukimaliza tu masaki na kuanza msasani unaanza kuona ladha ya umasikini. Msasani kuna slum.

4. Mtongani na bahari beach/ununio.
Watu wa mtongani wana maisha ya chini sana shughuli yao ni uvuvi, kokoto na bodaboda ila jirani zao bahari beach ni maghorofa na mitaa iliyopangika vizuri na watu maarufu wako huko.

Hayo ni maeneo ambayo wenye nacho na pangu pakavu wanaishi pamoja kwa ukaribu
Dodoma kuna sehemu wanaita Kilimani na Chenyoyo
Kilimani wanaishi watu wenye pesa na matajiri wa Dodoma wakati Chinyoyo wako wazee wa pamgu pakavu mnoooo
 
Kwenye kona ya coka hpo kuna duka kwa mpemba Osama ukinyoosha unakwenda kwa rwakatare
Sasa wee unakunja kushoto hko ndani ndani kna squatter lbda kma sahv watu wamewahamisha

Ova
Mkuu eneo hilo linaongoza kwa massage services centre wenyeji wengi wanapangisha na kusonga madale, kerege, goba etc

Mkali wa kama google earth mpaka osama unammanja
 
Natamani ungeambatanisha na tupicha kidogo maana kuna wengine tangu tuzaliwe huku mikoani hatujawahi kufika Dar.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Dodoma kuna sehemu wanaita Kilimani na Chenyoyo
Kilimani wanaishi watu wenye pesa na matajiri wa Dodoma wakati Chinyoyo wako wazee wa pamgu pakavu mnoooo
Hiyo mitaa ipo jirani ?
Nani kamkuta mwenzake?
 
Back
Top Bottom