Maestro Kisheti

Maestro Kisheti

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
MAESTRO ANDREA PIRLO 'REGISTA' THE FOOTBALL PIANIST VERSION YA LEIFE ANDSNES
.
Unamfahamu mtu mmoja anaetambulika na dunia kama mwenye ubora kwenye piano Kama Leif Ove Andnes, huyu bwana alipewa utukufu huo miaka ya 1970 mbele ya watu kama Martha Argerich, Claudio Arrau na Vladimir Ashkenazy
.
Kwenye soka Kuna binadamu mmoja kutoka nchi yenye hewa kutoka bahari ya Mediterranean, anaitwa Andrea PIRLO, huyu bwana ndie aliyeleta ladha mpya ya deep lying playmaker, Waitaliano wanaita Regista, neno lililotokana na movie, sahau kidogo kuhusu Tranquarista na aina zingine za maneno ya Kiitaliano.
.
Hold up a bit, unakumbuka Ile Italia ya World Cup 2006?? Waliketi kwenye hotel ya Landhaus Milser yenye hadhi ya nyota 5, walistahili kwakuwa walikuwa na mtu Kama PIRLO, alistahili heshima hiyo, kwenye michuano Ile PIRLO alikuwa na kazi ya kufanya dhahania iwe uhalisilia, hakuwa na speed wala nguvu bali utulivu tu.
.
Aliwasahaulisha Waitaliano juu ya Marco Tadelli, Ile rough tackling, ubabe na roho mbaya, yeye alicheza chini, alipiga pasi ndefu na kutawanya ngome za ulinzi atakavyo, Regista imezaliwa, PIRLO kutoka Brescia anasumbua Italia, the new football artist, hakutumika kama Orthodox 10
.
Mario Zagallo wa Brazil aliwahi kutengeneza pattern miaka ya 90 Ila bado haikuwa tamu, aliamini kuna mtu alipaswa kucheza Kati ya center midfielders wawili, Ila hakumpata, aliishia kumwambia Calros Alberto kuwa ipo siku atazaliwa binadamu wakuelewa nachotaka.
.
Mabadiliko ya Sheria offside zilitaka timu zicheze kutoka 40 yards mpaka 70 yards, hapa Pirlo akazaliwa, pale Juventus viungo watatu, Vidal, Pogba na Marchisio, alafu chini yao Kuna Pirlo, kazi yao ni kumtengenezea nafasi na yeye kupiga michimbo yake, alikuwa mnyama mpaka akawa anakuja kucheza back four eneo la mabeki [emoji2].
.
Wazo la miaka ya 90 linatekelezwa Turin, Pogba kutoka Afrika na Vidal kutoka Chile wanampa anachotaka Pirlo, anabeba vision, anacheza anavotaka na pasi zake, tulifurahi tulienjoy Ila ilikuwa kazi ya muda mrefu, Pirlo kashinda kila kitu kasoro UEFA.
.
Asante Andrea Pirlo Maestro, ulikuja na kiungo mpya wa ulinzi asiyetumia nguvu, Asante Carlo Mazzone kwa kutuletea Andrea The Football Architect.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Manuel Rui Cost , Gattuso,pirlo,na mbrazili left shooter

Kati ya hawa ulio waweka hapa Pirlo remains the best, kwa ladha yake ya uchezaji, Rui costa chenga zilikuwa nyingi, Gattuso undava mwingi mno. Kwa kiasi flani Luca Modric anataka kufanana na Pirlo kwa zile touch zake.
 
bahati mbaya humjui Pirlo ila unampenda

pirlo amebeba Uefa champions league 2007

amezungukwa na mdachi mmoja muitaliano mmoja mbrazili mmoja juu ya yupo mtu kutoka Ukraine
acha Milan hiyo ww
juve kaja mzee
 
Unanikumbusha pirlo ndani ya diamond formation ac milan anakufa kwa liver katika usiku wa istanbul miracle!! Hapa pirlo juu kidogo gattuso huku seerdorf juu kaka as ACM mbele kabisa shevchenko na mjomba crespo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
bahati mbaya humjui Pirlo ila unampenda

pirlo amebeba Uefa champions league 2007

amezungukwa na mdachi mmoja muitaliano mmoja mbrazili mmoja juu ya yupo mtu kutoka Ukraine
acha Milan hiyo ww
juve kaja mzee
mimi pia nmeshangaa eti anamzungumzia Pirlo wa juve akiwa na kina Pogba [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom