Mafanikio Hujengwa kwa nidhamu

Acha utoto....

Hela.. nidhamu bila hela.
 
Akha! kwahiyo mnatubadirikia tena si mlisema uchawi na freemason!, kwanini mnatuchanganya sasa tushike lipi..??
Amesema MAFANIKIO .kwani wewe neno mafanikio unalielewaje?
 
"Mafanikio huja kwa kupenda unachofanya"

Fid q, ielewe mitaa
 
Kwanza hili neno mafanikio ni dhana pana sana.

Watu wanapenda kulifanyia Hasty generalization.

Kitu unachodhani wewe kwako ni mafanikio makubwa sana, Kwa mwingine ni kitu kidogo sana.

Mfano kwa waafrika wengi hasa watanzania mtu akishajenga nyumba akanunua gari, akapeleka watoto wake English mediums. Basi anaona hayo ndio mafanikio.

Kumbe kwa wengine tunamuona bado maskini tu, Hana mafanikio yeyote.
 
Sioni kama kuna haja ya kuwazungumzia watu wengine, Maana kila mtu amebeba dhana yake juu ya mafanikio yake. Je, wewe kwa upande wako unatafsiri vipi mafanikio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…