SoC01 Mafanikio katika Umakini wa Mikakati

SoC01 Mafanikio katika Umakini wa Mikakati

Stories of Change - 2021 Competition

Olichite

New Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
1
Reaction score
0

1.1 Utangulizi​

Katika muingiliano unaotabirika na usiotabirika wa mambo mchanganyiko ambayo yanaathiri dunia katika upande chanya na hasi hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, kufanikiwa kunahitaji umakini katika mikakati ili shughuli ambazo mtu au taasisi imeanzisha au ni endelevu zifanikiwe. Ili kufanikiwa katika hilo umakini katika kimikakati hauepukiki ili kuwa na nadharia endelevu (Going concern).

1.2 Tafsiri ya Misamiati ya Andiko​

1.2.1 Mafanikio​

Mafanikio maana yake ni kitendo cha kufikia malengo au ya mtu au taasisi yoyote inayojishughulisha na shughuli yoyote yenye kuleta maendeleo. (Mwaandishi, 2021)

1.2.2 Umakini wa Mikakati​

Umakini wa Kimikakati maana yake ni kwa mtu au kitendo cha kuanzisha na kupanga mikakati au kudhibiti mambo yasiyotabirika na yanayotabirika yanayoweza kuathiri maendeleo kabla isipokuwa kupambana nayo baada yakutokea. (Mwaandishi, 2021)

1.3 Umakini wa Kimikakati katika Nyanja tofauti za Kimaendeleo​

Kila mtu au taasisi huwathiriwa katika upande wa hasi au chanya kupitia sababu za ndani na nje. Sababu za ndani ni zile ambazo mtu au taasisi ana/ina uwezo wa kudhidhibiti kimikakati kama vile malengo, na sababu za nje ni zile ambazo mtu au taasisi anahitajika kuzifuta kutokana na kutokuwa na uwezo wa kudhidibiti mfano ni sheria za nchi. Andiko hili limeeleza mambo yafutayo;

1.3.1 Umakini wa Mikakati katika Uchumi na Biashara​

1.3.1.1 Hali ya Ukosefu wa Ajira

Umakini wa Mikakati katika kukabiliana na jambo hili ni lazima kwa nchi husika kwa kubadili mfumo wa elimu pia na kuondoa fikra za watu wasome ili wapate ajira. Elimu ya kujitegemea ni mzuri zaidi kwa kumwandaa mtu ambaye anaweza kufanikiwa katika shughuli zake na kujiwekea umakini wa mikakati ambayo pia anajua inaweza kumwathiri moja kwa moja na kwa kutokuwa moja kwa moja ambayo kupambana na majanga yanayoweza kuathiri uchumi wake kama katika kipindi hichi cha sakata la COVID-19. (Mwaandishi, 2021)

1.3.1.2 Wizi wa Mitandao

Umakini wa Kimikakati unatakiwa uwe na njia mbadala wa kushughulikia linapotokea tatizo kwa wateja ambao wanaweza kupoteza fedha zao kutokana na changamoto za mtandao na kuathiri uchumi wao. Katika hatua hii napendekeza angalau kuwa na sera ya kiuchumi ambayo haitaathiri mteja kwa makubaliano kuwa gharama za huduma (service charge) zigawanywe kwa kuwawekea wateja binafsi na kitaasisi akiba (kama mfumo wa kibima) ambayo anapopotwa na majanga ya wizi wa mtandaoni anaweza pata fidia kwa mchango ambao alichangia kupitia gharama za huduma ya uhifadhi wa pesa zao ambazo zinazoendesha uchumi. (Mwaandishi, 2021)

1.3.1.3 Mshitukizo wa Bei za Rasilimali tegemezi katika Uchumi wa Nchi​

Kila nchi ina rasilimali ambazo hutegemea kama ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yao na watu wao. Kupambana na changamoto ya bei za rasilimali husika zinazotegemea uchumi wa nchi umakini wa mikakati katika bei ya rasilimali lazima uzingatiwe kwa kuangalia uchumi wa dunia unapushuka rasilimali hizo pia hupungua bei hivyo kama mahitaji ya rasilimali hiyo ni kubwa basi uchache wa rasilimali sokoni lazima upungue ili watu wahitaji kwa bei ambayo nchi inaweza kupanga kwa mahitaji ya dunia. (Mwaandishi, 2021)

1.3.1.4 Utawala Mbovu katika Nchi

Utawala ambao una umakini katika mikakati ya sheria za nchi na kanuni na taratibu huboresha hali ya maisha kwa kila raia ndio ambao unahitajika. Japo changamoto ya sheria ni pale ambapo mabadiliko yasiyotabilika yanapotokea na kuathiri masuala ya kiuchumi basi sheria zinakuwa ngumu kubadilika ili kuendana na mazingira hayo, hivyo basi ili kuondokana na changamoto hii basi nchi inapotunga sheria lazima izingatie vipaumbele na pia izingatie mambo yasiyotabirika ili sheria iseme inapambana vipi na matukio au majanga hayo ya dharura yaliyojitokeza ili kuhimili hali ya uchumi iliyopo. (Mwaandishi, 2021)

1.3.1.5 Changamoto ya Ukusanyaji wa mapato na Matumizi ya Serikali

Serikali inatakiwa kupunguza kukopa inapukuwa na ombwe la mapato na matumizi kwani huleta athari za kiuchumi ambazo zinaweza zikadumaza kufufua uchumi husika. Hii ni kwa sababu serikali inapokumbana na hali hiyo huanza kuanzisha kodi nyingi kwa watu, na taasisi ili kupunguza obwe la matumizi mengi ya shughuli za uendeshaji wa serikali. Ili serikali iweze kushughulikia suala kama hili umakini wa mikakati wa kuweka mzani sawa wa mapato na matumizi lazima uzingatiwe. (Mwaandishi, 2021)

1.4 Afya​

Umakini katika mikakati ya kiafya lazima uwekezaji katika tafiti mbalimbali ambazo zinaweza kuondoa changamoto nyingi kwa kujibu masuluisho mbalimbali ya changamoto (magonjwa) za kiafya. Umakini katika Mikakati pia katika upande wa Afya ni kuanzisha utamaduni kwa wananchi kujijengea utamaduni wa mazoezi na kula vyakula vyenye virutubisho vizuri ili kulinda afya zao ili wawe na uwezo wa kufanya kazi bila changamoto za kiafya. (Mwaandishi, 2021)

1.5 Maendeleo ya Jamii​

Maendeleo ya jamii kama vile kuhamasisha wananchi katika shughuli mbalimbali za kiujariliamali ili kujiinua kiuchumi zinahitaji pia umakini wa mikakati. Mara nyingi jamii hukosa elimu mzuri ya ujasiriamali hasa katika suala la matumizi ya mikopo ambayo huwaletea changamoto za kiuchumi kwa kuchanganya fedha za mitaji ya ujasiriamali na biashara na matumizi binafsi hivyo kujikuta shughuli za kimaendeleo katika jamii kukwama. Hivyo ili jamii iwe na maendeleo wengi wanapaswa kuelimishwa kwanza kutokana na mabadiliko mbalimbali ya kisheria, kiteknolojia pia na miundombinu huwa yaaathiri shughuli za maendeleo ya kila siku ili waweze kuendana nayo kwani mara nyingi ni sababu za nje ya uwezo wa uthibiti wa mtu au taasisi. (Mwaandishi, 2021)

1.6 Utawala Bora na Uwajibikaji​

Kwa upande wa Serikali utawala bora ni ule ambao huzingatia sheria, taratibu, kanuni na miongozo ambayo huzingatia demokrasia. Na kwa upande wa makampuni utawala bora hufaamika kama (corporate governance) ambao unaweka mamlaka za udhibiti na ufuatiliaji wa utekelezaji wa sheria na taratibu za ndani na nje ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali. Umakini wa Kimkakati katika Utawala Bora ni kuweka namna watu wanaweza simamia sheria ambazo haziwezi kuingiliwa na matakwa ya kisiasa na wala ushawishi wa mataifa ya nje kwani changamoto nyingi zinazojitokeza kutokana na muingiliano wa mambo yanayohusiana na siasa na sera za mataifa ya nje. Ili kuweza kujenga utawala bora mzuri mkakati mzuri ni wa kuweka umakini katika uwajibikaji wa kuzingatiwa sheria zilizopo ambazo hazionyeshi upendeleo wowote kulingana na mamlaka husika. (Mwaandishi, 2021)

1.7 Demokrasia​

Demokrasia imekuwa pia ni changamoto katika katika nchi zinazoendelea kwa watawala kukandamiza uhuru wa watu kuongea na kung’ang’ania madaraka. Umakini wa Mkakati wa kuweka Demokrasia mzuri ni ule wa kuruhusu maoni yanayojenga kuliko kuwa na tafsri ya maoni tofauti kama ni upinzani. Mfano ili kujenga Demokrasia uanzishaji wa midahalo ya maoni mbalimbali ambayo hayavunji sheria na ya kujenga lazima yazingatiwe. (Mwaandishi, 2021)

1.8 Kilimo​

Mkakati makini ni wa kuanzisha kilimo cha uzalishali wa mahitaji ya malighafi ya kwenye viwanda ambavyo huzalisha bidhaa za mahitaji ya raia husika hii itasaidia viwanda kuzalisha zaidi na kupeleka mahitaji ya bidhaa sokoni hivyo nadharia ya kiuchumi ya mahitaji na upelekwaji bidhaa sokoni kufanya kazi ipasavyo. Licha ya mahitaji ya malighafi kilimo pia kinasaidia kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula ambayo huwasaidia watu kufanya kazi. Kwa Mkakati makini kila mtu na taifa kunahitajika utamaduni wa kujiwekea akiba ambayo inatosheleza ya chakula ili kupambana na changamoto ya changamoto ya njaa inayosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo huikumba dunia mara kwa mara. (Mwaandishi, 2021)

1.9 Sayansi na Technolojia​

Dunia ya sasa inategemea teknolojia na sayansi katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo. Mkakati makini wa kuwekeza katika sayansi na teknolojia ni kuanzisha wakala wa teknolojia na sayansi ambayo itatambua ubunifu katika nyanja mbalimbali kama vile za kwenye kilimo, afya, habari, michezo na biashara na sekta nyingine nyingi ili kuwezesha urahisishaji wa utendaji. (Mwaandishi, 2021)

1.10 Usafirishaji, Mizigo na Ugavi​

Sekta ya usafirishaji katika Maji, Anga, na Nchi kavu, zinahitaji umakini wa kimkakati pia ambao utasaidia kuweka mazingira thabiti ya kusafirisha uhitaji wa bidhaa au malighafi ambayo au hayatoshelezi an hazipatikani kwa mahitaji ya nchi husika. Tanzania japo ina usafiri wa Anga, Maji na nchi Kavu bado sera za uendeshaji wa huduma husika hazijakuwa rafiki kwa washikadau hivyo sera zinatakiwa zipitiwe tena na kufahamu changamoto zilizopo ili zifanyiwe kazi. Lakini pia miundo mbinu lazima itengenezewe mbadala endapo upande mmoja wa usafisharishaji unaposumbua basi kuwe na njia mbadala ambayo haiathiri hali iliyojitokeza kwa uharaka na ufanikishaji wa mahitaji. Tukiwa na mikakati yenye njia mbadala basi umakini wa kuweka mikakati utakuwa umezingatiwa na kuondoa changamoto hizo. (Mwaandishi, 2021)

1.11 Haki za Binadamu​

Haki za bainadamu ni eneo ambalo linaleta changamoto katika dunia ya sasa hasa kulingana na muingiliano wa tamaduni mbalimbali ambazo zimeletwa na utandawazi. Masuala kama vile uhuru wa kujieleza, ushoga, mauaji yasiyo ya hiari, wafungwa kukosa haki ya ndoa kwa baadhi ya nchi na uhalifu wa kivita katika baadhi ya nchi na uhuru wa kuabudu ni baadhi ya mambo ambayo haki za kibinadamu kwa sasa huongelewa sana na yanaleta mkanganyiko mkubwa kutokana na kutokuwa na sera moja ya makubaliano ya watu kutokana na tamaduni tofauti tofauuti. Umakini katika mkakati wa Haki za Binadamu nchi husika inatakiwa iweke sheria ambayo inazingatia utamaduni wa watu husika na imekubaliwa na raia wengi wa nchi husika. Hii itasaidia kuondoa mkanganyiko na matwakwa ya kimataifa ambayo hulazimishwa kuwa na umoja wa haki za binadamu ambazo jamii nyingine haizikubali. (Mwaandishi, 2021)

1.12 Hitimisho​

Hivyo basi kwa nchi yeyote inayohitaji kufanikisha harakati za maendeleo yenye tija endelevu basi suala la kupambana katika umakini kwenye mikakati ni muhimu sana kwani husaidia kutatua changamoto zinazotabilika na zisizotabilika ambazo huweza kuathiri vizuri au vibaya maendeleo ya nchi husika.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom