VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,365
G hili lipo sana kuna watu wana ngekewa zao everything they touch turns to gold.
furaha, amani na upendo...ndio maneno makuu mliyoyagusia Gaijin na JouneGwalu...
mmewahi kufikiria ili kufikia hiyo furaha, amani na upendo mnahitajika kupitia njia gani
ambayo/ambazo unaweza kumbana na vikwazo vya aina kwa aina?
je, mnakabiliana vipi na changamoto hizo...!
........aiseee hapa sijui hata nisemeje!! Unaweza kuwa na pesa ukafikiri utafanikiwa kimaisha, lakini ikawa tabu.......huwezi hata kulala vizuri unafikiria mali zako.
Nikisema furaha, furaha haiji bila uhakika wa kula, kulala, na kuvaa vizuri....... ukisema elimu nayo, vile vile tu unaweza ukawa nayo ila afya ikawa mgogoro.Huku kufanikiwa kimaisha ni kupana sana, naweza kujadili hata kurasa 10 hapa.
.....Mie nadhani kufanikiwa kwangu kimaisha ni kuridhika na nilivyo, nilichonacho na uzima Mungu alionijalia.
msafi, aksante sana kwa angalizo hilo. Kusudio la kuishi........................ hivi ni wangapi wanjua makusudio yao?! Mie kusema ukweli nakiri kuwa weak wenye hii angle. Nadhani ndio maana mambo hayako sawa, I need a therapy.
Happiness kwa mimi na wale walionizunguka....
Kutumia kile nilichonacho / takachokipata, kuleta mabadiliko chanya from A to B (no matter how high or low that B is so long as its higher than A)
Dunia uwanja wa fujo...
Hakuna happiness..(umeme, bad news, oppression, work hard less pay, fraud, etc..)
I am thinking to quit and look for a Garden (a promised garden heaven)
How to have a garden is my happiness
...what if?....ukishindwa ku fulfil hizo 'multitasks' unajihesabu hujapata mafanikio maishani?
au nawe ni katika wale wanao accept their fates?
Mkuu unajua issue inategemea na talent ya mtu.., mfano ningekuwa na kipaji (potential) kama ya Messi alafu nikacheza ligi daraja la nne, au ningekuwa naweza kuimba kama Michael Jackson alafu nisitoe Single.., au Kuandika Vitabu kama Sydney Sheldon alafu nisiandike kitabu....!! Then siwezi kusema nimefanikiwa...
Its all about potential ya mtu.., na nikiweza kufanikisha hio potential isiwe kwa faida yangu tu wala isilete karaha kwa watu...
Lakini in really life most of us are average.., kwahiyo having a normal average life, bila kuwa mzigo kwa wanaokuzunguka na ku-play your part kwenye jamii (even if ni kusafisha vyoo au kuchimba makaburi) ni mafanikio katika maisha...
Sababu mafanikio hayawezi yakawa equated na monetary au status value.., bali ni ku-accomplish what you started in life.. (be it kuchimba vyoo, basi chimba vyoo vizuri na penda shughuli yako na kuleta furaha kwa wanao kuzunguka)
........aiseee hapa sijui hata nisemeje!! Unaweza kuwa na pesa ukafikiri utafanikiwa kimaisha, lakini ikawa tabu.......huwezi hata kulala vizuri unafikiria mali zako.
Nikisema furaha, furaha haiji bila uhakika wa kula, kulala, na kuvaa vizuri....... ukisema elimu nayo, vile vile tu unaweza ukawa nayo ila afya ikawa mgogoro. Huku kufanikiwa kimaisha ni kupana sana, naweza kujadili hata kurasa 10 hapa.
.....Mie nadhani kufanikiwa kwangu kimaisha ni kuridhika na nilivyo, nilichonacho na uzima Mungu alionijalia.
...lol...hahahahahaahah!....
maendeleo na mafanikio ni kitu kimoja?
VOR
utajijuaje kama wwe ni average tu? unapimaje kipawa chako?
Rocky are you saying kua mpaka hapo ulipo bado kabisa hujapata hata kijihisia kua kitu fulani ama mahala fulani ndo utaona umefanikiwa??
Potential huwa inaonekana wakati watu tunakuwa tangia wadogo.., kuna vitu huwa ni vyepesi sana kwetu kuliko wengine ila tu katika kukua unakuta mtu unaloose the way.
Au mtu sababu ya ulevi, au mambo ya kidunia kuanguka au kuacha kile alichokuwa anakifanya vizuri na kupotea njia.
Ingawa ukweli ni kwamba persistent kwa kila mtu akifanya anafanikiwa ila wengi huwa tunakata tamaa (lakini kukata kwetu tamaa kusifanye tuishi au kuwa mzigo kwa wengine) na tukifanya hayo tutakuwa tumefanikiwa in the eyes of an average community.
Na kuhusu kipawa chako bila kujaribu huwezi kujua kwahiyo kama unapenda kuimba, imba watu wakipenda nyimbo zako then una kipaji.., lakini ukiimba single kama moja alafu ukaanza kubwia unga na kunywa pombe hadi ukaharibu kazi zako nadhani utakuwa hujafanikiwa kwenye maisha..
nadhani unakubaliana na mimi kwamba "There is Nothing Worse than Wasted Talent.."
Hii topic nimejikuta nakumbuka maneno kwenye wimbo wa BRYAN WHITE
I guess I must be wishing on
Someone else's star
It seems like someone else keeps getting
What I'm wishing for
Why can't I be as lucky
As those other people are
I guess I must be wishing
On someone else's star
Unalosema ni kweli sio tu kwa wasichana hata wavulana kuna kitu kinaitwa UTHUBUTU nakumbuka kuna kipindi niliona kazi wanahitaji Project Manager at first nilipoona vigezo kwanza nilichoka nikasema that's not for me maana niliona zile qualification ziko juu sana lakini baadae sijui kitu gani kiliniijia kichwani nika-apply nilishangaa nilipopigiwa simu kuitwa kwenye interview of 20 people tulioomba walikuwa wanahitaji mtu mmoja tu but nafikiri kule kujiamini kwangu ndiko kulinifanya nipate, kwahiyo nafikiri tukiwa na uthubutu kwenye jambo lolote i believe you'll succeed]Nakubali potential inaonekana tokea wadogo na saa nyengine unakuja kugundua kuwa wewe ni hodari wa kitu fulani lakini hili la kutojaribu ndilo linalosababisha wasichana wengi wakatae kusoma masomo ya sayansi wakisema wao hawawezi japo hawajaweka effort
[/COLOR]
General speaking, kwa bidii ndogo tu majority ya watu wanaweza kufanya vitu vikubwa, lakini wengi hatufanyi kwa vile ama hatujiamini au tunaridhika kirahisi na tulichonacho.
Siwezi kusema ni mbaya kwa vile wasipofanya huwa wana furaha na wameridhika kwa hiyo kwa definition niliyoitoa (mmmh!!??) wanajiona kuwa weshafanikiwa though sisi tuliomzunguka tunaewza kuona kuwa ni wasted talent
Unajua Gaijin nilisoma lyrics za huu wimbo nikaanza kujiuliza what was in his mind alipokuwa anaandika na mawazo kama hayo yaki-dwell in your mind chochote utakachofanya utaona it's nothing at allhapo Mkuu umenipoteza, mimi mawazo ya aina hiyo sijawahi kuwa nayo. (My pasture is always green?? au ndio kuridhika tu)