SoC02 Mafanikio kupitia mtazamo chanya

SoC02 Mafanikio kupitia mtazamo chanya

Stories of Change - 2022 Competition

Costomino

New Member
Joined
Nov 29, 2019
Posts
2
Reaction score
0
Je una tatizo? hilo ni jambojema!.
Je una tatizo? Na ni jambo jema kwanini?

Kwasababu utatuzi wa matatizo yako unakuletea mafanikio makubwa katika maisha yako.

Kila mmoja wetu ana matatizo ndo maana kila kitu katika ulimwengu kipo katika hali ya kubadilika.Kitu cha muhimu ni kwamba, mafanikio yako yanategemea mtazamo wako wa akili kukabiliana na changamoto.

Kutatua tatizo lako inategemea hasa mitazamo miwili ya akilia ,mtazamo chanya au hasi. Ukitumia mtazamochanya kutatua kila changamoto ndipo utakapofanikiwa katika kila tatizo unalokutana nalo katika maisha yako.

Ni namna gani ya kutatua tatizo kupitia mtazamo chanya wa akili? kama unamwamini Mungu, SIKU ZOTE MUNGU NI MWEMA.

Soma stori ya kijana Costo alivyo fanikiwa kwa kupitia mtazamo chanya wa akili.

Costo alizaliwa katika familia masikini sana. Alipokuwa shule ya sekondari aliuza magazeti na kushona viatu ili kutimiza haja ya chakula na malazi ya mama yake. Baada ya kuhitimu elimu ya chuo kikuu aliamua kwenda mjini kutafuta maisha.Mjini kampani yake kubwa ilikuwa ya wacheza kamari na vibaka( vijana walio kuwa wakifahamika kama wahuni au mateja).

Costo alisema "kosa langu kubwa ni kuwa katika kundi lisilo sahihi, dhambi yangu kubwa ni kushirikiana na watu wabaya."

Kila muda alikuwa akishinda kamari za pesa nyingi na alikuwa akizipoteza bila kufanya chochote.Na hatimaye alikamatwa kwa madai ya utumiaji wa madawa ya kulevya(bangi,cocaine na heroine) na kuhukumiwa kwenda jela.

Costo alikuwa na umri wa miaka thelathini na nne alivyohukumiwa kwenda jela.Hakuwahi kwenda jela hapo kabla.

Gerezani hapakuwa na yeyote shupavu kama yeye ,hakuna wa kumtishia wala kumwambia chochote,kwani gerezani huwa wakinyanyaswa na kuonewa na wengine kulawitiwa kabisa,lakini kwa Costo haikuwa hivyo, hali iliyo mfanya kufikiria kutoroka .

Lakini kabla ya kutoroka Costo alifikiri kitu! Aliamua kubadili mtazamo hasi kuwa mtazamo chanya.Alikutana na changamoto la kutatua kupitia mtazamo chanya wa akili. Kuna kitu ndani yake ikamsemesha kwamba badala ya kuwa mkaidi badala yake awe mnyenyekevu na mfungwa bora ndani ya lile gereza.

Kwa kubadili mtazamo wake kutoka mtazamo hasi kwenda mtazamo chanya wa akili ,Costo aliona maisha yamekuwa mepesi ndaniya gereza lile.

Costo aliamua kubadilika,akamsamehe askari aliemkamata pamoja na jaji alie toa hukumu yake ya kufungwa.

Alimua kubadilisha mwonekano wake wa ukatili na uhuni wa zamani na kuwa mfungwa mwema pale gerezani.
Kwanza kabisa alijiuliza maswali kadha wa kadha. Kipindi cha ujana wake alipata jibu kwenye kitabu kimoja.Kitabu hicho ni BIBLIA.Hadi alipoaga dunia miaka sabini na tatu Costo alisoma biblia kila siku.

Kwa kuwa alibadili mtazamo wake wa akili Costo alikuwa mfungwa alie pendwa na askari magereza na kupewa nafasi ya kuwaongoza wengine.(Mnyapara).

Costo na wafungwa baadhi walipata fursa ya kwenda kutengeneza daraja lilokuwa mbali kidogo na gereza lao. Kwa kawaida hii huwa ni fursa adimu na ya bahati sana kwa wafungwa.

Costo kwa vile aliamua kutumia mtazamo chanya wa akili, alifanya kazi kwa juhudi kubwa sana hali iliyo wafurahisha askari ,na hata waziri wa miundombinu alistaajabishwa mno na juhudi za Costo alipo kwenda kutembelea maendeleo ya kazi hapo darajani. Ndipo waziri alipo muahidi Costo ya kwamba ukitoka gerezani uje nikupatie kazi.

Baada ya wiki tano Costo aliachiliwa huru,ndipo alipomtafuta yule waziri kama alivyo muahidi ,akapewa kazi alio lipwa shilingi elfu tano kwa siku. Ni kiasi kidogo sana kwa vile Costo alitumia mtazamo chanya wa akili alivumilia na hatimae kupandishwa cheo na mshahara baada ya miaka tatu mbele.

Kampuni ilikuwa kubwa na kupata faida kila mwaka, hata yule waziri alipo fariki Costo akawa meneja wa lile kampuni. Costo hatokuja kusahau maisha magumu aliopitia kipindi cha ujana wake hali iliyomfanya apambane kwa juhudi ya hali ya juu.

Funzo:
Costo alipata tatizo,Hilo ni jambo zuri!

Kwa sababu aliitatua changamoto hilo kwa mtazamo chanya wa akili ,ndo kisa cha kufanikiwa kwake.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom